Adverts

Aug 23, 2011

kutoka bungeni dodoma leo

Mbunge wa Ilala Mh. Azzan Zungu na Mbunge wa Mafia Mh. Shah akiperuzi kitabu cha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji iliyowasilishwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. Steven Wassira kwa niaba ya Waziri wa Maji profesa Mark Mwandosya ambaye yuko nchini India kwa matibabu. Kwa mujibu wa Spika Anne Makinda hali ya Profesa Mwandosya inaendelea vyema, Bajeti ya wizara ya Maji inajadiliwa kwa siku mbili na wabunge wengi waliochangia wameitaka serikali ifanya kila iwezalo kutatua tatizo sugu la maji nchini
Mbunge wa Magu Mh. John Cheyo, Mbunge wa Kigoma Kusini Mh. David Kafulila na Mbunge wa Vunjo Mh. Augustine Lyatonga Mrema wakiwa bungeni leo
Viongozi wa Wizara ya Maji, EWURA na wadau wa maji wakifuatilia kinachoendelea bungeni leo
Sehemu ya Wabunge ambao ni mawaziri
Baadhi ya wabunge kikaoni
Baadhi ya waheshimiwa wabunge bungeni
Toka shoto ni Mbunge wa Lushoto Dr Abdallah Kigoda, Mbunge wa Tabora Mjini Mh Aden Rage na Mbunge wa Singida kusini Mh. Mohamed Misanga. Mh. Rage pia ni Mwenyekiti wa Simba wakati Mh Misanga ni mwenyekiti Mstaafu wa Yanga
Mbunge wa Mafia Mh Abdulkarim Hassan Shah akiongea na mdogo wake na kaka bungeni leo
Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda (kulia) akiongea na Mbunge wa Musoma mjini Mh Vicent Nyerere
Mbunge wa Korogwe vijijni Mh Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu (shoto) na Waziri wa Fedha na mbunge wa Mh Mustafa Mkullo wakiangalia magazeti ya leo yanayouzwa bungeni
Mbunge wa Bumbuli, Mh January Makamba (shoto), Mbunge wa Sumve Mh Richard Ndassa (kulia) wakiongea na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Tolly Mbwete wakati wa mapumziko