Adverts

Oct 25, 2011

Mhe. Kikwete Akabidhiwa NBC Debt Master Card

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akionyesha kadi yake mpya ya NBC Debit Master Card mara baada ya kukabidhiwa na maofisa wa Benki ya NBC Ikulu, Dar es Salaam hivi karibuni. Kadi ya NBC Debit Master Card ilizinduliwa na benki hiyo Oktoba 18 mwaka huu. Kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la Corporate Bi. Jacqueline Sindano Mkuu wa Shughuli za Kibenki wa NBC, William Kallaghe na Mwakilishi wa Mauzo, Emmanuel Mseti.
Ris Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akijaza fomu ili kupata kadi mpya ya Debit Master Card ya Benki ya NBC Ikulu, Dar es Salaam hivi karibuni. Kadi ya NBC Debit Master Card ilizinduliwa na benki hiyo Oktoba 18 mwaka huu. Wanaomsaidia Rais kutoka kushoto ni, Meneja Tawi la Corporate Bi. Jacqueline Sindano, Mkuu wa Shughuli za Kibenki, William Kallaghe na Mwakilishi wa Mauzo, Emmanuel Mseti.
Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mkuu wa Shughuli za Kibenki wa NBC, William Kallaghe na baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliokwenda Ikulu, Dar es Salaam hivi karibuni ambako walimkabidhi kadi mpya ya NBC Debit Master Card. Kushoto ni Mwakilishi wa Mauzo, Emmanuel Mseti na Meneja wa Tawi la Corporate, Jacqueline Sindano.