Adverts

Feb 28, 2011

MTIHANI WA KCSE KENYA KUTANGAZWA LEO..!!!

"
Baraza la Taifa la Mitihani nchini Kenya leo linatangaza matokeo ya mitihani ya mwaka jana ya kumaliza elimu ya sekondari (KCSE). Matokeo hayo yanatangazwa na Waziri wa Elimu Sam Ongeri katika Taasisi ya Elimu nchini humo.
Jumla ya wanafunzi 357,488 waliofanya mitihani hiyo wanatarajia kujua hatma yao, iwapo wamefanikiwa kuendelea na Vyuo Vikuu, vyuo vya kawaida au wanalazimika kurudia mitihani ili wapate alama zinazohitajika.
Hata hivyo Wizara ya Elimu imesema mabadiliko makubwa yanatarajiwa katika mfumo wa elimu nchini humo ifikapo mwezi Julai, wakati ambapo kikosi kazi juu ya mpangilio katika sekta ya elimu kwa mujibu wa katiba mpya kitakapomaliza kazi yake.
Alliance High School students celebrate after a previous good performance in the Kenya Certificate of Secondary School (KCSE) examinations. The school emerged the top in the 2010 exams. Photo/Jennifer Muiruri
"