Adverts

Jan 14, 2013

Ugonjwa wa presha (blood pressure)


UGONJWA WA PRESHA (BLOOD PRESSURE)
kutoka jamii forums
Presha ya kawaida isiwe zaidi ya 140/90mmlHg.

Presha ikiwa haitibiwi huharibu mishipa ya damu katika macho, misuli ya moyo kuwa minene , kusababisha mshutuko wa moyo (heart attack), mshipa ya damu safi kuwa migumu, figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure) na kiharusi (stroke).

Presha kwa mwanamke mjamzito inaweza kusababisha kifafa cha mimba na kufanya hata kiumbe kufa tumboni. Hivyo ni muhimu kuchunguza presha ya wanawake wote wajawazito.Visababishi vya presha kuwa juu
 • Chumvi nyingi
 • Unene uliozidi
 • Umri mkubwa au uzee
 • Figo ikiwa haifanyi kazi
 • Historia ya ugonjwa wapresha kwenye familia
 • Ugonjwa wa kisukari
Dalili ya mtu mwenye ugonjwa wa presha

Mara nyingi presha haina dalili hadi ilete madhara na hivyo huitwa( silent killer ) muuaji wa kimyakimya • kichwa kuuma
 • kizunguzungu
 • kubanwa na pumzi
 • kutokuona vizuri
 • kichevuchevu


Vitu vinavyo changia hali presha kuwa mbaya zaidi ni • Kula chuvi nyingi
 • Unene uliozidi
 • Kutofanya mazoezi mara kwa mara
 • Kunywa pombe nyingi
 • Uvutaji wa sigara
Tiba ya ugonjwa wa presha 1. Mojawapo ya tiba ya presha ni kuacha vyakula vyenye chumvi kabisa kama itatumika iweke kidogo ya ladha wakati chukula kipo jikoni.
 2. Pia mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ni muhimu kwa tiba ya ugonjwa wa presha. Jitahidi kutenga mda wa mazoezi angalau dakika 30-60 mara tatu kwa wiki.
 3. Epuka vyakula vyenye mafuta na lehemu maana vinaganda kwenye mishipa ya damu na kusababisha presha.
 4. Daktari atakapo baini kuwa presha yako ipo juu, kulingana na aina na kiwango cha presha atakushauri kuhusiana na vyakula na jinsi ya kubadili mwenendo wa maisha au atakuanzishia dawa mara moja. Ni muhimu uelewe kuwa utakao anzishiwa dawa hutakiwi kuziacha maisha yako yote vinginevyo hali ya presha itarudi kama mwanzo.