Adverts

Sep 30, 2010

KAKOBE AKANA KUHUBIRI SIASA KANISANI

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF),Zachary Kakobe amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kumzushia uongo kuwa amekuwa akifanya kampeni kwenye kanisa lake.
Akizungumza  leo asubuhi, mchungaji Kakobe amesema kuwa hawezi kufanya kitendo hicho kwani anafahamu haki ya kila raia.
“Mimi siwezi kumpigia mtu kampeni isipokuwa Jumapili iliyopita nilikuwa nikitoa elimu ya uraia kwa waumini waungu ili kujua haki na wajibu wao katika siku ya kupiga kura, ” amesema.
Mchungaji Kakobe amesema kuwa katika siku hiyo kulikuwa na wagombea mbalimbali kutoka katika vyama siasa kwenye ibada.
Amesema kuwa aliamua kutoa elimu ya uraia kwa waumini wake ili kutekeleza agizo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) la kila kiongozi kutoa elimu ya uraia kwa watu wake.
“Mimi nilikuwa natimiza agizo la NEC kwani kitendo cha mtu kumpigia kura mtu ni cha utashi wake mwenyewe na siwezi kumlazimisha mtu amchague mtu fulani, ” amesema Kakobe.
Amesema kuwa kuna baadhgi ya watu wana mambo yao ambapo wamekuwa wakitengeneza jambo bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha.
Hata hivyo Kakobe amesema kuwa wakati huu ni muhimu hivyo kitendo cha kutengeneza jambo na kulizungumza hadharani si kizuri.
Jana Taasisi ya Maimamu ya Bukhary ya Kiislam inayoongozwa na Sheke Khalifa Khamisi ilitoa tamko la kumkanya Askofu Kakobe kuacha ushabiki wa kisiasa ndani ya kanisa kwa kitendo cha kuwataka waumini wake kumchagua mgombea fulani.
Katika taarifa ya taasisi hiyo ilisema kuwa kitendo cha askofu huyo kufanya hivyo kinaweza kuhatarisha amani nchini.