Adverts

Nov 30, 2011

TIMES RADIO FM YAZALIWA UPYA LEO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Times Radio FM, Rehule Nyaulawa akielezea historia na mafanikio ya kituo hicho, wakati wa hafla ya kukitambulisha upya kituo hicho, Dar es Salaam jana.Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2000, hivi sasa kinaongoza kusikilizwa na watu wengi katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiy, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam.


Mmoja wa watangazaji wa Times Radio FM, Ali Masoud 'Kipanya' akiongoza hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Times Radio FM, Rehule Nyaulawa (katikati), akiwa na aliyemwakilisha mgeni rasmi, Sihaba Nkinga (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, SihabaNkinga akihutubia kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Emmanuel Nchimbi, wakati wa hafla hiyo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Times Radio FM, Rehule Nyaulawa (kulia) akigana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga baada ya hafla hiyo kumalizika.