Adverts

Apr 30, 2011

WATOFAUTIANA KWA KURA MBILI

Hatimaye matokeo ya uchaguzi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya umekamilika baada ya kumchagua Bw.Christopher Nyenyembe kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu hiyo.

Awali nafasi hiyo ilikuwa ikichukuliwa na Bw. Nico Mwaibale aliyejiuzulu uongozi baada ya kuhamishiwa kikazi katika mkoa wa Tabora..

Katika uchaguzi huo Nyenyembe amepata kura 15 na Luhanga kupata kura 13, huku mgombea mwingine Mpanji akipata kura 1.

Katika hali ambayo ni ngumu, hatimaye uongozi wa Mwenyekiti mpya amerejesha mamlaka kutoka kwa wananchama waamue kutokana na kukosa imani na katibu mkuu kufanya naye kazi.

katika hali hiyo ukumbi ulipoza, baada ya mwenyekiti mpya kutamka hilo kutokana na kutofautiana katika maelezo kati yake katibu na mwenyekiti wa kamati ya Nidhamu hatua ambayo alilazimika kutamka katika maneno yake ya kushukuru na hivyo kurejesha kwa wanachama kumkubali katibu ama kumkataa.