Adverts

Feb 4, 2011

MASHINDANO YA KOMBE LA MBUNGE FILIKUNJOMBE KUANZISHWA LUDEWA

MASHINDANO YA KOMBE LA MBUNGE FILIKUNJOMBE KUANZISHWA LUDEWA: " mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa Deo Haule Filikunjomb (kulia) akionyesha vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya kombe la Mbunge
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Haule Filikunjombe akikabidhi mpira kwa wanafunzi wa shule ya msingi Madunda
Wanafunzi mnaona Kombe la mbunge
Mkuu wa shule ya Sekondari Madunda akiwa ameshika kombe ambalo lilitolewa na mbunge Filikunjombe
Gari la mbunge Deo Filikunjombe likiwa limezuiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ndoa
Mbunge Filikunjombe akikabidhi mpira kwa wanafunzi wa shule ya msingi Ndoa
MASHINDANO ya kombe la mbunge wa jimbo la Ludewa kuanzishwa katika wilaya ya Ludewa mkmoani Iringa kama njia ya kuhamasisha michezo ya kupambana na gonjwa hatari la UKIMWI kwa vijana. Akikabidhi vifaa vya michezo pamoja na kombe maalum litakaloshindaniwa katika wilaya hiyo katika kijiji cha Iyunguya kata ya Mawengi wilayani humo wakati wa,mbunge wa jimbo hilo . Mbunge huyo alisema kuwa kuanzishwa kwa mashindano hayo katika wilaya ya Ludewa kutasaidia soka ndani ya wilaya hiyo kukuwa na kuweza kupata timu ya wilaya ambayo mbeleni itaweza kuchezea ligi kuu ya Voda com. Aidha alisema kuwa katika mashindano hayo ambayo yatachezwa katika ngazi ya kata ,tarafa na baadaye wilaya lengo ni kupata timu moja na kuwa kwa mshini wa ngazi ya kata atapewa zawadi ya kombe maaalum pamoja na ng’ombe mnyama kama sehemu ya zawadi ila kwa ngazi ya wilaya mshindi atazawadiwa zaidi. Pamoja kutoa vifaa hivyo vya michezo kwa vijana mchanganyiko wa CCM na wale wasio na ushabiki wa chama chochote cha siasa wakiwemo wale wa vyama vya upinzani pia alisema kuwa mashinadano hayo yatajenga umoja kwa wananchi wote hasa kwa kipindi hiki mara baada ya uchaguzi kumalizika na mbunge,Rais na madiwani kupatikana. Filikunjombe alisema kuwa hakuna sababu ya wana CCM kuwabagua wananchi ambao hawakutoa kura kwa CCM na kuwa kwa sasa uchaguzi umekwisha na wote wanapaswa kuwa kitu kimoja katika kuharakisha maendeleo. Katika hatua nyingine mbunge huyo amekabidhi vifaa vya michezo katika shule ya sekondari ya Madunda kama njia ya kuhamasisha michezo kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Kabla ya mbunge huyo kutembelea shule hiyo msafara wake ulizuiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ndoa iliyopo umbali wa Km zaidi ya 20 kutoka kijijini hapo ambao waliacha vipindi na kuja kuzuia msafara huo ili kuomba mpira.
"