Adverts

Jan 31, 2011

MUUMIN MWINJUMA ARUDI NA BWAGAMOYO SOUND.

MUUMIN MWINJUMA ARUDI NA BWAGAMOYO SOUND.: "
Muumin Mwinjuma Kocha wa Dunia kama anavyojulikana kwa jina la kimuziki akiimba jukwaani jana wakati bendi yake ya Bwagamoyo Sound ilipoisindikiza bendi ya African Stars wana Twanga Pepeta kwenye Bonanza lao linalofanyika kila siku ya jumapili kwenye viwanja vya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam, Ambapo watuo wengi waliojitokeza katika onysho hilo walionekana kuvutiwa na kibwagizo cha ghani zake za 'Nipate japo Kikombe cha Chai, Nipate japo Kikombe cha Kahawa'.
Kundi zima la Bwagamoyo Sound likiongozwa na Muumin Mwinjuma kiongozi wa bendi hiyo katika onyesho lao lililofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Wangenguaji wa kundi la Bwagamoyo Sound wakifanya vitu vyao wakati wa onyesho lao la jana kwenye bonanza la jumapili.
"