Adverts

May 28, 2011

SEMINA YA NDOA KWA WANANDOA NA WANAOTARAJIA

MAMA SALMA AWATAKA VIONGOZI WA UWT KUSHIRIKIANA NA WASOMI

Na Anna Nkinda – Maelezo, Dodoma
Wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nchini wametakiwa kushirikiana na vijana wasomi katika kufanya kazi zao ili kuboresha utendaji wao wa kazi kwani nguvu kazi zaidi itatokana na vijana hao na siyo vinginevyo.
Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanachama wa umoja huo katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa hivi sasa vijana wasomi wanafanya kazi zao na kushindana kwa hoja zenye nguvu kutokana na elimu waliyo nayo hivyo basi kama wataamua kuwatumia umoja huo utanufaika na kuwa na mabadiliko ya kiutendaji.
“Shirikianeni na wasomi wa vyuo vikuu, wafundisheni kazi, wapeni nafasi na siyo kuwapinga kwa kuwaona kuwa wao wanajua zaidi kuliko ninyi kwani hivi sasa Dunia imebadilika inaenda sambamba na teknolojia hivyo basi ni rahisi kwa vijana kufahamu mambo mengi tofauti na wazee na mkumbuke kuwa ili muweze kushindana ni lazima mfanye mageuzi,” alisema mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete aliwasisitiza kina mama hao kuwa na tabia ya kutunza siri na kuhifadhi yale yote ambayo yanajadiliwa ndani ya vikao vya Chama na siyo kuyaongea nje kwa watu wasiohusika.
Mwenyekiti huyo wa WAMA pia aliwataka wanawake hao kuongeza juhudi ya kuwahamasisha akinamama wengi zaidi kujitokeza kuwania uongozi katika nafasi za majimbo na kata , kwani ni dhahiri kwamba wanawake wengi wamejitokeza kwenye nafasi za viti maalum kuliko za kata na majimbo.
Alimalizia kwa kuwasisitiza kina mama hao kuongeza ushirikiano kupitia vikundi vya maendeleo ya kiuchumi kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia wanawake wengi zaidi kufaidika na fursa zilizopo chini ya mipango ya Serikali ya kumkomboa mwanamke.
Akisoma taarifa ya UWT ya mkoa wa Dodoma Katibu wa umoja huo Amina Kanyogoto alisema kuwa wamekuwa wakihamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa kufanya semina kwa kila kata, kutoa semina kwenye mabaraza ya wilaya na mkoa, kutoa ushauri nasaha kupitia kwa viongozi wao kujitokeza kwenda kupima kwa hiari na kutoa semia kwa waelimisha rika.
Aliyataja mafanikio waliyoyapa hadi sasa ni wanawake wengi kuwa na mwamko wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi zote baada ya kuhamasishwa na pia kina mama wengi wamekuwa na ari ya kufanya biashara ndogondogo za kujitafutia kipato cha familia zao.
Kanyogoto alisema, “matatizo yanayotukabili ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za uzalishaji mali kwa wajasiriamali wanawake, mikopo inayotolewa haitoshelezi mahitaji na bidhaa zinazotengenezwa na kina mama bado ni tatizo kwa ajili ya ukosefu wa masoko na uuzaji wa bidhaa hizo.”
Mama Kikwete yupo mjini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria matembezi ya uchangishaji wa chakula kwa shule za msingi yatakayofanika kesho tarehe 29/5/2011 yaliyoandaliwa na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya hapa nchini.
Mwisho.

KOCHA WA MAPINDUZI JUMA MWAMBUSI AVUNJA REKODI KWA KUCHUA UBINGWA MARA MBILI MIKONONI MWA MWANZAKijana Juma Mpola akionyesha makeke yake, alikuwa mchezaji wa majimaji katika msimu unaomalizika na ni kijana wa Simike jijini Mbeya ambaye katika mashindano Kili Taifa Cup amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa jumla wa mashindano hayo
 Na Danny Tweve Mbeya.

Kocha wa Mapinduzi starz Juma Mwambusi, leo amevunja rekodi baada ya kuiwezesha timu yake kuifunga Timu ya Mkoa wa Mwanza( Mwanza Herous) kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali wa Kili Taifa Cup uliochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Hii ni mara ya pili kwa Mwambusi kuwafunga  Mwanza katika fainali za mashindano haya baada ya kufanya hivyo kwa mara kwanza mwaka 2005.

Timu hizo zilipokutana katika fainali iliyochezwa katika uwanja wa jamhuri mjini Morogoro, Mbeya iliweza kuwafunga Mwanza kwa mikwaju ya penarti 4-3.

Mwaka jana Mbeya iliondolewa mapema katika mashindano hayo pasipo kumtumia kocha huyo dalili za wazi zinazoonyesha kuwa mzizi wa Mapinduzi Starz anao yeye.

Mbeya kwa mara ya mwisho iliingia fainali za mashindano hayo mwaka 1966 wakati huo mashindano haya yakiitwa Taifa CUP  baada ya kufungwa bao 1-0 na Timu ya Kilimanjaro katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa Kumbumbuku ya Karume zamani ukiitwa Ilala stadium.

Ushindi wa Mbeya ulionyesha dhahiri katika mchezo wa leo ambapo kulikuwa na mashambuzi ya mara kwa mara kwenye lango la timu ya Mwanza, hata hivyo uimara wa ngome ya Mwanza uweliza kupunguza madhara kwa kiwango kikubwa kwa kuwazuia mapinduzi wasipate bao la ushindi mapema.
Hadi  timu hizo zinakwenda mapumziko, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake.

Hazta hivyo hali ya mchezo ilibadilika baada ya timu ya mapinduzi starz ya Mbeya kukianza kipindi cha pili kwa nguvu na hivyo kuwabana wapinzani wao katika nusu yao ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Alikuwa ni mshambuliaji asiyekata tamaa na mwenye uchu wa magoli Gaudensi Mwaikimba ambaye ametwaa tuzo ya mfungaji bora, kuwainua mashabiki wachache wa mbeya kwenye viti katika dakika ya 88 baada ya kuunganisha kwa kichwa  wavuni  mpira wa krosi iliyopigwa na Juma Mpola  kutoka wingi ya Kulia na kumuuacha kipa wa Mwanza akichupa pasipo mafanikio.

Ikumbukwe kuwa Juma Mpola ametwaa shilingi Milion 2.5  baada ya kuchaguliwa kama mchezaji bora wa jumla katika mashindano hayo huku Mwaikimba naye akitwaa nafasi ya mfungaji bora wa mashindano hayo  kwa kufunga mabao 8 na kumwacha mpinzani wake Jerson Tegete wa Mwanza Herous aliyeambulia kufunga magoli sita tu.

Kutokana na hilo Mwaikimba amejizolea kitita cha shilingi Milion 2.5 na kuisadia pia timu yake ya mapinduzi kutwaa zawadi ya shilingi  Milion 40 kama mabingwa wapya wa Kili Taifa cup kwa mwaka 2011.

Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya soka mkoani Mbeya Ggeorge Chanda mashindano ya mwaka huu yalikuwa na ushindani wa hali ya juu ambapo kila timu ilikuwa inajitahidi kadiri ya uwezo wake kuweza kuchukua kombe hilo, hata hivyo bahati imewaangukia Mbeya ambao wameonyesha ni timu bora kwa kutwa taji hilo.
Kocha Juma Mwambusi ambaye ameonekana kuwa na nyota nzuri na timu ya Mapinduzi Starz pia aliiwezesha klabu ya  Tukuyu staz kucheza katika nane bora katika ligi kuu ya mwaka 2001 na pia kutwaa zawadi ya timu yenye nidhamu bora.

FUATILIA MISS TABORA ALIVYOTANGAZWA JANA

SHUKRANI MDAU NICO MWAIBALE TBC TABORA

PICHA ZA MATUKIO YA AJALI YA SUMRY ZAANZA KUINGIA MTANDAO WA INDABA AFRICA

BASI LA SUMRY KAMA LINAVYOONEKANA
Hili ndilo basi la Sumry  likifunikwa na wafanyakazi wa Sumry fasta fasta baada ya kuona timu ya wandishi wa habari ikisogea eneo la Tukio
ASKARI WA usalama barabarani akikagua sehemu ya mabaki ya basi hilo baada ya kunyofoka kwa front excel

Manusura wa ajali hiyo Bi Mary Karoli akisimulia namna gari hilo livyopata masahibu hayo, anaeleza kuwa dereva alikuwa akitafuna tafuna majani kila alipofika mahala kushusha abiria dalili zinazoashiria kulikuwa na chakula kinachokatazwa kwenye safari za madereva (mirungi).
Shuhuda wa ajali hiyo akisimulia jinsi walivyotoa msaada kwa majeruhi  usiku jana


Na Danny Tweve -Mbeya

Hatimaye takwimu sahihi za vifo vya abiria katika ajali ya basi la Sumry iliyotokea jana usiku mpakani wa Iringa na Mbeya imefikia watu 13 na siyo 15 kama ilivyoripotiwa hapo awali na mtandao huu.

Akizungumza na wanahabari mchana huu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema mpaka sasa maiti 13 wamepokelewa katika hospitali ya rufaa  wazazi ya Meta ambako kwa sasa wamehifadhiwa kutokana na kuwepo kwa vifaa vya kutunzia maiti.

Mpaka sasa maiti zilizotambuliwa ni pamoja na Dereva wa Basi hilo Makame Juma, Abiria Frolence Kitaule ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Ubaruku-Mbarali, Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe Thomas Mchalo, ingawa pia taarifa zaidi zinaonyesha kondakta wa basi hilo pia amefariki kutokana na sare za basi la sumry alizovaa ambazo maiti yake imekutwa nazo. 

MSAADA KWA WAZAZI, IKITOKEA MAMA AMEZIWA AKIWA KWENYE GARI WAKATI WA KUJIFUNGUA MTOTO.

http://www.ehow.co.uk/video_4441670_deliver-baby-taxi-cab.html

MASHABIKI WATUPIA BARUTI UWANJANI NA KUHARIBU MCHEZO

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=3ln06429pfw#t=46s

AJALI YA SUMRY TAARIFA RASMI WALIOFARIKI SASA NI 15

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya ADVOCATE NYOMBI amesema idadi ya waliokufa katika ajali ya Sumry iliyotokea jana majira ya saa 4.45 Usiku ni watu 15. Akizungumzia ajali hiyo kamanda Nyombi amesema gari hilo limepinduka baada ya kupasuka kwa gurudumu la Mbele na kwamba sehemu kubwa ya majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya misheni ya Ilembula na Chimala.
Amesema gari hilo likitokea Arusha lilikuwa katika mwendo kasi na baada ya kupasuka gurudumu la mbele dereva alishindwa kulimudu hatua ambayo lilikwenda pembeni na kupinduka hatimaye kukatika eneo la juu kuanzia kwenye vioo na kusababisha vifo15 na majeruhi 20.
Dereva wa gari hilo ni miongoni mwa waliofariki papo hapo.

Hili ni tukio la pili katika kipndi cha miezi minne ambapo January 13 basi jingine la Sumry lililokuwa likisafiri kati ya Dar na Mbeya katika eneo la Mikumi  liligongana na roli aina ya Fuso katika eneo la Masimba -Mikumi na  na kuua watu 8 na wengine 20 kujeruhiwa.
Waliokufa katika ajali ya jana bado majina yao hayajawekwa hewani na taarifa zaidi zitawajia baada ya muda mfupi kwani ripota wetu yupo eneo la Tukio kwa sasa.
endelea kuwa nasi www.dtwevetz.blogspot.com

DU POMBE NI NOMAA!!! BABA ANAPOAMUA KUWA GAIDI!

Hivi ndiyo maisha zya vijijini! kupigana ni sehemu ya chachandu za ndoa! kuwanining'iniza watoto hivi kama kuku wa mnadani ni sehemu nyingine ya ukatiri unaoshuhudiwa siku hadi siku -Du pombe nomaaa!

BREACKING NEWS: BASI LA SUMRY KUTOKA ARUSHA-MBEYA LAPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO VINGI!

Zaidi ya watu 12 wanahofiwa kupoteza maisha baada ya basi la Sumry High Class linalotoka Arusha kwenda Mbeya kupinduka eneo la Igawa.
Taarifa zilizoufikia mtandao wa www.dtwevetz.blogspot.com zinaeleza kuwa basi hilo limepinduka majira ya saa nne usiku likitokea Arusha ambapo limekatika kuanzia kwenye  vioo na cabin yote ya juu imetoweka.
Mmoja wa walioshuhudia ajali hiyo  Frank Tweve ambaye alikuwa safari kutoka Dar Es Salaam akiendesha gari jingine amesema, akipita hapo majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo  ameshuhudia Maiti 7 za wanaume, 2 za watoto na 4 za wanawake na inaelezwa kuwa maiti zingingine tayari zilikuwa zimeondolewa eneo la ajali na maiti nyingine zikiwa zimebanwa na vyuma kwenye basi hilo..
Gari hilo kulingana na maelezo hayo liliburuzika kwa umbali mrefu. na Taarifa zaidi mtaendelewa kuletewa na blog hii, endelea kuwa na indaba africa.
Tayari  mtandao umetuma kamera ya matukio katika eneo la ajali na mtaanza kuzipata picha asubuhi hii kadiri tunavyounganishwa na mpiga picha aliyeko eneo la ajali.

May 27, 2011

JAMANI MWENYE MAWASILIANO NA WADOGO ZAKE MAREHEMU FREDY KAOMBWE ATUWEZESHE

UJUMBE WA JANA
Hello Indaba Africa,
I am  Mr...........kindly requesting you more information about Mr.Fredy
Kaombwe. I have studied with him in Korea and now lots of our friends
want to know what happened to him.
Please, send me any information, including his address and names of
family members (if possible in English).
Thank you very much in advance.
Best,
.............................
Uzbekistan

UJUMBE WA LEO
Dear INDABA
Thank you for the quick reply and the information. Please send us any
contact information, Fredy had a lot friends in different countries of
the world. We would like to say some supportive words to the family
members.
Thank you very much once again.
Best,
............................

Nimeamua kuweka mezani mails zinazohitaji mawasiliano na familia ya Kaombwe, sasa kwa nia njema kabisa nawaombeni wana mipango mnaofahamu contact za wadogo zake basi nitumieni ama za watu wa karibu na marehemu manake kuna mails zingine wananitaka nieleze namna gani watume rambi rambi zao nami sina contact za hao please hebu facilitate hilo
niandikie kwenye indabaafrica@gmail.com

BAADA YA KUKAA GIZANI KWA SAA 3 NURU YAREJEA MBEYA

Kukatika kwa umeme kulikotokea leo hii kuanzia saa 11.00  jioni kumetoweka majira ya saa 3.10 Usiku huu baada ya TANESCO kuturejeshea nuru tena.

Kimsingi shughuli nyingi zilisimama tangu mgao huo utokee mjini Mbeya ambapo taarifa pia kutoka wlayani zinaeleza kuwa Mkoa wote wa Mbeya kwa kipindi hicho haukuwa na umeme.
Bila shaka ni utelelezaji wa lile suala la mgao!!!!!!!!!!!!!!

KIPANYA NAYE BWANA!!!!

MKE WA WAZIRI MKUU WA INDIA ATOA MSAADA WA MILION 15 KWA WAMA

Na Anna Nkinda – Maelezo
27/5/2011 Dar es Salaam Mke wa waziri Mkuu wa India Mama Gursharan Kaur ametoa msaada wa shilingi milioni 15 kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleoo (WAMA) fedha ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali za kuwasaidia watanzania zinazofanywa na taasisi hiyo.
Msaada huo umetolewa leo katika ofisi za WAMA zilizopo jijini Dar es Salaam wakati mama Kaur alipoitembelea taasisi hiyo inayoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kufahamu shughuli zinazofanywa na WAMA.
Akikabidhi msaada huo Mama Kaur alisema kuwa ameguswa na kazi zinazofanywa na WAMA za kuisaidia jamii ya kitanzania, hivyo msaada huo utasaidia kutekeleza majukumu mbalimbali wanayoyafanya.
Kwa upande wake Mama Kikwete alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua matatizo yanayoikabili jamii ya kitanzania.
Alisema kuwa taasisi ya WAMA imekuwa ikipokea misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa maendeleo wa ndani na wa nje ya nchi hivyo aliwaomba wananchi wenye moyo wa kusaidia wasisite kufanya hivyo bila ya kuangalia kama msaada watakaoutoa ni mdogo au mkubwa.
Mama Kikwete alisema kuwa Taasisi ya WAMA imekuwa ikifanya kazi mbalimbali za kuhakikisha kuwa inawasaidia wanawake kuinua maisha yao, kuisaidia jamii ya watanzania kuwa na afya bora, kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa vijana na kada tofauti, kushughulikia uzazi salama na kuwawezesha watoto wa kike ambao ni yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu.
Mama Kaur ameambatana na mumewe waziri Mkuu wa India Dr. Manmohan Singh aliyeko nchini katika ziara ya kikazi ya siku tatu.
Mwisho.

MDAU KUTOKA BONDENI AENDELEZA FANI KIWANDANI

 Mtaalamu wa Kitanzania anayefanya kazi  nchini Afrika Kusini Bwana Ismail Mwilenga ni miongoni mwa  wataalamu wa kitanzania wanaokubalika kutokana na uwezo wao katika kutekeleza majukumu ya kila siku na kutoa tija kwenye viwanda wanakofanya kazi, Nadhani siku akirejea Bongo lazima atoe lecture how to work efficiently for effective .............malizia msomaji, kingereza kimegoma!!!!!

UJUMBE WA LEO KWAAJILI YA WEEKEND

Happy weekend everyone. MY USUAL MESSAGE: IF YOU ARE GOING TO MAKE LOVE...MAKE SURE YOU CUM AND PLEASE MAKE SURE IT'S SAFE ...AND MAKE SURE IT'S WHAT YOU WANT.
Love you all

KWA WALIOSOMA SHULE HII MTAIKUMBUKA SANA HASA MZEE NDIMBO!!

Turejeshe fadhila kwa shule hii kwa wale waliosoma hapa manake naona kama mmeisahau!!

VING'AMUZI VYA STAR TIMES LEO NDIYO ISSUE YA HAPA MJINI MBEYA

Abiria mmoja akisoma bango la matangazo la Star Times baada ya gari la matangazo la kampuni hiyo kuvimwaga barabarani ovyo kuwapa fulsa wananchi kusoma na hatimaye kufanya maamuzi ya kwenda kuvinunua katika ofisi zao walizofungua mjini Mbeya.

JIWE HILI LINA UMUHIMU MNO KWA MAISHA YA WANANCHI WA MBOZI HADI AFRIKA KUSINI

 Huu mwamba wa jiwe ndiyo kimfuniko cha mwamba wa maji unaopeleka mkondo wa maji yake kwenye mto Zambezi na kuunganishwa na Limpopo. Watu wamekuwa wakipita eneo hilo bila kufahamu umuhimu wake na wakati mwingine wanalaumu kwanini TANROADS hawajaling'oa bila kujua umuhimu wake.

PSI wao wakaona watumie eneo hili kama sehemu ya kuweka Tangazo lao la Kondomu! Biashara ni ujanja na kuwahi kujitangaza.

ENEO JIPYA LA KUOSHA MAGARI - NI KITUO KIKUU CHA MABASI MBEYA

May 26, 2011

,MAADHIMISHO YA SIKU YA KEMIA , TANZANIA YAFANAKakue Mafole kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali (kulia) akiwaelezea waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) na waziri wa ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya Huvisa (wapili kushoto) jinsi ofisi hiyo inavyofanya kazi za kupima vitu mbalimbali. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Picture no.2 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimshauri Mkuu wa kitengo cha Kemia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Phillip Joseph jinsi gani wanaweza kufanya kazi ya kuchuja maji hadi kufikia hatua ya kuwa maji safi na salama kwa ufasaha zaidi na hivyo kuingia katika soko la ushindani wa biashara. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picture no.3 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiangalia aina mbalimbali ya vitabu vya kufundishia somo la kemia wakati wa ufunguzi wa mwaka wa kimataifa wa kemia. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe hizo zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picture no. 4 Brighton Jacob (wan ne kulia) mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka shule ya Sekondari Kiluvya iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi ya kutambua aina mbalimbali za udongo. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picture no. 5 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimsikiliza Sara Rubagumya (wa kwanza kulia) mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Tegeta iliyopo jijini Dar es Salaam kuhusu jinsi ya kuzalisha umeme kwa njia isiyo na gharama. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picture no. 6 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (watatu kutoka kushoto) akimsikiliza Salim Buyogera mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya Sekondari Mbeta iliyopo jijini Mbeya alivyokuwa anaelezea jinsi vipande vya mabati vinavyoweza kuhifadhiwa na kutumika kufanya mambo mengine wakati wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Kushoto kwa waziri ni Naibu waziri wa wizara hiyo Philipo Mulugo na kulia kwa waziri ni Chande Othman mwenyekiti wa chama cha wakemia nchini.

Picha namba7 Elizabeth Mlay (kulia kwa waziri ) mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi ya kutengeneza dawa ya kusafishia na kuondoa harufu chooni. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Picha na Anna Nkinda - Maelezo


MAREHEMU FREDY KAOMBWE AAGWA, SALAM KUTOKA NJE YA NCHI NA NDANI ZAMIMINIKA

Ndugu zangu kwanza tupeane pole nyingi maana jambo hili limetushtua sana na hasa tunaomfahamu Fredi tangu tukuwa IRDP.

Nilibahatika kuhudhuria ibada ya kumuaga Fred iliyoongozwa na wachungaji 3 wa kanisa la anglikana Dodoma. Watumishi hawa katika sala zao, na hususan mahubiri wamejitahidi kutukumbusha kumtegemea Mungu kwa kila jambo na kuacha tamaa za kidunia.

Waombolezaji walikuwa ni wengi sana wakiongozwa na wakuu wa Wilaya za Bahi, Chamwino na Manispaa. Aidha mh.Mkuu wa mkoa wa Dodoma alihudhuria.

Mambo mengi sana yanasemwa kwamba inawezekana kajiua, au kauwawa. Hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza akasema ndiye alimpeleka hospitali kutoka eneo la tukio au ndiye aliyemjulisha marehemu kwamba mke wake alikuwa na hawara. Watu wa usalama watatusaidia ikifikia mahali pa kuchunguza kifo cha marehemu. Wengine wanasema hata simu yake haikupatikana.

Watu walihuzunika zaidi baada ya kusikia marehemu miezi 3 iliyopita amehitimu shahada ya pili katika fani ya maendeleo ya uchumi na biashara ya kimataifa huko korea ya kusini.

Fred amefariki akiwa na umri wa miaka 28 na ameacha mke na mtoto mmoja . Atazikwa Sikonge Tabora kesho. Msafara wa kuelekea Sikonge una watu wasiopungua 50-60 na tumeusindikiza hadi Nala (njia ya kuelekea singida saa 9.15 mchana.

Wale waliopo Tabora, hususan Wilaya ya Sikonge mtuwakilishe pia.

Tumwombe Mwenyenzi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.

Regards,

Nringi S.N.Urassa
BAHI-DODOMA.

TUNAOMBA WADAU  ANGALAU MUENDELEE KUTUHABARISHA  TUKIAMBATANISHA NA PICHA ZA MATUKIO HUSIKA ILI TUWE PAMOJA KATIKA SAFARI YA MWISHO YA NDUGU YETU FREDY KAOMBWE  HADI PUMZIKO LAKE LA MILELE! AMEN BY ANCHOR

UWATA SECONDARY SCHOOL YAJIIMARISHA ZAIDI

Hii ni miongoni mwa mijengo kama siyo majenfo ya taasisi ya Uamsho wa Wakiristo Tanzania UWATA ambao wamejielekeza zaidi katika kutoa elimu bora kwa watoto wa kitanzania. Majengo haya yapo eneo la ISYESYE katika jiji la Mbeya

NDIZI ZA VWAWA TAAAAAAAAAAAAAAMU


Hapa ni mjengoni nilikopanga, ukitoka nje tu unakutana na Migomba yenye afya iliyoshiba na hatmaye inaleta
 ndizi kama hivi!!!!!

VIWANGO VYA USHURU WA MAZAO MBEYA VIJIJINI NI KAMA IFUATAVYO


Hivi ndiyo viwango vya kodi na ushuru vilivyothibitishwa na TBS!! EEE mkulima unalima kwa shida , unafuga kwa shida, hakuna fidia Nguruwe wakikumbwa na ugonjwa wa Swain Fluu lakini ukifiksha sokoni hali unakutana nayo ndiyo hii

ENZI ZA KUANIKA UNGA KWENYE MKEKA, SASA TUNAANIKA KWENYE UNGO

SOKONI VWAWA-MBOZI LEO HII MCHANA KUPO HIVI


Baada ya Biashara ya machungwa kuchukua nafasi kwamuda mrefu leo mchana nikiwa katika soko la Vwawa nimekutana na aina hii ya matunda! Mie nikajua maboga ya Iringa kumbe yanaitwa Matikiti maji ati!!!!

COMPLEX MPYA YA MADUKA KABWE MBIONI KUFUNGULIWA

Kama inavyoonekana ni sehemu ya maduka yaliyojengwa kuelekea barabara ya Ruanda -KKKT ukitokea  kituo cha mabasi ama makutano ya Kabwe mjini Mbeya

COMPLEX MPYA YA MADUKA KABWE MBIONI KUFUNGULIWA

Kama inavyoonekana ni sehemu ya maduka yaliyojengwa kuelekea barabara ya Ruanda -KKKT ukitokea  kituo cha mabasi ama makutano ya Kabwe mjini Mbeya

BARABARA YA KABWE -UWANJA WA NDEGE CHOOKA MBAYA

KATIKA MAISHA YA MTANZANIA NANI HAJAPITIA KULA MOJAWAPO YA MBOGA HIZI?Kama kuna mtu hajawahi kula mojawapo ya mboga hizi bofya kwenye comment, ili niweze kutoa takwimu hadhrani za watembeleaji wa blog hii ambao hawajawahi kukutana na mboga hizi katika maisha ya uswazi,Tanzania.

TOYOTA WATOA DUDE JINGINE- NI FT V6


Baada ya mikwara ya Toyota Kluger, sasa kitu kinaitwa Toyota FT kipya hicho hapo, tayari kimo mitaani, tena mbeya!! ebwana wee angalia milango inavyofunguka! mlango mmojaunafunguka kwenda mbele mwingine kwenda nyuma (kama geti vile).

KAMPUNI YA VING'AMUZI YA STARTIMES YAINGIA MBEYA KWA SPEED YA UMEME

 Hili ni jengo la Star Times linalotumika kutoa huduma za kuunganisha wateja na ving'amuzi  vyake kwaajili ya kuangalia televisheni kupitia teknolojia ya digitali- jengo hili limefunguliwa rasmi wiki tatu zilizopita katika eneo la kituo cha mabasi cha Mbeya-Terminal.
hapa ni eneo la kutolea somo somo kwa wateja kabla hajafanya maamuzi na baada ya kufanya maamuzi ya kununua king'amuzi cha star tiems

May 25, 2011

VODA M- PESA MBEYA SASA YAKAA MKAO WA KIBENKI


Kaunta Mbalimbali za  M-pesa  kama inavyoonekana asubuhii katika jengo la shirika la Posta la Mbeya ambapo mawakala tofauti tofauti wa M-Pesa wameunganishwa pamoja ambapo kila mmoja ana kaunta yake, sasa burudani ni pale mteja unapowasili- kila lugha ya kubembelezwa unaipata-- karibu baba karibu hapa , welcome , this is a favolable counter na kila maneno matamu! Ubunifu muhimu kwenye biashara

OFA YA MATANGAZO MWEZI MMOJA BURE

BLOG HII INATANGAZA OFA MAALUMU YA MATANGAZO BURE KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA KUANZIA  LEO 25/05 HADI 25/06/2011.
Tuma tangazo lako kupitia indabaafrica@gmail.com ama nitwangie kwa 0764947555

META LEO ASUBUHI KUPO HIVI

Hapa ni eneo la Meta linalotenganisha makazi ya Forest Mpya na Meta ambapo kuna minara mingi ya kampuni za mawasiliano kama linavyoonekana asubuhi hii kuna dalili kuwa baridi Mbeya mwaka huu ni balaa !

USHINDANI WAMFANYA DHANDO COMPLEX KUBADILI SURA

Ukumbi maarufu wa Dhando Complex upo kwenye hatua za kuezuliwa na kuezekwa upya kufuatia ushindani mkubwa unaojitokeza katika uwekezaji kwenye kumbi za starehe na shughuli mbalimbali jijini Mbeya. Hii nimeinasa asubuhi hii

Huu ni Ukumbi wa Rehema  City Conference Centre uliojengwa ukitazamana na Dhando Complex ambapo sasa shughuli nyingi zimekuwa zikimiminika kufanyika kwwenye ukumbi huu na kuusahau ukumbi wa makuti wa Dhando, e bwanaee biashara ni maboresho!
Sura ya Ukumbi wa Rehema kwa mbali, Ukumbi ambao upo kando kando mwa barabara ya Mwanjelwa-Meta