Adverts

Apr 20, 2009

MRISHO NGASSA KAKWAMA LAKINI KESHA TUTANGAZA

NGASSA PAMOJA NA KUSHINDWA, KESHA TUTANGAZA Habari nilizozipata hivi punde ni kuwa Ngassa ameshidwa kufuzu kwenye majaribio kwa nujibu wa wakala wake Yusufu Bakhresa ni kuwa ameshindwa kupita kwenye mchujo wa wachezaji wengine 14 waliokuwa wanawania nafasi 3 tu kujiunga na kikosi cha Gianfranco Zola. Hata hivyo Ngasa aliaenza majaribia hayo jumatatu iliyopita kwa kufanya mazoezi na reserve team ya West Ham United alipandinshwa siku ya Alhamisi iliyopita kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza kinachoshiriki ligi kuu Uingereza.Hizi ni habari sa kusikitisha lakini Ngassa anapaswa asife moyo kwani wakala wako yuko kwenye mazungumzo na team ya Fulham kuona kama anaweza kupata nafasi ya kufanya majaribio na team hiyo au hata timu nyingine nchini humo.Pia afahamu kuwa amefungua njia ya soka letu kukua na kujitangaza kimataifa maana hata kipindi cha Soccer Africa cha wiki hii walimzungumzia na kumtakia kila la kheri. Usife moyo Ngassa safari ndio kwanza imeanza na umri bado unakuruhusu