Adverts

Aug 14, 2012

PICHA KUTOKA BUNGENI JIONI YA LEO

Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt. Fenela Mkangara(kulia) akijadili jambo na Naibu waziri wa Ujenzi Eng. Gerson (katikati) wabunge wa viti maalum Maulida Komu (kushoto) nje ya ukumbi wa bunge ambako mkutano wa nane unaendelea.

Mbunge wa Ilala Mussa Zungu Azzan (kulia) akiongea jambo na Mbunge wa Kigoma Kaskanzini Zitto Kabwe (kushoto) katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma wakati wakiingia ndani ya ukumbi wa bunge kwa ajili yakuhudhuria mkutano wa nane, kikao cha arobaini na saba kinachoendelea mjini humo.

Msemaji Mkuu kambi ya upinzani wizara ya Maliasili na Utalii Mchingaji Peter Msingwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi watatu wa wizara hiyo badala ya kuwachukulia hatua wwatumishi wote waliohusika kwenye sakata la usafirishaji wa wanyama pori kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar. Kulia ni Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akifuatiwa na Mbunge wa Musoma mjini Vicent Nyerere.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa wosia kwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2012 bungeni leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti , kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.

Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti na Waziri Mkuu, kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo