Adverts

Aug 28, 2011

LALA SALAMA YA UCHAGUZI ZAMBIA, TIMU YA MAPAPARAZI YATUA MBEYA KUFUATILIA URAIA WA MMOJA WA WAGOMBEA

Timu ya wandishi wawili pamoja na Dereva kutoka vyombo vya habari vya serikali ya Zambia wakiwa na mmiliki wa blog hii,wakati wakirejea Zambia baada ya kutia timu kupata habari za uzao wa mmoja wa wagombea wa urais nchini humo MICHAEL SATA anayedaiwa kuwa wazazi wake walikuwa watanzania waliohamia nchini ZAMBIA kufanya kazi migodini.

Mwandishi Nebart Mbewe kushoto akizungumza jambo na Mmiliki wa blog ya Indaba, wakati wa kuagana mjini Mbozi baada ya kushindwa kuthibitisha kama Sata ni jina la watanzania, ikumbukwe kuwa mbinu za watu wanaohamia nchi za wenzetu hubadili majina ili yaendane na yale ya wenyeji wanaowakuta, hivyo kwa koo za makabila ya mkoa wa Mbeya hakuna majina ya Sata!!! kwishinei, wakarejea bila ushindi mkononi!!

Sasa mdogo wangu sijui tutaeleza nini, manake Bongo hawa majina ya sata na story tumeshaitengeneza itakuwaje|? ndivyo wanavyoonekana wakiulizana hawa washkaji!!