Adverts

Oct 31, 2010

Oct 28, 2010

Njoo ufanyiwe maombi

Mhubiri akifanya huduma zake  kwa staili ya nyumba kwa nyumba  kama iliovyo kampeni za siasa bongo, hapa akiwa madukani Tunduma akitoa huduma kwa wafanyabiashara. indaba2010

punddq qfe mzigo ufike

indaba2010

haya ndiyo maisha ya kawaida, siyo mnakuja na benzi baada ya siku mbili mnaachana!

picha nimelamba kwenye mtandao wa face book ahsante Mwaissango kwa kutupa vitu kama hivi

HAWA WANASAKA MAISHA SIYO MABOX

indaba2010

MPUNGA HUU UNALIWA NA WAZAMBIA KULIKO WABONGO

shehena ya mpunga ikishushwa  mashineni katika eneo la Karoleni Tunduma tayari kwaajili ya biashara ya mchele kwa wazambia ambao ndiyo wateja wakubwa katika eneo hilo^mpakani.

JAMANI BEI NZURI YA MAYAI YA KIENYEJI YAPO HUKU VIJIJINI

Mayai ya kienyeji bei yake ni 250 kwa moja wasiliana  nasi kwa nambari hapo juu kona ya kulia hata kama unataka trey 1000.

NAUZA NAUZA NAUZA

haya nauza nauza  hivi ndivyo biashara haigombi katika eneo la Tunduma, eneo hili maarufu kama black market hata mafuta ya ndege yanapatikana hapa

Mtaa wa Kongo katika mji wa Tunduma

Wadau wa blog hii wakiwa katika mitaa ya border ya Tunduma kufanya shopping kabla ya siku ya uchaguzi manake kwa eneo la Tunduma huwa mambo hayatabiriki, watu wameshaanza kununua mchele,unga na bidhaa za chakula kujihami na vijimambo vya mpakani, wakati ambapo tayari jeshi la polisi nalo limeweka lile gari maarufu kama kojozi kwaajili ya rasha rasha za election2010

SHAMBA LA EKARI MIA TANO LINAUZWA MBOZI

Ndugu watanzania, shamba kubwa lenye ukubwa wa ekari 500 lipo wilayani Mbozi kilometa 9 kutoka kwenye lami linalofaa kwa kilimo cha Ngano/shayiri, kahawa, mahindi na viazi.  wasiliana  na muuzaji kupitia namba iliyopo kwenye utangulizi wa blog hii hapo juu, tutakuunganisha na muuzaji.

Tundumq na bajaj mpaka lini?

huu ndiyo usafiri wa kila siku Tunduma inakadiriwa kuwa kila bajaj wastani kwa siku hulaza mapato kati ya shilingi 20,000 hadi 30,000 hizi ni zile zinazopelekwa kwa wamiliki wake achilia mbali walizobana madereva wake

Kiatu kinachoitwa bajaj kinavyowatoa chicha akina dada

Kiatu kinachoonekana hapo juu ndicho kinachovaliwa na watanzania wanawake wengi ikilinganishwa na viatu aina zingine vilivyotengenezwa na viwanda vya wachina vilivyopo hapa nchini na nje ya nchi, wakati wanaume wengi wakiwa wamevaa yebo yebo!

Mkemia wa umri mdogo akifanya uchakachuaji wa maji Tunduma

Mkemia kutoka mitaa ya Tunduma akijaribu kufanya uchakachuaji wa maji katika moja ya mitaa ya Tunduma, haifahamiki alikuwa analenga kufanya nini katika utafiti wake na matokeo yake atayatangaza wapi.
Hivi ndivyo jamaa wa yebo yebo Tunduma wanavyofanya, wengi wao leseni zao ni vitambulisho vya kupigia kura hivyo hawafahamu taratibu za barabarani, jamaa ameamua kutuma meseji katikati ya barabara katika eneo la kona ya Shangazi hotel jana mchana.

Oct 27, 2010

MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU MBOZI


Vifaa kwaajili ya uchaguzi mkuu 2010 vikiwa vimewekwa nje ya bohari kuu ya halmashauri ya wilaya ya mbozi tayari kusambazwa kwenye vijiji na kata.

Oct 25, 2010

TAARIFA KUTOKA SCOAN(TB JOSHUA JUU YA UNABII WA UCHAGUZI WA BONGO FEKI!!!!

Katika siku za hivi karibuni kulizuka uvumi nchini kwamba TB Joshua ametoa unabii kuhusiana na uchaguzi mkuu wa Tanzania kwa mwaka 2010,  anchor wa mtandao huu baada ya kufuatilia kwa muda kwenye vipindi vyake hakuona chochote na hivyo kulazimika kumwandikia TB joshua kutaka ufafanuzi kupitia official website yake ya www. scoan.org  haya ni sehemu ya majibu aliyonipa kupitia e mail yangu.
To: http://de.mc526.mail.yahoo.com/mc/compose?to=dtweve1@yahoo.com
Sent: Wed Oct 20th, 2010 6:58 AM PDT
Subject: IMPORTANT NOTICE

Calvary greetings in the mighty name of Jesus Christfrom The Synagogue, Church Of All Nations.

We have received inquiries from various persons inTanzania regarding a rumour that is being spread throughout the countryconcerning Tanzania’s upcoming elections. The rumour states that a prophecy wasgiven by Prophet T.B. Joshua concerning these elections and the partiesinvolved.

We, The Synagogue, Church Of All Nations, hereby statethat there was no prophecy given by Prophet T.B. Joshua regarding Tanzania, hergovernment, or her people.
Please note with utmost importance: If a prophecy hasbeen revealed by Prophet T.B. Joshua, it will first be broadcast on Emmanuel TVand subsequently posted on our websites: www.scoan.org (http://www.scoan.org/)and www.emmanuel.tv (http://www.emmanuel.tv/)

We continue to keep the nation of Tanzania, her peopleand her leaders in prayer. For the only way to show someone you love them is bypraying for them. We love the nation of Tanzania and believe, by God’s grace,that the best is yet to come.

Emmanuel! God is with us!

The SCOAN
www.scoan.org
info@scoan.org

KWETU KUDUNDANA NI SEHEMU YA JANDO

Haya ni maisha ya kila siku kwa vijana waliopigika vijiweni, wanapodhulumiana hata shilingi 50/= ya sigara mambo huwa hivi kila siku. Ndiyo sababu kazi ya polisi kukamata vibaka inakuwa nyepesi kwakuwa kwa kuwaaangalia tu makovu usoni utabaini kuwa hawa ni watu waliozoea vipigo!!!!! hapa ilikuwa ni kituo cha mabasi cha Vwawa makaburini Jumamosi iliyopita.

WADAU VALUE FOR MONEY WANAPOPOZI KWA FOTO!!!

Jamaa wa idara ya ukaguzi wa ndani katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi (Kama wanavyofahamika kwa jina la utani la Value for money) wakiwa ngangali kinoma nje ya mjengo wa halmashauri hiyo baada ya kurejea kutoka shughuli za vijijini ambako kunahitaji usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa program mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa kupitia halmashauri hiyo. Kuanzia kulia ni dada  nani hii, akifuatiwa na Sheikh Waziri Mwasa, Girlbert Rwehumbiza na Maganga Henze

WADAU NAO WALIKUWEPO

 Kuanzia kulia ni Dr Charles  Mkombachepa(mganga mkuu wa wilaya ya mbozi), Papa, Mwanasheria wa mji mdogo wa Tunduma Mwasalemba wakiwa kwenye pozi la picha katika harakati za kukabidhiana magari ya taka.
Hii ni sehemu tu ya mambo ya taka zinazozalishwa na wakazi wa mji wa Tunduma, wastani wa tani 37 huzalishwa kila wiki katika mji wa Tunduma hali ambapo uzoaji wake hapo awali ulikuwa kati ya Tani 15,000 hadi 20,000. Baada ya kupatikana magari haya mawili hali ya mambo inatarajiwa kubadilika na kuwa bomba sana man!!!!!!!!!!!!!!

CHILEWA AKIFANYA MAJARIBIO KWENYE MOJA YA MAGARI YA TAKA

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Levison Chillewa akijaribu kuwasha moja ya magari yaliyotolewa kusaidia shughuli za usafi katika mji mdogo wa Tunduma ambao upo mpakani mwa Tanzania na Zambia.

MAANDALIZI YA WEKA TUNDUMA SAFI YAANZA

Kampeni kubwa ya kuufanya mji wa Tunduma kuwa safi ikiwa ni harakati za kuiondoa aibu kwenye macho ya nchi jirani kutokana na hali ya uchafu wa mji huo hapo awali- sasa imepamba moto baada ya halmashauri mama ya wilaya ya Mbozi kuamua kuusaidia mji mdogo wa Tunduma magari  mapya mawili ya kuzoa taka yaliyonunuliwa kwa zaidi ya milion 150. Huu ni mfano mzuri kwa miji mingine katika kuhakikisha suala ya la usafi wa mazingira kuwa moja ya maeneo ya kimkakati. Tunduma ingawa ni sehemu ya eneo la wilaua ya Mbozi bado shughuli zake za kiuchumi kwa sehemu kubwa zinachangia mapato ya moja kwa moja kwenye serikali kuu (HAZINA) lakini  wananchi wanahoji kiasi gani kinarejeshwa kwa uhalibifu wa mazingira unaofanywa na shughuli hizo kwenye eneo hilo kwa ujumla? manake maambukizi ya HIV kwa sehemu kubwa yanachangiwa na shughuli hizo za border post  any way tupo kwenye majadiliano karibuni

Christian naye ana matumaini na Tanzania ijayo

Ingawa mama yake anaonekana kama anaelekea kukata tamaa kwa jinsi ninavyoendesha serikali ya familia yangu  lakini kijana wangu Christian anaonekana ana matumaini makubwa na serikali yangu baba yake! Nakutakia maisha marefu na yenye busara na neema mwanangu Christian

Oct 5, 2010

UWANJA WA AMANI ZANZIBAR UPO TAYARI KUTUMIKA

Baada ya ukarabati wa kampuni kutoka China, uwanja wa amani unaonekana murua ukiwa umewekwa zuria kwenye eneo la kukimbilia huku hoteli zake zikiwa saafi baada ya ukarabati mkubwa: picha kwa kudesa kutoka issamichuzi blog

Oct 4, 2010

PM AKIWA NA BAN Ki Moon septemba 27,2010

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana huku akipiga picha na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kabla ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za Umoja huo jijiniNew York Septemba 27, 2010. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye umoja wa Mataifa.indaba2010

MAMBO YA FEDE KWENYE MTANDAO WA KATUNI

Mtembelee Mtaalam wa katuni hizi za kisiasa na kijamii na nyanja nyingine muhimu katika 
.BLOG: www.artsfede.blogspot.com.
indaba2010

Morooooooooooooooooooobwana

indaba2010

ETI WANAWAKE HAWABEEP!!! JAMANI WAPENI FULSA

Ujumbe umefika watoto eeeeeeee(indaba2010)

BARUA YA MTOTO KWA MWENYEZI MUNGU

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 alikuwa anahitaji sana shilingi 100,000
(Laki moja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake
akamwambia "muombe Mungu atakupatia.  Mtoto alianza kuomba kila siku na kila
mara lakini  hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia  uamuzi wa
kumuandikia barua Mungu ili asome maombi  yake.

Kisha akai-post barua ile.  Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua
kwa
ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona  bahasha iliyoandikwa
"Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali pa kuipeleka, Wakaamua
kuifungua.

Barua ilisomeka hivi:
"Mpendwa Mungu,

Jina langu ni EMMANUELEY, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la tatu
katika
jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania ,  bara la Africa .

Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja baada ya
kuomba bila kupata majibu toka kwako.
Naomba sana unisaidie kwani mimi ni mtoto mdogo na sina uwezo wa kufanya
kazi na
kupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu ni maskini
sana .

Natanguliza shukrani.

Wako mtiifu,
EMMA."


Wafanyakazi wa posta walifurahishwa sana na barua hiyo na kisha wakaamua
waipeleke kwa Rais . Rais  naye alipoipokea ilimfurahisha
sana na
kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto huyo akidhani
kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingi sana .
Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:
"Mpendwa Mungu wangu,

Nashukuru sana kwa kusikiliza maombi yangu na kunitumia pesa nilizokuomba.
Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu ya Tanzania .Kama ilivyo kawaida yao, wamekata kiasi cha sh. 98,000 kwa ajili ya kodi , kwa hiyo wameniletea Sh. 2000 tu

MAMBO YA MUSTAPHA HASSANALI

 Designers listerning to Patrick Lumumba of the Production Facility they visited on 30 September 2010.
Designers attending how the pattern drafting works

Picha kupitia mtandao wake.

UNAKUMBUA ENZI ZA BUJAGA IZENGO KADAGO?

Hii ni taarifa ya habari kutoka Radio Tanzania Dar es salaam  Msomaji ni BUJAGA IZENGO KADAGO" huyu ndiye askofu wa sasa namkumbuka sana mdau huyu kwa vichekesho balaa! hongera mdau kwa kukamua shule kisawa sawa! (indaba2010)

What is Lipenenga? wazee wanawafundisha vijana

Kwenye watu wazima haliharibiki neno, Wazee kama hawa ni hazina kwa utamaduni wetu ni nadra sana kuona vijana wakiendeleza ngoma zetu za asili na matokeo yake utamaduni wa asili unazizimia na badala yake mambo ya vidole juu yoyo nyiiiiingi!! vimetawala kwenye maisha ya kila siku
indaba2010

KIJIJINI KWETU WANAFUNZI WANA NJIA NYINGI ZA KUJIFUNZA JIOGRAFIA

Kama huko mjini mnatumia ramani za Ukutani, siye huku tupo kivitendo zaidi! ramani zetu zipo physically yaani mwanafunzi anashiriki kuiandaa hadi kuitumia! si unajua soda nazo za shida hivyo mnatangaziwa kwesho kila mtu aje na visoda(vizibo) kumi sawa sawa!!!!!  basi baada ya kuleta inakuwa raw material ya ujenzi wa ramani ya africa mashariki.(indaba2010)

HII SIYO SEKONDARI YA KATA, NI PRIMARY MOJAWAPO KATI YA NYINGI ZILIZOMO MBOZI

 Jengo la shule ya msingi mojawapo iliyopo wilayani Mbozi, kwa ujumla wilaya ya Mbozi inapokuja kwenye ujenzi wa shule zake za msingi kwakweli inafagiliwa kwa namna majengo yake yalivyosimama! DED ujiko ujiko!!!!!!!
indaba2010

VIJIJINI NDIYO ZETU KILIMO NA UFUGAJI SAMAKI

Mmoja wa wananchi wa wilaya ya Mbozi aliyejengewa uwezo kupitia idara za Kilimo, Maliasili na Maji namna ya kuhifadhi raslimali maji na huku akitumia bwawa lake kwaajili ya Kilimo cha Bustani, Migomba  pamoja na ufugaji Samaki kijiji cha Igamba (indaba2010)

HUYU DOGO AKICHOKA MIKONO ANAWEZA KUSOGEZA MDOMO!

Kazi ya kukamua ng'ombe inaelekea kuhama kutoka matumizi ya vidole vya mkono hadi kwenda mdomoni manake dogo anaonekana kusogea kila dakika inavyoyeya baadaye atakamulia mdomo wake! (indaba2010

SIJASIKIA KWENYE KAMPENI WATU WAKIAHIDI KUTOA BAJAJI BURE VIJIJINI

Hivi wazee kama hawa wananyunda kwa mguu kilometa 850 kwa siku nyie mnawaangalia tu!! mbona hatuwasikii mkitoa ahadi ya kuwagawia bajaj bure? hivi mzee na yebo yebo zake hizi unadhani zitadumu kwa wiki mbili kama kila siku utaratibu ndio huo? yangu macho (indaba2010)

HAPA NDIPO MAKAO MAKUU YA WILAYA YA MBOZI

Eeebwana Ndiyo: hapa ndipo wa hapa hapa tunaishi! ndiyo makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi na pia ofisi za Mkuu wa wilaya Mbozi zimo humu humu mjengoni, vipi kwenye upande wa mazingira tunajalieeee? (indaba2010)

SASA TUMEHAMIA ILASI BUS BAADA YA WAHAPA HAPA MWINGINE KUTOKOMEA

Safari zetu kwenda mjini sasa hivi zinaaminika kupitia kampuni hii ya mzawa baada ya Mzawa mwingine kufulia sijui kufanya nini manake tunaona kama inasua sua vile! any way tunawapongeza kwa pamoja kutufanya wakazi wa Mbozi kuiona Dar Kila siku  kupitia mabasi yenu (indaba2010)

Oct 3, 2010

ENZI ZA KUREKODI HOTUBA KWA RADIO CASSETTE!!!!

Wakazi wa mjini Iringa wakirekodi moja ya mikutano ya kampeni zinazoendelea hivi punde kwa kutumia chombo hicho kipyaaaa! aina ya Aterch kama enzi za mwalimuuuu kumbe kuna recoders ndoooooogo kama pini technolojia bwana!!!

KARIBU KWA HUDUMA ZA INTERNET

Kwa huduma mbalimbali za bidhaa za ofisini, photocopy, fax na internet kwa ujumla tembelea Indaba Business Centre iliyopo mkabala na MBOCU ama wasiliana nasi kwa +255764947555. KARIBUNI SANA

KIJIWE MAARUFU CHA DRAFT MBOZI


Kijiwe hiki siku zote hukosi wadau wa draft, hapa ni ustadh -teacher akiwa anamenyana na Profesa Kipara huku wadau wengine wakifuatilia !!