Adverts

Aug 31, 2011

SHEKHE BAKWATA AWACHIMBA MKWARA RADIO IMAAN FM
SHEKHE MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM,(BAKWATA) ALHAD MUSSA AMEKIPIGA MKWARA KITUO CHA REDIO CHA KIISLAMU REDIO IMAAN FM KINACHORUSHA MASAFA YAKE TAKRIBANI SEHEMU KUBWA YA NCHI KUTOKEA MJINI MOROGORO,KWAMBA HAKINA MAMLAKA YA KUTOA TAARIFA ZA KUTANGAZA MWEZI NA AMEIOMBA SERIKALI KUKICHUKULIA HATUA KITUO HICHO KWA KUWA KIMESABABISHA KUWAPA USUMBUFU WANANCHI AMBAO WENGI WAO HAWAKWENDA MASHULENI NA MAKAZINI WAKIAMINI KUWA NI SIKU YA SIKU KUU KUTOKANA NA MATANGAZO YAKE.stori kwa hisani ya blog ya www.mkwinda.blogspot.com

Aug 30, 2011

KUTOKANA NA UKATA, NIMEFUNGA KESHO MSINITEMBELEE!!!MAAJABU YA UUMBAJI WA MWENYEZI-SHINA MOJA LAKINI MATAWI YA MITI TOFAUTI MITATU

Shina la Mti uliopo katika shule ya sekondari ya Myovizi wilayani Mbozi ambalo chini limeungana na kuwa shina moja lakini matawi yake juu yamegawanyika katika miti mitatu ya aina tofauti, kuna mkuyu, na aina nyingine mbili za miti ambayo kwa kiswahili siijui labda uniulize kikwetu!!!!

Matawi yanavyoonekana juu yakiwa mchanganyiko wa miti aina tatu

Matawi ya aina tatu yakionekana kwa uzuri zaifi


ANSWAAR SUNNA WAKISWALI IDD LEO

Waumini wa dini ya Kiislamu wa madhehebu ya Answaar Sunna wakiswali swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Aug 28, 2011

LALA SALAMA YA UCHAGUZI ZAMBIA, TIMU YA MAPAPARAZI YATUA MBEYA KUFUATILIA URAIA WA MMOJA WA WAGOMBEA

Timu ya wandishi wawili pamoja na Dereva kutoka vyombo vya habari vya serikali ya Zambia wakiwa na mmiliki wa blog hii,wakati wakirejea Zambia baada ya kutia timu kupata habari za uzao wa mmoja wa wagombea wa urais nchini humo MICHAEL SATA anayedaiwa kuwa wazazi wake walikuwa watanzania waliohamia nchini ZAMBIA kufanya kazi migodini.

Mwandishi Nebart Mbewe kushoto akizungumza jambo na Mmiliki wa blog ya Indaba, wakati wa kuagana mjini Mbozi baada ya kushindwa kuthibitisha kama Sata ni jina la watanzania, ikumbukwe kuwa mbinu za watu wanaohamia nchi za wenzetu hubadili majina ili yaendane na yale ya wenyeji wanaowakuta, hivyo kwa koo za makabila ya mkoa wa Mbeya hakuna majina ya Sata!!! kwishinei, wakarejea bila ushindi mkononi!!

Sasa mdogo wangu sijui tutaeleza nini, manake Bongo hawa majina ya sata na story tumeshaitengeneza itakuwaje|? ndivyo wanavyoonekana wakiulizana hawa washkaji!!

MBWAA!! BURUDANI MNAITAKA KAZI NI KUACHIA MSUMALI!KARIBU KYAI MUKIKOMBE KYA KYUMA!!!!

Kwa wale waliozaliwa miaka ya uhuru watakubaliana na mi kuwa vyombo hivi vilikuwa vya heshima sebuleni, kwenye kabati lenye fomeka, halafu unakunywa chai kwa adabu manake kikombe cha moto, chai ya moto, huku unyakyusani wakawa wanaita unakunywa kyai mukikombe kya kyuma kangi kya  moto!!!!!!

DUNIA NI MFULULIZO WA MATUKIO! SIKU YAKIKUKUMBA BALAA!!!!!

Hapa ni majira ya saa 5 asubuhi nikiwa katikati ya mji wa Mbeya nikaona nisafishe sura ya gari kabla sijaondoka kwenda kijijini

Nikiwa milima ya senjele nikakumbana na tatizo, kumbe wakati wanaosha gari jamaa walifungua mfuniko wa rejeta kuchungulia maji, wakasahau kurejesha, nami nikaendesha bila kuangalia, gari likazima lenyewe, tukalazimika kuvuta umbali wa kilometa 40 hadi wilayani kwangu
Nafika Kijijini nakutana na jambo jipya kabisa, kijana wangu amelazwa hospitali ati kapata jeraha wakati wanajifunza sarakasi na wenzake, kitu chenye ncha kali kimemchana kwenye paji la uso!!! kwakweli akili ilisimama kwa dakika kadhaa kufikiri, mbona ni mfululizo wa matukio? nikagundua hii ni dunia, na ina mfululizo matukio

Kumbe wiki hii nikiimaliza salama, itakuwa kumbukumbu kubwa kwangu kwa  matukio ya mfulilizo matatu yenye afya!

Aug 26, 2011

President Jonathan Speak on Suicide Attack on United Nations Building

"By today's attack, we are once again reminded of the international character of terrorism and its indiscriminate targeting of innocent civilians, I affirm Nigeria's determination to continue to play its part in the global effort to eradicate the scourge of terrorism in all its ramifications." - GEJ. #talktalk Meanwhile, not to cause any panic o, but here's a broadcast I got that I feel I should share. We might have nothing to fear in Lagos, but just in case, let's all be conscious. These animals can obviously strike at any time and any place. RIP to all those who lost their lives today. May God keep us all safe. Read the broadcast below.

Stay off the Third Mainland Bridge and surrounding areas. "Lagosians are advised to stay off the Third Mainland Bridge and surrounding areas. Unconfirmed report says terrorists plan to bomb Lagos within 24 hours of bombing the UN building in Abuja. This information comes from 1st suspect arrested in connection with the Abuja blast. The law enforcement agencies are working to thwart the latest threat. Military roadblocks and other emergency and security measures might result in traffic congestion. The use of alternative routes is strongly advised."

Aug 24, 2011

taswa yaunda kamati kuratibu tamasha la michezo kuadhimisha miaka 50 ya uhuru

TASWA imeunda Kamati ya Watu 16 kwa ajili ya kusimamia masuala ya tamasha la wanamichezo kwa ajili ya miaka 50 ya Uhuru.
Kamati hiyo itaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Uhariri ya gazeti la Raia Mwema, Johnson Mbwambo, ambaye amepata kuwa Mhariri wa Habari za Michezo wa magazeti mbalimbali nchini na pia ni miongoni mwa waasisi wa TASWA.
Pia TASWA imemteua Mhariri Mkuu wa gazeti la SpotiStarehe, Masood Sanani kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Sanani ni Mhariri mzoefu, ambapo pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Tuzo za Wanamichezo Tanzania inayoandaliwa na TASWA, ambayo Mei mwaka huu ilifanya kazi kubwa kuandaa tuzo za aina yake.
Pia wapo Wajumbe wa Kamati hiyo ya Tamasha la Miaka 50 ya Uhuru, ambao ni wahariri wa siku nyingi na wana uzoefu mkubwa na masuala ya michezo na waandishi wa michezo, wajumbe hao ni Said Salim ambaye licha ya kuwa mhariri veteran pia ni mwalimu wa waandishi wa habari, ambapo anaishi Zanzibar, jambo litakalosaidia pia kuhusishwa wanamichezo wa zamani wa Zanzibar.
Mwingine ni Mhariri wa gazeti la ThisDay, Willy Chiwango, ambaye pia mkongwe katika masuala ya taaluma ya habari na mwenye uelewa mkubwa wa mambo ya michezo.
Wajumbe wengine ni:
1. Asha Muhaji-Mhariri Leap Media
2. Rashid Zahoro- Mhariri gazeti la Burudani
3. George John-Katibu Msaidizi TASWA
4. Mahmoud Zubeiry- Mhariri Dimba
5. Mohammed Mkangara-Mhazini Msaidizi TASWA
6. Juliana Yassoda-Naibu Mkurugenzi Idara ya Michezo
7. Majuto Omary-Mwenyekiti TASWA FC
8. Ephraim Kibonde- Mtangazaji Clouds FM
9. Deo Rweyunga-Mkurugenzi Radio One
10. Chacha Maginga-Mtangazaji TBC1
11. Amour Hassan-Mhariri Nipashe
12. Zena Chande-TASWA
Chama cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU).
Katibu wa Kamati atakuwa George John Katibu Msaidizi wa TASWA. Kamati itafanya kikao chake cha kwanza Jumapili Septemba 4, 2011.
(D) Semina ya waandishi Morogoro
Maandalizi yanaendelea kuhusiana na semina kwa waandishi wa habari itakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao mkoani Morogoro na ile itakayofanyika Oktoba mkoani Arusha, ambazo tunaamini zitakuwa za manufaa kwa wadau wetu.

TMTV kurusha Muziki wa Kitanzania

TUNAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WANAOISHI NDANI NA NJE YA TANZANIA KATIKA SIKU ZIJAZO ZA KARIBU TUTAFUNGUA TELEVISHENI. CHANELI YA MUZIKI WA KITANZANIA, KWA JINA LA TANZANIA MUSIC TELEVISION {TMTV} (WWW.TMTV.CO.TZ) AMBAYO ITAKUWA INAPATIKA KWENYE MTANDAO,SETILATI,SIMU ZA MKONONI NA VING'AMUZI(DECODER) CHANELI HII ITAKUWA NA VIPINDI VIFUATAVYO: 1.BONGO BOX 2.SALAMU BOX 3.BENDI ZETU 4.TAARABU 5.ZILIPENDWA 6.NYIMBO ZA DINI 7.VIPAJI 8. HABARI ZA MUZIKI 9.SWAHILI HIP-POP 10.NYIMBO ZA UTAMADUNI ILI KUBORESHA UFANISHI WA CHANELI TUNAOMBA MAPENDEKEZO YENU KUPITIA: info@tmtv.co.tz BONYEZA HAPA KWA KUANGALIA CHANELI www.tmtv.co.tz KWA KOMPYUTA NYINGINE UTALAZIMIKA KUDOWNLOD SOFTWARE YA MICROSOFT SILVER LIGHT KWA AJILI YA KUANGALIA TV. SOFTWARE ITAJITOKEZA KTK SCREEN KWA AJILI YA KUDOWNLOD. WENU UTAWALA TANZANIA MUSIC TELEVISION

Waasi wayateka makazi ya Gaddafi mjini Tripoli

Victory in sight: Rebel fighters celebrate near a partially obscured golf buggy belonging to Gaddafi inside the leader's compoundWalibya wakishangilia kutekwa kwa makazi ya Gadhafi, Tripoli
Madarzeni ya makombora aina ya Grad yamevurumishwa mjini Tripoli mapema leo. Waasi wameyateka makazi ya kanali Gaddafi.
Mtu mmoja aliyeshuhudia ameiambia televisheni ya al-Arabiya kwamba barabara ya Al-Sour, karibu na makaazi ya Bab al-Aziziya ya kiongozi wa Libya kanali Muammar Gaddafi, inashambuliwa kwa makombora.
Waasi wameyateka makazi ya Gaddafi na kupandisha bendera yao, lakini hawamkumpata kiongozi huyo wala wanawe. Kumekuwa na shangwe na nderemo katika kiwanja cha Kijani na barabara za mji mkuu Tripoli. Wafuasi wa Gaddafi wangali wanaendeleza upinzani katika baadhi ya sehemu za mji huo, na wanaidhibiti hoteli ya Rixos, makao makuu ya waandishi wa habari wa nchi za kigeni, na wanawazuia wasitoke.
Gaddafi aapa kuichoma Libya
Kufikia sasa Gaddafi hajulikani aliko, lakini amesema katika hotuba iliyotangazwa na redio moja ya Tripoli, na kuripotiwa na televisheni ya Al-Orouba, kwamba kuondoka kwake kutoka makazi yake ni mbinu ya kivita. Gaddafi pia ameapa kufa kama shahidi au apate ushindi dhidi ya jumuiya ya kujihami ya NATO.
Mtu mmoja aliyeshuhudia ameiambia televisheni ya al-Arabiya kwamba barabara ya Al-Sour, karibu na makaazi ya Bab al-Aziziya ya kiongozi wa Libya kanali Muammar Gaddafi, inashambuliwa kwa makombora.
Waasi wameyateka makazi ya Gaddafi na kupandisha bendera yao, lakini hawamkumpata kiongozi huyo wala wanawe. Kumekuwa na shangwe na nderemo katika kiwanja cha Kijani na barabara za mji mkuu Tripoli. Wafuasi wa Gaddafi wangali wanaendeleza upinzani katika baadhi ya sehemu za mji huo, na wanaidhibiti hoteli ya Rixos, makao makuu ya waandishi wa habari wa nchi za kigeni, na wanawazuia wasitoke.
Gaddafi aapa kuichoma Libya
Kufikia sasa Gaddafi hajulikani aliko, lakini amesema katika hotuba iliyotangazwa na redio moja ya Tripoli, na kuripotiwa na televisheni ya Al-Orouba, kwamba kuondoka kwake kutoka makazi yake ni mbinu ya kivita. Gaddafi pia ameapa kufa kama shahidi au apate ushindi dhidi ya jumuiya ya kujihami ya NATO.
Fedha zilizowekwa na utawala wa Gaddafi katika nchi za kigeni, zilizuiliwa na Umoja wa Ulaya, Marekani na mataifa mengine ya magharibi, kufuatia hatua ya kiongozi huyo kukandamiza upinzani dhidi ya utawala wake. Bi Ashton amesema Libya ina uwezo wa kuimarisha uchumi wake kwa haraka na hatarajii kutolewa msaada wa kiuchumi kwa ajili ya nchi hiyo.
Ashton amesema wanataka uhuru na demokrasia katika maisha ya kila siku ya Walibya. Amependekeza mkutano mwingine Ijumaa wiki hii mjini New York wa kundi la Cairo kwa ajili ya Libya, mkutano unaowaleta pamoja viongozi wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na jumuiya ya nchi za Kiarabu. Umoja wa Ulaya utakuwa na jukumu muhimu katika kibarua kigumu cha kukusanya silaha zilizotapaa mjini Tripoli.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, amesema jumuiya ya kujihami ya NATO itaendelea na harakati yake ya kijeshi nchini Libya mpaka usalama utakapoimarika kikamilifu.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Benghazi, akiwa ameandamana na mwenyekiti wa baraza la kitaifa la mpito, Abdel Jalil, waziri Davutoglu alisema mali za Libya zinazozuiliwa zinapaswa kuachiwa kabla kumalizika kwa mwezi wa Ramadhani kwa manufaa ya Walibya.
Aliongeza kusema kuwa Walibya wanahitaji fedha kwa dharura kwa ajili ya kuijenga Libya huru na yenye demokrasia. Davutoglu alisisitiza umuhimu wa kuulinda umoja wa Libya na mipaka yake, na kuiahidi Libya msaada kamili wa umma wa Uturuki.
Wafadhili wakutana Doha
Mawaziri wa kigeni wa nchi za kiarabu wamewataka Walibya wajiepushe na kulipiza kisasi kwa ajili ya kuijenga Libya mpya. Mawaziri kutoka Qatar, Saudi Arabia na Misri waliokutana mjini Doha kwenye kikao cha kamati ya amani cha jumuiya ya nchi za kiarabu, pia wamelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa haraka kuachia dola bilioni 2.5 mali za Libya zinazozuiliwa, kulipa mishahara na kugharamia misaada ya kiutu nchini Libya.
Mawaziri hao wamependekeza kulialika baraza la kitaifa la waasi kwenye mkutano wa mawaziri wa kigeni wa jumuiya ya nchi za kiarabu utakaofanyika Jumamosi ijayo, kujadili matukio katika ulimwengu wa kiarabu, ikiwemo Libya na Syria.
Qatar leo itandaa mkutano wa mataifa fadhili kuliwezesha baraza la kitaifa la mpito kupata dola bilioni 2.4 ili kuliwezesha kulipa mishahara ya Walibya kabla siku kuu ya Eid na kugharamia matibabu na miguu bandia inayohitajika na watu waliojeruhiwa.
Mwandishi: Josephat Charo/RTRE/AFPE/DPAE

HINA IZOOO....MKAPRINT MPAKE EID