Adverts

Sep 29, 2010

HIZI NDIZO HARUSI ZETU VIJIJINI

Mmoja wa wadau wa karibu na blog hii akiwa kwenye mwinuko mkali kutoka upande wa pili wa mto  huko Ileje hii ilikuwa ni baada ya kufunga pingu za maisha  na kwa kuwa huku kwetu vijijini magari yanaachwa upande wa pili yaani ng'ambo ya mto kutokana na masuala  mazima ya miundo mbinu  basi ilibidi Bi Harusi atambulishwe kwa staili hii kuwa  nyumbani ni nyumbani hataka kama hatupandi magari!!!!

Baada ya hapo tulimpitisha kwenye vitindi vya Ulanzi -wenyewe tunaita kwenye mianzi na kumtambulisha rasmi kuwa hapa ndipo tulipokulia na kilikuwa kinywaji chetu cha kila wakati tulipojisikia kuondoa uchovu wa mazingira yetu hatarishi basi tulizima stim na ulabu kidogo na nchi ikaendelea kuwa nzuri mpaka leo!