Adverts

Jan 18, 2013

KANDORO AKATAA SOKOMATOLA KUNYANG'ANYWA VIWANJA


MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAHESHIMIWA MADIWANI HIVI KARIBUNI
MKUU WA WILAYA MBEYA NORMAN SIGALLA AKIWA NA MKURUGENZI WA JIJI LA MBEYA IDDI WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA
WAHESHIMIWA MADIWANI
HIZI NDIZO NYUMBA ZA SOKOMATOLA JIJINI MBEYA HUU NI MTAA WA KANISA
HUU NI MTAA WA NONDE

HALMASHAURI ya jiji la Mbeya imeshauriwa kumaliza mgogoro kati yake na wakazi wa eneo la Sokomatola kwa kuruhusu wakazi hao kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa wao wenyewe ili waweze kukubaliana na kuuziana nyumba.
Kwa muda mrefu halmashauri imekuwa ikilumbana na wakazi wa eneo hilo ambapo ilitaka kuwahamisha na kisha ichukue ilichukue na kugawa viwanja upya kwa watu walio na uwezo wa kujenga maghorofa lengo likiwa ni kupendezesha mji. Hali hiyo inatokana na nyumba nyingi zilizopo katika eneo la Sokomatola kuwa za kizamani na zilizochakaa hali isiyoendana na madhari ya kisasa yaliyopo kwenye kituo cha mikutano cha Mkapa cha halmashauri ya jiji la Mbeya kilichopo maeneo hayo. Lakini Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameshauri halmashauri kuwaruhusu wamiliki wa nyumba katika eneo hilo kufanya maamuzi wao wenyewe kwa kukubaliana na watu walio na uwezo wa kujenga magorofa na si kuwaingilia. “Tumeona mahala kwingi wafanyabiashara au wawekezaji wakubwa wanawafuata watu walio na viwanja na kufanya mazungumzo nao na wanakubaliana vizuri.Wengine wanawajengea nyumba mbali kisha wanawaachia viwanja ama wanakubaliana ikijengwa ghorofa huyu amiliki vyumba kadhaa na mwenzake vinavyobaki”. “Halmashauri isiingilie makazi ya watu.Mnadumaza eneo la Sokomatola.Na mnatudanganya kusema ninyi mtalinunua kasha muuze viwanja upya pesa hamna mtazitoa wapi.” Kandoro pia alishauri halmashauri kufanya mazungumzo na kituo cha utafiti wa kilimo cha Uyole jijini hapa ili ili iweze kupewa eneo la mbele lililo pembezoni mwa barabara ili litumike kwa ujenzi wa makazi badala ya kilimo kama linavyotumika hivi sasa. Alisema ili kuwa na mji wenye mwonekano mzuri ni vema halmashauri ikajipanga na kuhakikisha hakuna vichaka katikati ya mji badala yake iwezeshe wakazi kupata viwanja kwenye maeneo yaliyo wazi na kujenga
MBEYA YETU