Adverts

Dec 10, 2011

MH SUGU ATANGAZA KUSUSIA BIDHAA ZA AIRTEL KWA KILE ALICHOITA MCHEZO MCHAFU

Katika kile kinachoonekana, mtiti unazidi kukua, Kampuni ya Clouds imetangaza kuendelea kufanya matamasha mikoani huku ikiwa ratiba zake zikiingiliana na kundi la Vinega linalopinga udhalimu dhidi ya wasanii wa kizazi kipya ambalo ratiba yake ni mwendelezo wa kuamsha wasanii katika kanda zote nchini.
Habari ambazo indabaafrica blog imezipata zinaonyesha kuwa Clouds wamepanga kufanya show jijini Mbeya jimboni kwa mh Sugu tarehe ambayo tayari Sugu alishatangaza kufanya show kama ile ya jijini Dar Tarehe 24 Decemba 2011. Kutokana na hali hiyo kunajenga mashaka kama vyombo vya dola vitaachia mazingira ya vita vya ushindani huu uendelee kwa kufanya matamasha eneo moja kwa siku moja kwani, sura ya mbeya inaeleweka ni vyema busara zikachukua nafasi kupitia vyombo vya dola kudhibiti hali hiyo. hapa ni sehemu ya ujumbe uliopo kwenye ukurasa wa Mh Sugu katika facebook wall page yake!
Na naomba nitoe msisitizo kwa mara nyingine,ubunge haunizuii kuendelea na harakati za sanaa kama ambavyo ubunge haumzuii mh tundu lissu ambaye ni wakili kufanya kazi za sheria!cha msingi ni kutosahau majukumu ya wananchi,kitu ambacho nafurahi tunaenda sawa nacho kabisa...so tutaendeleza harakati humu fb na twitter,na kwa anayependa kufuatilia shughuli zetu jimboni namkaribisha atembelee
 
‎...boycott CLOUDS FM...boycott AIRTEL na huduma zao zote kama AIRTEL-MONEY kwa sababu watumishi wake kama Twisa wanashirikiana kwa hila na wanyonyaji hawa wa wasanii...mfano ni kitendo cha Twisa kuwasapoti Clouds kwa fedha za AIRTEL na katika mazingira ya 'TATA' bajeti ya kuzunguka mikoani na wasanii ili kuwaharibia VINEGA wa ANTI-VIRUS tour yao ya kitaifa...THIS IS LONG WAR!!!