Adverts

Nov 14, 2012

MGAMBO KUKABA NAFASI ZA RAIA KWENYE MAKAMPUNI YA ULINZI


Na  Magreth Sikambale

Mafunzo ya awali ya Mgambo yaliyodumu kwa kipindi cha miezi mitatu yakishirikisha vijana 80 kutoka kata za Iyula na Ruanda wilayani Mbozi ,yamefungwa rasmi leo na Ruteni kanali Emanuel Mwikuka.
Akifunga mafunzo hayo, Kanali Mwikuka ametoa wito kwa vijana nchini  kujtokeza na kushiriki  katika mafunzo hayo ili kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa na wanchi wenzao  ujumla.
Alisema hayo wakati akijibu risala ya washiriki hao iliyoeleza kuwa vijana wengi wamekua wakikwepa kujiunga na mafunzo hayo kwa dhana kuwa mafunzo hayo ni mateso na hayana umuhimu kwao.
Kanali Mwikuka amesema,  mafunzo hayo hayataishia hapo bali kutakuwepo kozi nyingine kwa wale walio fuzu.
Ameongeza kuwa lengo la kuweka msukumo kwenye  mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuimarisha ulinzi, na kwamba  jeshi lina mpango wa kuondoa wananchi walio ajiliwa katika sekta ya ulinzi  ambao hawajafuzu mafunzo ya Mgambo  na badala yake nafasi zao zitachukuliwa na waliohitimu mafunzo ya mgambo.
“vijana  mtakuwa na  nafasi kubwa yakupata ajira katika ngazi za Serikali na Sekta binafsi” aliongeza Kanali Mwikuka.
Sambamba na hayo pia aliweza kuwatunuku vyeti washiriki wa 5 waliyofanya vizuri katika mafunzo hayo Rebeka Mbembela, Jonas Mgala, Musa Mgala, Heneriko Shonde, na mwile Stanlesi.
Katika risala iliyosomwa na Elia Japhet, wahitimu hao walieleza kuwa mafunzo yao yalianza mwezi Julai mwaka huu na kwamba walianza mafunzo hayo ni 120 hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali washiriki 40 waliishia njiani.
Mbali na hayo  taarifa fupi  ilisomwa na mshauri wa mgambo wa wilaya ambapo amesema vijana hao wameweza kujifunza mambo muhimu yanayotakiwa kufundishwa katika mafunzo ikiwemo elimu juu ya rushwa toka Takukuru, ulinzi na usalama wa  nchi.

Katika Maadhimisho hayo Kanali Mwikuka pia alikagua gwaride la wahitimu wa mgambo kabla ya kuwatunuku zawadi washindi mbalimbali.


MAFUNZO YA MGAMBO MBOZI YAFIKIA UKINGONI w


Kanali Emanuel Mwikuka  ambaye alimwakilisha Mshauri wa mgambo mkoa

Add caption

Mgambo wakila kiapo mbele ya mgeni rasmi

Gwaride la Mgambo katika maonyesho ya kugfunga mafunzo tarafa ya Iyula


Wakipita kutoa heshima mbele ya mgeni rasmi, hii ni staili ya SOOOOSI UP SOOOS UP

Hapa wakiwa kwenye hatua za awali za Paredi

Askari wa Mgambo wakionyesha uwezo wao katika kukamili matukio mbalimbali ya kivita

Wahitimu wa mafunzo ya Mgambo wakiwa kwenye maonyesho ya medani za kivita




PICHA NA CHARLES SHITINDI

Nov 11, 2012

Msaidizi wa askofu wa KKKT Dayosisi ya Konde Mchungaji Geofrey Mwakihaba akitamka neno la baraka kabla ya kuuweka mche wa mparachihi  kwenye shimo tayari kuupanda ikiwa ni hatua ya kuzingua program ya sharika, majimbo na taasisi za Kilutheri kwenye Dayosisi hiyo katika upandaji wa miti kama sehemu ya hifadhi ya mazingira.


Msaidizi wa askofu  mchungaji Mwakihaba akipanda mche wa mparachichi kwenye kituo cha watoto kinachoendelea kujengwa kwenye usharika wa Vwawa

Mkuu wa Jimbo la Magharibi Mch. Mwambola akizungumzia uendelezaji wa program ya hifadhi mazingira kwenye sharika za jimbo hilo


Mwanafunzi wa  kipaimara  akipanda mti kama sehemu ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Makanisani na kwa waumini lililoanza msimu huu kwa KKKT dayosisi ya Konde

Pia familia ya Danny Tweve imeshiriki kwenye ibada  hiyo ikikumbuka miaka minne iliyopita ambapo Mch Mwakihaba ambaye alifungisha ndoa hiyo hapakuwa na matunda haya kwa mtoto wa kiume  na aliyebebwa 


Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Konde, imetoa maelekezo kwenye majimbo na sharika zake kujielekeza katika utekelezaji wa mipango ya kuhifadhi mazingira ili kuepusha  madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kushindwa kutawala vyema mazingira kwenye maeneo yao.
Akizungumza kwenye ibada ya Kipaimara  katika usharika wa  Vwawa wilayani Mbozi Msaidizi wa Askofu Mch. GEOFREY MWAKIHABA amesema utaratibu uliobuniwa na uongozi wa jimbo la Magharibi utasaidia kuwakumbusha waumini na wananchi kwa ujumla juu ya uhifadhi wa mazingira
Amesema jimbo hilo limeanzisha utaratibu wa kupanda miti kila msimu wa mvua unapoanza na kwamba kanisa linatumia fulsa ya ibada maalumu kama za kipaimara na ubatizo kwenye nyakati hizo kuzindua kampeni za upandaji miti  kama kanisa, na waumini wake.
Amefafanua kuwa hatua hiyo pia itasaidia watoto kujihusisha zaidi na shughuli za kutunza mazingira kutokana na kuandaliwa katika malezi yao wakijua umuhimu wa raslimali rafiki za mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wake

Oct 25, 2012

big4regions: STACO LTD GOWDON CLOSED TODAY AFTER ALLEGATION OF ...

big4regions: STACO LTD GOWDON CLOSED TODAY AFTER ALLEGATION OF ...: STACO LTD a  agency company selling fertilizers in Mbozi District, has closed today by officials from ministry of Agriculture who accompanie...

Oct 16, 2012

UCHAGUZI WA CCM MBEYA, ZAMBI AULA

Mmoja wa wapiga kura akiwa anatumbukiza kura yake kwenye kapu la uchaguzi


ELIMU YA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWA WAJENZI WA BARABARA TUNDUMA- SUMBAWANGA

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya waelimisha rika kwenye eneo la ujenzi wa barabara ya Tunduma -Sumbawanga wakiwa kwenye picha ya pamoja katika shule ya JK Nyerere

Oct 12, 2012

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa India


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia) akisalimiana na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw aliyefika ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri kwa lengo la kujitambulisha ambapo pia walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Mhe. Naibu Waziri (kushoto) akizungumza masuala mbalimbali na Mhe. Balozi Shaw wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha.
Mhe. Balozi Shaw (kushoto) akizungumza  huku  Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza kwa makini.
Mhe. Balozi Shaw akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri.
Mhe. Naibu Waziri akiendelea na mazungumzo na Mhe. Balozi Shaw. Wengine katika picha ni Bw. Charles Faini (kushoto kwa Mhe. Naibu Waziri), Afisa Mambo ya Nje na Bw. D.K. Pant (kulia kwa Mhe. Balozi) Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini.
KUTOKA BLOG YA MTAA KWA MTAA

ABBAS KANDORO AONYA WATAALAMU WA KILIMO KUFANYA KAZI KWA MAZOEA


MKUU wa Mkoa wa Mbeya Bw.Abbas Kandoro amewaonya wataalamu wa kilimo kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kukaa maofisini badala ya kwenda mashambani waliko wakulima na ili waweze kusaidiana wakulima kujua mbinu za bora za kuboresha mazao yao kuliko kuendelea kufanya kazi za kilimo bila wataalamu kilimo kuwepo .

Mwandishi wetu Esther Macha anaripoti kutoka Mbeya kuwa Bw. Kandsoro alisema wataalamu wa kilimo wanapaswa kuwa karibu na wakulima wao waliopo vijijini kuliko mazoea yaliyojengeka miongonbi mwao yao ya kukaa maofisini kusubiri taarifa za kilimo wakati taaluma yao inawataka kufika mashambani waliko wakulima wenyewe.

 Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo baada ya kupewa taarifa ya idara ya kilimo ya halmashauri ya wilaya ya Mbeya alipofanya ziara na ndipo akakutana na madudu kama aliyosikia kwenye tarifa ya wilaya ya Mbozi na kuikataa.

 Alisema hatua iliyopo kwa wataalamu kutokuwa karibu na wakulima ndiyo chanzo kikubwa cha wachuuzi kupata fursa ya kwenda majumbani kwa wakulima na kununua mazo kisha wanaondoka nayo pasipo hata kulipa ushuru.


Bw. Kandoro alisema madudu hayo ni pamoja na kuwepo kwa takwimu zinazoonyesha taarifa za makadirio ya mavuno ya nafaka hali iliyoashiria mavuno bado yanaendelea ama hayajafanyika wakati umekwisha hivyo kulipaswa kuwepo takwimu sahihi na si matarajio tena.

“Ndugu zangu hatuwezi kwenda katika utaratibu kama huu haiwezekani kabisa.Unasema shughuli zinaendelea! Wapi wanaendelea kuvuna mpaka leo hii?.Hivi unajua tayari tuko katika msimu mwingine wa kilimo?” alihoji Bw.Kandoro.

“Kwa nini mnafanya kazi ya kukokotoa takwimu mkiwa maofisini?Na hili nimeliona mahala pengi eneo la kilimo lin a ubabaishaji mkubwa.Mabwanashamba wapo lakini kila kukicha wanacheza na takwimu maofisini.Vijijini waliko wakulima hawaonekani”


Alisisitiza kuwa  utaratibu maalumu wa ukusanyaji takwimu zinazohusiana na kilimo ikiwemo kupeleka maaofisa takwimu katika magulio ili waweze kujua ni kiasi gani cha mazao kinauzwa.

KUTOKA FRANCIS GODWIN BLOG

UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA MBEYA, MKWE KIONGOZI ANYANYULIWA NJE




Na francisgodwin.blogspot.com

USAILI wa wagombea wanaowania nafasi  mbalimbali  za uongozi  katika chama cha soka  mkoa wa Mbeya, (MREFA), jana uligubikwa na vituko vya aina yake,  baada ya mmoja wa wagombea wa nafasi ya Uenyekiti,  kumkataa mjumbe wa kamati ya uchaguzi kwa madai kuwa ana mgongano wa kimasilahi na mpinzani wake.

Mjumbe wa Kamati ya uchaguzi aliyekataliwa na kulazimika kutolewa ndani ya chumba cha usaili ili haki itendeke kwa mgombea ni Katibu, Prince Mwaihojo, ambaye anadaiwa kuwa ni Mkwe wa mgombea mmoja wa nafasi ya Uenyekiti John Mwamwaja.

Mtandao  huu umeshuhudia katibu huyo wa Kamati ya uchaguzi, akitoka nje muda mfupi tu baada ya mmoja wa wagombea ya nafasi ya uenyekiti Elias Mwanjala, alipoitwa ndani ya chumba cha usaili.

Alisema kuwa haiwezekani mimi nihojiwe na mtu ambaye anamafungamano ya kidamu na mpinzani wangu, ndio maana nilipofika ndani ya chumba cha usaili nilitoa angalizo na nashukuru Mwenyekiti alielewa na kukubali kumtoa nje.

Kwa upande wake, Mwaihojo alipoulizwa juu ya sakata hilo la kukataliwa,  alikiri kuwa lilitokea na si la ajabu katika mahala popote ambapo haki inaafutwa, hivyo kitendo hicho hakizuii mchakato wa kuwapata viongozi wa chama hicho.

Akitoa taarifa ya mchakato wa zoezi hilo baada ya kumalizika, Mwaihojo alisema zoezi hilo la usaili kwa limefanikiwa kwa asilimia 90 kwa kuwa wagombea 14 walifanyiwa usaili na kubakiza wagombea wanne tu ambao watamalizia hawakufanyiwa.

Kwa mujibu wa Mwaihojo, wagombea wanne ambao hawajafanyiwa usali ni Katibu anayemaliza muda wake Lawrence Mwakitalu, Andongwisye Panja, Thomas Kasombwe Sinkwembe ambao wote walitoa udhulu kutokana na kukabiliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kusimamia mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa.

Uchaguzi wa MREFA unatarajia kufanyika oktoba 27, jambo litakalowezesha kupatikana kwa uongozi mpya utakaohudumu kwa miaka mine kama katiba ya chama hicho inavyoeleza.

 Amewataja watu waliojitokeza kuomba nafasi za uongozi  kwa nafasi ya Mwenyekiti kuwa ni John Mwamwaja ambaye ni makamu Mwenyekiti wa uongozi unaomaliza muda wake, wakati wengine ni Majuto Mbuguyo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanga, pamoja na Elias Mwanjal ambaye katika uchaguzi Mkuu uliopita aligombea ubunge katika jimbo la Kyela na kuangushwa vibaya na mbunge wa sasa Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye pia ni Waziri wa Uchukuzi.


Makamu Mwenyekiti ni  Omary Mahinya, wakati nafasi ya Katibu Mkuu, Lawrence Mwakitalu, anayemaliza muda wake,Suleiman Haroub na Redson Kaisi, ambapo Katibu Msaidizi ni William Mwamlima na nafasi ya Mkutano Mkuu wa Taifa Tahdeo Kalua na Danny Korosso.

Kwa upande mweka Hazina ni Asajile Kavenga, Uswege Luhanga, wakati wajumbe wa kamati ya utendaji ni Lwitiko Mwamndela, Thomas Kasombwe, Boniface Sinkwembe.
Mwisho.

UTAPELI WA KUTUMIA MAJINA YA VIONGOZI KWENYE M-PESA WAWAUMIZA WANANCHI

Wizi mpya ulioanza hivi sasa kwenye mifumo ya fedha ya kielektronikia ikiwemo MPESA, umewaliza wananchi wengi wilayani Mbozi ambapo jana jioni mmoja wa viongozi wa chama cha walimu alilizwa kiasi cha zaidi ya Milion Moja imefahamika.
Akizungumza wakati akifuatilia kwenye kituo kimojawapo kinachotoa huduma za MPESA katika mji wa Vwawa, kiongozi huyo wa kike alifikwa na tukio hilo baada ya kupigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni George Lubeleje ambaye ni Mbuge wa jimbo mojawapo la mkoa wa DODOMA akimtaka amsaidie kiasi cha shilingi 600,000 za mafuta wameishiwa wakiwa mikumi wakisafirisha maiti kwenda sumbawanga.
Inaelezwa kuwa kwakuwa anamfahamu, aliomba pia mwenyeji huyo amfanyie booking ya hoteli katika mji wa Vwawa ili ujumbe huo uweze kupumzika angalau usiku mmoja kabla ya kuendelea na safari ya kupeleka maiti Sumbawanga.
Mama huyo alifanya haraka kutoa fedha benki na kuzituma kwenye simu ya mheshimiwa huyo akijua ndiye Lubeleje halisi, na baada ya kutuma fedha hizo ripoti ya fedha kutumwa kwa njia ya MPesa ilionyesha kuwa jina ambalo fedha zimepokelewa ni George Lubeleje.
Hata hivyo dakika chache baada ya fedha kuingia kwenye simu hiyo, inaelezwa kuwa mh huyo feki alipiga simu tena kwa mwalimu huyo na kumweleza kuwa zimeingia lakini bahati mbaya tangu asajiri simu yake hajawahi kutumia huduma ya mpesa, hivyo alimwomba awapigie voda ili wazirejeshe fedha hizo na badala yake atumie simu ya dereva wake ambaye ana uzoefu wa kutumia huduma hizo za Mpesa.
Mwanamke huyo alisisitizwa kuwa angekopa mahala popote ili waweze kuondoka pale walipo waendelee na safari wakati yeye akiendelea kushughulikia kurejesha fedha hizo kutoka Vodacom, hata hivyo baada ya kutuma fedha hizo mara ya pili alienda kufuatilia kwenye kituo cha kutolea fedha lakini ikabainika kuwa fedha za awali zimechukuliwa.
Licha ya kuwasiliana na kampuni ya vodacom, majibu ya mtoa huduma hayakuonyesha kutii kiu ya mama huyo na kuamua kwenda kituo cha polisi cha Vwawa ili kutoa taarifa kuwezesha uchunguzi kufanyika kwakuwa inaonyesha kuwa mtandao huo umeingia kwa kasi wilayani mbozi na tayari watu wengi wamelizwa kutokana na aina hiyo ya utapeli.
Watu wanajiuliza imekuwaje watu wajisajiri kwa majina ya viongozi na mawaziri na makampuni ya simu yameendelea kukaa kimya bila kufuatilia taarifa za usajiri zinazofanywa hivi sasa na mawakala maarufu kama freelancers na kudanganywa na matapeli kutokana na uelewa mdogo walio nao baadhi yao.

Oct 8, 2012

MPISHI MAARUFU KUTOKA INDIA ATIA TIMU BONGO NA KUTOA SOMO

Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam jinsi vyakula vya asili vinavyoweza kuwavutia watalii kwenda kutembelea nchi mbalimbali na hivyo kukuza utalii wa nchi husika huku Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akimsikilia kwa makini. Mpishi Kapoor amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.


Mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki leo jijini Dar es Salaam kitabu kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India.  Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. 

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kitabu alichopewa na mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor  kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India. Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya  asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India. 


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki (kushoto) akimkaribisha mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev  Kapoor ili aweze kuongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam ili aweze kuongea nao kuhusu umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii wa utamaduni. Kulia ni Naibu Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena Daniel Sambai ambayo imegharamia gharama za  chakula na maladhi kwa mpishi huyo kwa kipindi chote  atakachokuwepo nchini. 
Picha na Anna Nkinda - Maelezo

SHIMIWI IKULU SPORTS YAWIKA NA KUTWAA VIKOMBE KIBAO



Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Ikulu Bw Peter Ilomo Akikagua timu ya Ikulu sports club ya kamba wanaume aliyemwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kwenye kilele cha mashindano ya Shimiwi mkoani Morogoro jumamosi tarehe 6.10 2012.
Timu ya Netball ya Ikulu sports club wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wao kabla ya fainali na timu ya Wizara ya Afya Ikulu sports club ilishida kwa magoli 50- 25 kuwa washindi wa kwanza.
Wachezaji wa Ikulu sports club na Wafanyakazi wenzao ambao walienda kushangilia timu yao wakifurahia baada ya kushinda na kupata vikombe vitano kwenye michezo ya Mpira wa pete, kamba wanaume, kamba wanawake, kuendesha baiskeli, na mshindi wa pili Riadha.
Ikulu sports club Kamba wanaume wakifurahia kikombe baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.
Ikulu sports club yaongoza Yapata vikombe vitano kwenye mashindano ya Wizara na Taasisi za serikali (SHIMIWI) Mashidano hayo yalifanyika Mkoani Morogoro na kufungwa na Katibu Mkuu Ikulu Bw Peter Ilomo. 
KUTOKA MICHUZI BLOG

Tuzo za Uandishi wa Habarai za Utalii wa Ndani na Uhifadhi yaanzishwa na TANAPA



Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Bw. Pascal Shelutete akiongea na wanahabari mjini Arusha mwishoni mwa wiki ambapo aliatangaza kuanzishwa kwa Tuzo za Uandishi wa Habarai za Utalii wa Ndani na Uhifadhi ambapo kuanzia mwaka huu amesema TANAPA itakuwa ikikitambua, kutahmini na kutoa tuzo kwa waandishi watakaoandika habari zitakazohamasisha Utalii wa Ndani na Uhifadhi katika HIFADHI ZA TAIFA. Namna ya kuingia kwenye shindano hilo 
HABARI ZAIDI NENDA KWENYE BLOG YA MUHIDIN MICHUZI



KUPANDA OVYO KWA BEI YA MAFUTA KWACHANGIA MWITIKIO MDOGO WA MATUMIZI YA TREKTA MBOZI



Mbozi

Kupanda ovyo kwa gharama za mafuta kumetajwa kuwa na athari za kiwango cha juu katika uendeshaji wa kilimo cha kisasa na hasa matumizi ya zana kama trekta na vikokotozi maarufu kama powertillerkwenye wilaya maarufu kwa kilimo cha mahindi imefahamika.

Katika taarifa ya utafiti  aliyoiwasilisha Chuo cha Mipango Dodoma kwaaajili ya kuhitimu  stashahada ya uzamili katika mipango ya Mikoa, mtafiti Danny Tweve ameeeleza kuwa, katika  sampuli ya watu 103 walioshiiriki kwenye utafiti huo ni watu 4 tu waliokiri  kutumia teknolojia ya kisasa katika kulima mashamba yao.

Asilimia 98 ya washiriki wa utafiti walikiri kutumia jembe la mkono na wanyama kazi , na walipohojiwa sababu za kutotumia trekta ama powertiller kwa sehemu kubwa sababu zilizotolewa zilielekezwa kwenye gharama za mafuta kutovutia watu kuendelea kutumia teknolojia hiyo licha ya kutambua ukweli kwamba hurahisisha kazi.

Ingawa katika miaka ya 80 wilaya ya mbozi iliweza kupandisha idadi ya watumiaji wa teknolojia ya trekta kupitia mipango ya vijiji vya Ujamaa, gharama za mafuta, ukosefu wa vipuli na gharama za bidhaa hizo zilirejesha nyuma mwitikio wa wananchi hatua ambayo wengi wa wakulima walihamia kwenye matumizi ya jembe la mkono na wanyama kazi.
Utafiti huo uliofanywa katika vijiji vya Ivwanga na Mbimba unaonyesha kuwa kutokana na hali hiyo wananchi wengi wanapenda kubadili kilimo chao kutoka kile cha jembe la mkono kwenda kilimo cha kutumia zana za kisasa, hata hivyo suala la bei ya mafuta linaendelea kuwa kikwazo kwakuwa Dar es salaam ambako hawalimi ndiko mafuta yanakouzwa kwa bei ya chini ikilinganishwa na mikoani ambako mahitaji kwa shughuli za kilimo ni makubwa zaidi.
Bei ya Diesel katika wilaya ya Mbozi kwa wakati ambapo utafiti huo ulikuwa unafanywa ilikuwa ni shilingi 2300 ilihali mafuta hay ohayo jijini Dar es salaam ilikuwa 2005  kiwango ambacho kinathibitisha kuwa serikali haijaweka nia ya dhati kumsaidia mkulima kuondoknaana kilimo cha jembe la mkono.
Kutokana  na gharama kubwa za vilainishi, trekta bado limeendelea kuwa zana ya usafirishaji zaidi kuliko kutumiwa kama zana ya uzalishaji shambani ambapo idadi ya matrekta 79 yaliyopo wilayani humo kwa sehemu kubwa yanatumiwa kwaajili ya kusafirisha mizigo na kubebea mazao baada ya kuvuna, huku wamiliki wakillalamikia kukosa watu wa kukodisha hasa wananchi wa kawaida.
“ili uwe na uhakika na kurejesha mkopo wa trekta, ni lazima kwanza uwe na eneo la kutosha kwaaajili ya kujilimia mwenyewe na kuzalisha mahindi mwenyewe kwani ukitegemea kukodishwa kwa wananchi hawa wa kawaida itakula kwako” anaeleza mmoja wa wamiliki wa zana hizo bwana Mwazembe.
Aidha ufuatiliaji mdogo miongoni mwa makampuni yanayosambaza mbegu za mahindi umetajwa kuchangia kupunguza mwitikio wa wananchi katika kutumia mbegu za kisasa . Inaelezwa kuwa huduma za ugani kwa makampuni hayo na hasa ushauri umekuwa ukisitishwa mara tu wanapofanikiwa kutangaza mbegu  wanazozizalisha na kutoweka.
Hatua hiyo inapoteza dhana ya mwendelezo kwa mkulima hasa pale anapokumbana na changamoto mpya kutokana na matumizi ya mbegu husika, hivyo kupendekeza kuwepo kwa mfumo wa uratibu wa makampuni yanayosambaza mbegu kwa wakulima  kama njia ya kuyafanya yawajibike kwa bidhaa yanazozisambaza hii ikiwa ni pamoja na dawa  za kuulia wadudu na uhifadhi  wa nafaka.
Changamoto zingine zilizobainishwa kwenye utafiti huo ni pamoja  na ongezeko la malalamiko ya usambazaji wa bidhaa feki msimu hadi msimu ambapo mbegu za mahindi, Mbolea na dawa za kuulia wadudu vimekuwa  vikiwaingiza hasara wananchi kutokana na usimamizi mbovu wa soko la bidhaa hizo katika mikoa iliyopo mipakani.
Baadhi ya mbinu ambazo zimebainishwa na wananchi kwa upande wa mbegu za mahindi ni pamoja na wafanyabiashara kuchanganya mahindi yaliyohifadhiwa kwenye magunia na kuyaweka rangi zinazofanana na mbegu zinazopendwa na wakulima na hatimaye kuchapisha mifuko katika nchi jirani ambayo hutumia kusambaza mbegu hizo zikiwa na sura halisi ya mbegu zinazozalishwa na makampuni ya ndani
Kwa upande wa Mbolea imedaiwa kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakichanganya na chokaa, chumvi na majivu ili kupata mifuko mitatu ya mbolea kutoka katika mfuko mmoja halali, wakati ambapo kwa upande wa dawa za kuulia wadudu, majivu, unga wa mahindi na rangi vimekuwa vikitumika kuwahadaa wakulima.

sehemu ya matokeo ya utafiti huo yamo kwenye taarifa ya utafiti "adoption of improved maize technologies among farmers in Ivwanga and Mbimba Villages in Mbozi District.