Adverts

Aug 5, 2012

WAZEE WATAKA KIPAUMBELE KWENYE HAMASA YA SENSA

Mratibu wa sensa wilaya ya Mbozi Eliud Mwakibombaki akizungumza kwenye uzinduzi huo

Baashi ya watu waliohudhulia uzinduzi huo

Mzee Mdalavuma akifuatiwa na Mkuu wa wilaya wakiwa meza kuu

Dr Michael Kadeghe Mkuu wa wilaya ya Mbozi akiwahamasisha wananchi kushiriki kwenye zoezi la sensa

Kikundi cha Ngoma cha Ndili miongoni mwa vikundi vilivyoshiriki kwenye zoezi la uzinduzi wa kampeni ya hamasa  ya sensa jioni ya leo uwanja wa kituo cha mabasi cha Mlowo


Na Danny Tweve  

BAADHI YA WAZEE WILAYANI MBOZI WAMEPENDEKEZA KUSHIRIKISHWA WAKATI WA UHAMASISHAJI WA ZOEZI LA  SENSA KUTOKANA NA UKWELI KWAMBA BADO KUNA IMANI  NA MILA POTOFU KWA JAMII WILAYANI HUMO , HASA  INAPOFIKIA HATUA YA KUHESABU WATOTO KUWA NI UCHURO KWA KAYA ZAO.

AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI KWAAJILI YA HAMASA YA SENSA WILAYANI HUMO, MWENYEKITI WA CCM WILAYA MBOZI MZEE ALOYCE MDALAVUMA, AMESEMA NJIA PEKEE NI KWA WAZEE MAARUFU KUTUMIKA HASA MAENEO YA VIJIJINI KATIKA KUTOA UFAFANUZI JUU YA UMUHIMU WA ZOEZI HILO ILI KUPATA MWITIKIO MKUBWA NA KUWEZESHA MAFANIKO YA JUU YA ZOEZI LA SENSA

AMESEMA KWA JAMII YA WANYIHA KUHESABU WATOTO KATIKA HALI YA KAWAIDA HAIKUBALIKI, LAKINI KWAKUWA ZOEZI LA SENSA LINAFAHAMIKA VYEMA UMUHIMU WAKE NI VYEMA WANANCHI NA HASA WAZEE WAKAHAMASISHWA KUSHIRIKI VYEMA KWENYE UHESABUJI  ILI KUWEZESHA UPATIKANAJI WA TAKWIMU SAHIHI

KWA UPANDE WAKE MZEE BENNY MWANG’AMBA AMESEMA KUNA HAJA KWA VIONGOZI WA DINI WILAYANI HUMO KUTUMIA VITABU VITAKATIFU IKIWEMO BIBLIA AMBAPO KUNA ENEO INAZUNGUMZIA MAJIRA AMBAYO YESU ALIZALIWA ULIKUWA WAKATI WA SENSA YA WATU NA KWAMBA NJIA HIZO ZITAWEZESHA WATU KUFUNGUKA NA KUACHA USIRI KWENYE TAARIFA ZA FAMILIA ZAO

MAPEMA KATIKA TAARIFA YAKE MRATIBU WA SENSA WILAYA YA MBOZI BWANA ELIUD MWAKIBOMBAKI AMESEMA WILAYA YA MBOZI IMETEUA JUMLA YA MAKARANI 1471 WATAKAOSIMAMIA MAENEO YA UHESABUJI 230 AMBAPO MIONGONI MWAKE MAKARANI  460 WATAJIELEKEZA KATIKA DODOSO REFU

AMESEMA KATIKA MAANDALIZI YA ZOEZI HILO MAFUNZO YA WAHESABUJI YANATARAJIWA KUANZA JULAI TISA KATIKA VITUO VINNE VYA VWAWA, IGAMBA, ITAKA NA MAHENJE AMBAPO WAKUFUNZI WAMESHATENGWA KWA MAENEO HAYO ILI KUFANYA MAANDALIZI YATAKAYOFANIKISHA ZOEZI HILO
AKIZINDUA ZOEZI HILO KWA KUPIGA KING’ORA MKUU WA WILAYA YA MBOZI DR MICHAEL KADEGHE AMESEMA , PAMOJA NA KUANZISHA MASHINDANO YATAKAYOBEBA UJUMBE WA SENSA KUANZIA NGAZI YA KIJIJI PIA WILAYA IMEJIPANGA KUHAKIKISHA KUWA ZOEZI HILO LINAFANIKIWA NA HASA MAENEO YA VIJIJINI

DK KADEGE AMESEMA KATIKA KUFANIKISHA ZOEZI HILO WILAYA IMESHATUMA TIMU YA UHAMASISHAJI AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE TIMU HIYO INAPOKEA CHANGAMOTO NA MAPENDEKEZO YA KUFANIKISHA ZOEZI HILO KUTOKA KWA VIONGOZI WANGAZI ZA JUU NA WALE WA JAMII ILI HATIMAYE WAKATI WA UTEKELEZAJI ZOEZI HILO LIWEZE KUWA LA MAFANIKIO