Adverts

Aug 23, 2011

bunge lazizima kwa kifo cha Mkewe mbunge Mussa Khamis Silima

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh Samwel Sitta (shoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh William Lukuvi (kulia) na kaimu Katibu wa Bunge wakipanga mikakati ya kufanikisha shughuli hii ya msiba katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kufuatia ajali ambayo alipata
Mbunge mteule kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mussa Khamis Silima, alipata ajali juzi katika eneo la Nzuguni, Dodoma, ambapo mkewe, Mwanaheri fahari, alifariki dunia na yeye na dereva wake kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospital ya Muhimbili kwa matibabu zaidi
Mwili wa mke wa Mbunge Mussa Khamis Silima, Hayati Mwanaheri, ukiombewa dua na Wabunge n waombolezaji wengine baada ya kuwasili katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa mjini Dodoma leo kuswaliwa kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi. Marehemu alifariki Jumapili jioni kwa ajali ya gari katika eneo la Nzuguni, nje kidogo ya mji wa Dodoma
Mwili wa Marehemu ukiingizwa msikitini kuswaliwa kabla ya safari
Gari la mafuta lililohusika katika ajali hiyo ambapo mfanyakazi wake anaonesha mahali ambapo gari dogo lililokuwa na marehemu na mumewe kugonga wakati likitaka kupita
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo akimweleza mbunge wa Mafia, Mh Shah, kilichotokea
Mbunge wa Mafia Mh. Shah akiliangalia gari dogo la Mh. Silima lilivyoharibika baada ya ajali hiyo
Baadhi ya wabunge wakiwa chumba cha maiti cha hospitali ya Dodoma kusubiri kuchukua mwili wa marehemu
Dereva Chezani Sebunga aliyekuwa akiendesha gari la Mbunge, Mussa Khamis Silima na kupata ajali eneo la Nzuguni, Dodoma , akiwa katika machela akiingizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo asubuhi, akitokea mkoani Dodoma. Mke wa Mbunge Silima, Mwanaheri Fahari alifariki dunia katika ajali hiyo. Mbunge mteule kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mussa Khamis Silima, ambaye alipata ajali juzi katika eneo la Nzuguni, Dodoma, akiwa katika machela baada ya kushushwa kwenye gari jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, alikoletwa na ndege kutoka Dodoma. Mke wake, Mwanaheri Fahari alifariki na dereva wao Chezani Sebunga alijeruhiwa kwenye ajali hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA