Adverts

Mar 31, 2011

KIJANA WA MBEYA AENDELEA KUTOA DOZI YA KUTIBU MAGONJWA SUGU

Kijana Jafari Wema ama Fikiri akigawa dozi kwa mmoja wa wakazi wa Mbeya waliojitokeza kupata huduma hiyo
Mmoja wa wasaidizi wa Mjukuu wa kiokombe akikokea moto kuchemsha dawa
Na Thompson Mpanji,Mbeya KIJANA mdogo aliyeibuka na kuanza kutoa huduma ya tiba kwa kutumia kikombe kama alivyokuwa Babu wa Kijiji cha Samunge,Wilaya ya Loliondo,Mch.Ambilikile Mwasapila ameishukuru serikali kwa kumruhusu kuendelea kutoa huduma kwa jamii lakini mizimu yake imekataa kufanya huduma hiyo nje ya nyumbani kwao kwani dawa hiyo haitafanyakazi. Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi,kijana Jafari Werna au Fikiri (17) maarufu ‘Babu mtoto wa mabatini,’alisema baada ya kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Bw.John Mwakipesile ofisini kwake alimweleza kuwa yeye ni kijana mdogo hivyo hapaswi kufanya shughuli ya uganga wa jadi hadi atimize umri wa miaka 18 na zaidi. Alisema baada ya kujieleza kuwa shughuli hizo alianza akiwa na umri mdogo kwani alikuwa amerithishwa na Bibi yake hivyo alitakiwa kukata kibali ambacho alilipiwa kiasi cha sh.55,000 baada ya viongozi wake wa mashina (mabalozi) na serikali ya Mtaa wa Mianzini anapoishi kufanya mchango huo. “Sasa naendelea kutoa huduma na wakaribisha waje wahitaji kutoka maeneo mbalimbali nje na ndani ya mikoa,nawaambia hasa wagonjwa na wenye shida mbalimbali ziwe za ukimwi na magonjwa sugu wanaoishi ndani ya mkoa wa Mbeya wawahi kwani itafika wakati watapata shida kuniona kabisa,alisema. Aliongeza,”madudu yangu yamekataa kuhama hapa na yamesema nikihama hapa hii tiba haitafanyakazi tena, wagonjwa na wahitaji waje watu wanapona na wanarudi kunishukuru,wanakunywa kikombe kimoja leo na kingine kesho basi, wanachangia Sh.200 ya kuni za kuchemshia dawa,na kama wanataka kuniona kwa shida nyingine Sh.1000, viongozi wa shina na mtaa wanaendelea kuboresha huduma na usafi ili kuondokana na magonjwa ya milipuko.” Mwandishi wa habari hizi amekuta msululu wa magari yaliyoegeshwa katika maeneo mbalimbali ya mtaa wa mianzini huku maelfu ya wananchi katika foleni wakiwa wameshika kikombe cha plastiki mkononi wangine wakiwa wamebebwa katika machela na ndugu,jamaa na marafiki. Akisimulia historia yake Jafari alisema alishindwa kumaliza masomo akiwa kidato cha kwanza mkoani morogoro baada ya kushindwa kusoma na kutokewa na maruwe ruwe na kushindwa kuona katika ubao na hivyo kurudishwa nyumbani kwa Bibi yake mzaa mama yake aliyefariki mwaka 2004 mkoani Mbeya ambapo alikabidhiwa mikoba na Bibi yake na kuanza kufanya shughuli za uganga akiwa na umri mdogo. “Baada ya mama kufariki baba alinichukuwa kwenda morogoro na huko nikashindwa kuendelea na masomo kutokana na kutokewa na vitu vya ajabu na kushindwa kuona,nikarudishwa kwa Bibi na baadaye nilipoanza uganga siku moja nilioteshwa kuna dawa ya kuponywa ukimwi na magonjwa sugo Mbozi ingawa mbozi sikujuwi nilichukuliwa na kwenda kuchimba usiku na ndiyo hii ninayotoa tiba,”alisema. Baadhi ya wananchi waliofika kupata kikombe kwa kijana Jafari wamemshukuru mungu kwa kuwaletea tabibu huyo ambaye atawasaidia hata watu wasio na uwezo wa kwenda Loliondo.
"

MTOTO AJA NA KIKOMBE CHA DAWA MOROGORO

Fatuma Sengo akimimina dawa
Habari toka Morogoro zinaeleza kuwa Ashinuri Pichuu (4) anayeishi Kichangani, ametangaza kutibu magonjwa sugu na tayari viongozi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya Ya Morogoro Mheshimiwa Mwambungu alifika kwa "mtaalamu" huyo wa kikombe kwa habari zaidi tembelea http://www.jumamtanda.blogspot.com/

"

Dotnata afanya kufuru kwa kvuta "Hummer" la nguvu

MSANII matawi ya juu katika tasnia ya filamu Bongo, Husna Mohamed Posh ‘Dotnata’ amefanya kufuru baada ya kutoa ‘burungutu’ kununua‘mkoko’ wa kifahari aina ya Hummer, Amani Jipya limeinyaka. Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali za kuukomboa mkoko huo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam, Dotnata alisema kuwa ametumia kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 270 kununua ‘mchuma’ huo kutoka katika tawi la kiwanda cha magari hayo huko Detroit, nchini Marekani. “Kila mtu atasema lake lakini ni kweli nimenunua gari hili kutoka Marekani na nimetumia kiasi cha shilingi milioni 270 mpaka linafika hapa,” alisema Dotnata. Akiendelea zaidi, msanii huyo mwenye heshima kubwa ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo alianika kuwa watu wasimuelewe vibaya kwa kununua gari hilo amefanya hivyo akiwa na lengo la kulikodisha kwenye kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kupunguza makali ya maisha na siyo kutanua nalo kwa matanuzi yasiyo na lazima. “Leo natarajia kukamilisha usajili hivyo mwishoni mwa wiki hii litakuwa barabarani lakini sitalitumuia kwa matanuzi kama ambavyo watu wanaweza kufikiria, nimepanga kulikodisha kwenye sherehe na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili linisaidie kujikwamua, ” alimaliza Dotnata

Dotnata afanya kufuru kwa kvuta "Hummer" la nguvu

MSANII matawi ya juu katika tasnia ya filamu Bongo, Husna Mohamed Posh ‘Dotnata’ amefanya kufuru baada ya kutoa ‘burungutu’ kununua‘mkoko’ wa kifahari aina ya Hummer, Amani Jipya limeinyaka. Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali za kuukomboa mkoko huo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam, Dotnata alisema kuwa ametumia kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 270 kununua ‘mchuma’ huo kutoka katika tawi la kiwanda cha magari hayo huko Detroit, nchini Marekani. “Kila mtu atasema lake lakini ni kweli nimenunua gari hili kutoka Marekani na nimetumia kiasi cha shilingi milioni 270 mpaka linafika hapa,” alisema Dotnata. Akiendelea zaidi, msanii huyo mwenye heshima kubwa ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo alianika kuwa watu wasimuelewe vibaya kwa kununua gari hilo amefanya hivyo akiwa na lengo la kulikodisha kwenye kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kupunguza makali ya maisha na siyo kutanua nalo kwa matanuzi yasiyo na lazima. “Leo natarajia kukamilisha usajili hivyo mwishoni mwa wiki hii litakuwa barabarani lakini sitalitumuia kwa matanuzi kama ambavyo watu wanaweza kufikiria, nimepanga kulikodisha kwenye sherehe na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili linisaidie kujikwamua, ” alimaliza Dotnata

Mar 26, 2011

KILI MUSIC AWARD

1.WIMBO BORA WA ASILI -MIMBA -MPOKI
2.WIMBO WA...... -MAPACHA WATATU
3.WIMBO BORA WA TAARABU-JAHAZI MORDEN TAARAB

Mar 25, 2011

Haya Ndiyo Aliyoyasema Sumaye Kuhusu Matamko/ Shutuma Za UVCCM Zidi Yake

Nimejiunga na TANU tangu mwaka 1966, mimi ni mwana CCM tangu kuanzishwa kwake 1977 na ni mjumbe wa NEC Sina uhusiano mbaya na UVCCM, sina uhusiano mbaya na yeyote ambaye ni mwana CCM. Napenda kuongelea kuhusu 2015, sijaamua kama nitagombea au sitagombea Wananchi ndio wenye uwezo wa kila jambo katika nchi, wananchi ndio wanaopiga kura na ndio wanaoamua nani awe kiongozi na nani asiwe. Makundi matatu yanayoamua nani awe kiongozi ni WANANCHI, CHAMA anachotoka mwanasiasa na DOLA Kwanini nimewaita? Kumeibuka malumbano ndani ya CCM na UVCCM kutokana na matamshi ambayo yanakanganya na mimi ni mmojawapo ambaye nimeshambuliwa sana. Nipo hapa kwa niaba yangu mwenyewe, sijatumwa na yeyote na SIMSEMEI YEYOTE. Nipo hapa kama Frederick Sumaye. Ningeyapeleka kwenye chama hasa NEC lakini kwakuwa na wenzangu wameanza kwa mtindo wa kuitisha vyombo vya habari nami nafuata utaratibu huo Lengo si kushindana wala kupimana nguvu, lengo ni kuweka uwazi kwa wananchi watambue uhalisia Baada ya kuona wananchi wanavyoyapokea maandamano ya CHADEMA na kwa hamasa kubwa nilishauri CCM itoe ushirikiano kwa serikali kwa kuyajibu wanayotoa CHADEMA ili kuweza kuweka hali halisi. Mimi kusema CCM ifanye sikumaanisha MIMI SIMO. Aidha, sijasema serikali isifanye kazi yake. Waziri Wassira amefanya kazi ya serikali vema tu Katika utaratibu wa kawaida, chama kinafanya kazi yake baadae serikali inakuja kumalizia yanayobakia. Kama kazi ya siasa haijafanyika vema na chama basi serikali hubeba lawama zisizostahili. Malumbano ya kisiasa hujibiwa kisiasa, CCM walitakiwa kuwajibu CHADEMA na si kazi ya serikali kufanya kazi ya kisiasa CCM inafahamu kazi ya kisiasa na kimekuwa kikifanya hivyo tangu zamani. Viongozi wetu wamekuwa wakifanya hivyo kwenye kila ngazi. Ni shughuli ya chama na haihitaji maamuzi ya vikao. Akiongea Sumaye linaonekana tatizo kubwa na tena ni utovu wa nidhamu. Nimeshutumiwa na hata kutukanwa na wengine ndani ya chama Nifafanue: Nimeshutumiwa kuwa namshutumu mwenyekiti wa chama. Nilijibu nikadhani mambo yameisha kumbe ndo kwanza yameanza. Nimeshutumiwa na UVCCM Pwani kuwa - Sumaye na Lowassa wana mpango wa kukivuruga chama ili wafikie malengo yao 2015 Kama Lowassa na Sumaye wanautaka urais 2015, kwanini washirikiane? 2015 kutakuwa na marais wawili? Hakuna sehemu hata moja ambapo niliwahi kumtaja rais katika maongezi yangu, madai kuwa namtukana na kumchafua rais ni tuhumu za uwongo kabisa UVCCM wanadai sisi tumeshiba na sasa tumevimbiwa... Tuwaache nao wale kama sisi. Haya ni matusi na kejeli na inasikitisha sana Ina maana UVCCM wana mgombea wao ndo maana wengine tunaonekana kero kwao kwani tunamvurugia mtu wao. Vijana wenye tamaa ya KULA ni hatari kwa taifa Eti vijana wanataka wamweke mtu wao ili wale? Imenishtua sana! Wanadai tunakibomoa chama, wanadai kuwa tunataka rais atoke kaskazini. Kwa madai yao nchi itaendelea kusonga mbele na wanatupa pole tunaodhani rais lazima atoke kaskazini. Ubaguzi huu wa ukanda tena kutoka UVCCM mkoa wa Pwani usipochukuliwa hatua utalipeleka pabaya taifa! UVCCM wana mpango wa kupambana kina Sitta na Sumaye. Wanataka hawa wasipewe nafasi katika chama, wanadai watapigana ndani na nje ya chama kuhakikisha watu hawa hawapewi nafasi. My comment: Sitta yashaanza kumkuta ya UVCCM huko Tabora! Kuna maoni mengine yanaweza kuwa na athari kwa chama hivyo ni juu ya kiongozi husika kuangalia athari ya kutoa maoni husika. Serikali yoyote iliyochaguliwa kidemokrasia LAZIMA itasemwa na kukebehiwa. Kiongozi yeyote na chama chochote kilichochaguliwa kidemokrasia, kitasemwa na watu watakikebehi. Si ajabu Nimeshtushwa SANA na kauli ya UVCCM mkoa wa Pwani kuwa suala la rais ajaye 2015 lipo mikononi mwa rais Kikwete! Hili linanishtua, siamini kama rais Kikwete anamjua rais ajaye 2015 Sasa hivi mtu yeyote akiongea ndani ya CCM ataambiwa anautaka urais, hii inaweza kuwaziba wengi midomo Nawaomba watanzania, yeyote atakayejaribu kutumia njia za udanganyifu kwa RUSHWA, KUTENGANISHA WATU, tumkatae kwa nguvu zote Tunakosa muda wa kujielekeza katika mambo ya msingi tunaanza siasa za kupakana matope - Sumaye Nategemea nimeeleweka, sitarajii kuibua malumbano na sitarajii kurejea kuongea na waandishi juu ya hili. Mimi ni mwana CCM na sipo chama chochote cha siasa zaidi ya hiki. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika MASWALI SWALI: Kwanini hujaandika barua CCM? JIBU: Mimi sijaandikiwa barua, sijibu kwa barua SWALI: Mtu akikutukana ujue KATUMWA NA BABA na ndo maana baba kakaa kimya. Kwanini usijiondoe CCM? JIBU: Ukiona mtoto anamtukana mtu mzima uelewe ametumwa ama anamtukanisha mtu mzima lakini kwa hili la sasa yote yamo. Maana hatujakaa kutuma vijana. Siwezi kutoka CCM sababu ya vijana SWALI: Toka miaka ya 70 kwanini watu wa kaskazini wanasemwa vibaya? Hawafai? Toa ufafanuzi kuhusu kauli yako ya 2005 kuwa ATAKAYEINGIA KWA KUCHAFUA WATU KWA KALAMU ATATUMIA VISASI kuongoza. JIBU: Nilishasema awali, ubaguzi wa kimaoeneo ni hatari sana na si kwa kaskazini tu. Kuhusu suala la U-Kaskazini haina maana maana haijawahi kutoa rais hata akitokea Bagamoyo leo akawa anafaa hakuna neno. Tusitazame watu kwa wanakotokea ama dini zao na rangi zao. Hata bungeni kuna kauli za kibaguzi, tumezikemea bila kujali eneo. Pili, ya 2005: Ni tabia mbaya kuchafuana hata kama ni udiwani, niliyasema na bahati hayajatokea. SWALI LA KUBENEA: Vijana wamejitokeza kutetea mafisadi, unatoa rai gani? Lakini ultimatum wanazotoa si sahihi, labda watoe ushauri. JIBU: Vijana wanatetea mafisadi ama nani, sijui... ila misemo yao inanitisha SWALI LA BBC: Imejitokeza kuzungumza mambo ya chama nje ya chama, kama chama mnalionaje hili haliwaaibishi? JIBU: Future ya CCM ni nzuri ila kuna mambo LAZIMA yafanyike. Yale madhaifu lazima tuyaondoe. kutoka www.mjengwa.blogspot.com
"

BAADA YA BABU WA LOLIONDO SASA ATOKEA BIBI WA MBEYA- DAWA NI BURE

Watu Mbali Mbali wakingojea Dawa
Hapa watu wakijitayarisha kwenda kupata kikombe
Umati wa watu wakienda kupata kikombe eneo hilo la dawa
Bibi akitoa Dawa kwa wahitaji
Tayali foleni zimesha anza eneo hilo
Ni habari ambayo mtandao wa Mbeyayetu.blogspot imetufikia Punde pande za Mabatini ambako ameibuka mtu anatoa dawa Bure na kama mnavyo ona hapo tukio zaidi baadae kidogo...endelea kuwepo
"

"Matajiri" wanavyodhalilisha watawala waroho

Zuma amwagiwa pombe Kituko kilitokea hivi karibuni nchini Afrika Kusini ambapo rais Jacob Zuma alimwagiwa pombe na mwananchi mmoja. Zuma ambaye anasifika kwa kupenda vimwana na matanuzi alipatwa na mkasa huu mjini Durban nchini mwake. Japo yaweza kuchukuliwa kama bahati mbaya, huu ni ushahidi kuwa watawala wetu wanajifanyia mambo hovyo hovyo hasa kutokana na kujiingiza kwenye shughuli zinazoweza kuhatarisha usalama na hata madaraka yao. Inakuwaje kiongozi wa nchi ajikute kwenye mazingira rahisi kumwagiwa pombe? Kuna siku watanaswa vibao kutokana na kuwa na shughuli haramu za siri. Kwa habari zaidi, BONYEZA HAPA
"

MZUNGU WOOOOH NICE SCENE!!!!!!

Wazungu alipofika pale Selou ilikuwa burudani kweli kweli kila mnyama anayepita ni kamera kupicha piga!!!!reverse reverse

MZUNGU ANAPOMZUGA MTOTO WA KIBONGO

Mzungu huyu  akimpa chupa ya maji iliyoisha mtoto katika eneo la Chita  haya ndiyo mambo yanayotusibu watz hapa pale tunapoonyesha nia ya kupiga mizinga kwa wageni si unajua siyo kila mzungu ni Padre!!!!!

MAAJABU JAMAA ANAMILIKI KIBERENGE NYUMBANI KWAKE

Hii niliikuta pale Ifakara jamaa amehifadhi Kiberenge nyumbani kwake kama vile tunavyopack bajaj vile upenuni mwako pale home!!!!

MLIMBA HII

Sasa tujionee maajabu kwa Loliondo kwa Babu Ambilikile Mwasapile

NIMEIPENDA HII MAAJABU YA LOLIONDO"
"

JAMANI TUNA UTAJIRI WA VIVUTIO , HEBU SAFIRI KWA TRENI UONE

 Hii kona ni kivutio tosha, ipo mbele ya vituo vidogo vidogo kabla ya Mgeta.
 Burudaaaniiiii
 Yes how dou see? beutifuleee!
ebwana eee ndiyo uumbaji wa mwenyezi mungu na baadaye mikono ya  mchina

MASHOSHOROZA(TRENI) ZA TAZARA ZIFANYIWE MABORESHO

 Hizi taa za Treni zimeshachakachuliwa vioo vyake kwahiyo unalala kimachale hasa ukiwa kwenye deka!
 Mbu kibao hakuna net!!! jamaa wa upande wa pili wa deka langu nilimvizia akiwa amelala nikabonyeza kamera kutaka ushahidi wa huduma za TAZARA!  blanketi na shuka pia changamoto zingine hazifuliwii!

 Hapa sikulenga kuwaonyesha hawa jamaa wakiwa wamekaa kwenye second class ila nilitaka nionyeshe hiyo soketi pembeni haifanyi kazi waya zake zilishachakachuliwa nikashindwa kupost matukio yote kwa siku hiyo kwakuwa hakukuwa na chaji kwa laptop
 Hapa ndiyo TOILET aka mariwatoni, kwa treni la Express la zambia wanajitahidi kufanya usafi na kuweka maji wakati wote, lakini nimeambiwa express ya Bongo ni bongo kweli kweli hakuna cha maji wala nini, unaenda huku na chupa yako ya maji!!!!!

BIASHARA KANDO KANDO YA RELI INAWATOA WANANCHI WETU

 Hapa ni kituo cha Uyole ambapo kuna shehena kubwa ya Viazi vikiuzwa kwa abiria wa Treni la EXPRESS  njia hii ya uchukuzi inasaidia sana kuuumua uchumi wa wakazi walio pembezoni hasa kando kando mwa reli ya Tazara kwani kwa hali ya kawaida wasingweza kuuza kwenye barabara kuu ambako ni mbali na maeneo ya vitongoji na vijiji vyao
Nauza nauza!!!!!!!! Hiyo ilikuwa Uyole bado

MJAMAICA AAMUA KUSHUKA KWENYE TRENI NA KUONYESHA MAZINGAOMBWE KWA ABIRIA WENZAKE

 Mjamaica aliyefahamika kwa jina la Fernando akizungumza na wandishi wa dtweve.blogspot juu wakati akijiandaa kutoa vimbwanga kwenye behewa la daraja la pili TAZARA jana katika moja ya stesheni ambako alishuka na kuanza kufanya mazingaombwe.

 Kisa cha kuonyesha mazingaombwe ni baada ya kuhama kutoka daraja la tatu na kuja kujificha daraja la pili chumba ambacho mwandishi wa mtandao huu alikuwemo, sasa akaanza kuomba kaptula kutoka kwenye begi la Mwandishi wa mtandao huu, jambo ambalo kidogo lilikuwa gumu kwani siyo kawaida kuvaliana nguo na mtu usiye mfahamu labda  mkeo!!, lakini jamaa aling'ang'ania huku akizungumza kingereza cha kuunga unga akiitaja kama Puantalelo, hii ilitokana na yeye kutaka afue suruali yake haraka halafu aikaushe, sasa hapo ndipo watu wakataka waone anaikaushaje haraka naye akawaambia mbona rahisi tu, ngoja niwaonyeshe vimbwanga vingine kabla sijakausha! ilibidi nizame na nitoe kaptula yangu hiyo na ndipo akawa huru na kutoka nje ya behewa na kuanza kufanya show hadharani kama anavyoonekana. Alichonifurahisha zaidi yeye anaona tu Tanzania sawa na jamaica ni nchi ya kijamaa kwa hiyo kila kitu yeye alikuwa anaomba, naomba maji ya kunywa, naomba sijui nini!!!! bahati mbaya treni la express la jana lilikuwa la wazambia hawana huo utaratibu wa kuombana ilikuwa  balaa kwake akaanza kutukana Boushiiiiiiiiiit mother.....f.....c...k nakadharika ikawa kituko kwenye treni hilo, manake walimg'ang'ania aende third class hadi wakamfikisha
Wanufaika wa show yake wakiwa wanachungulia dirishani wakati akifanya mambo yake hapo ilikuwa stesheni ya Mbeya

BARAZA LA MADIWANI MBOZI WAJIPANGA KUIMARISHA ELIMU WILAYANI MBOZI

 Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya MBOZI Bw. Lington Ngaikwela akitoa maelezo kwenye baraza la madiwani lililoketi jana wilayani Mbozi

Baadhi ya waheshimiwa madiwani wakifuatilia mjadala na makarabrasha kwenye kikao hicho

 Diwani wa kata ya Ipunga Mh Burton Sinyenga akichangia mjadala kwenye kalabrasha lake ambapo alizungumzia kuimarisha kwa makazi ya walimu kama njia ya kuvutia walimu vijijini
Diwani wa viti maalumu kata ya Luanda Mh Eva  Mlonganile akichangia kwenye baraza hilo ambapo alijielekeza zaidi katika kuitaka idara ya maendeleo ya jamii isaidia kuviimarisha vikundi vya VICOBA ambavyo vimeanzishwa na wanawake kwenye kata hiyo.,

Mar 24, 2011

SHIMO HILI LINATOKEA ZIWA RUKWA

Shimo lenye urefu wa zaidi ya maili 200 lipo katika kijiji cha songwe wilayani mbozi na linatokeza kwenye ziwa rukwa umbali wa zaidi ya maili 200 kutoka kijiji cha Songwe, ni sehemu ya utalii pia ambapo baadhi ya wageni wamekuwa wakitumbukia humo na kutembea kwa umbali fulani kuangalia maajabu yaliyomo na hasa idadi kubwa ya popo kwenye shimo hilo