Adverts

Sep 29, 2010

HIZI NDIYO MBWEMBWE ZETU WATU WA VIJIJINI

 Wakati nyie huko mijini mpaka sijui muende klabu sijui mnaita casinoni sijui  wapi siye huku vijijini burudani zetu ni hizi! waangalie wajanja wetu wakiwa wamepiga tinted halafu na jina la kijiji kwenye paji la uso wakimaanisha ni wazalendo zaidi!!! mjini utakuta mtu amevaa sijui Justin Timberland, Tupac nk huku sisi ni uzalendo zaidi!.
 Midadi ikitupanda  huwa tunamwaga radhi, sema tu mshukuru kuna watoto wanatembelea blog hii vinginevyo ningeachia tu !!!!!!!
Halafu nani kakwambia ngoma inachezwa bila wazee? lazima palipo wazee haliharibiki neno!!!