Adverts

Feb 28, 2013

BREACKING NEWS!!!!!!!!!!!!!!!!!!BASI LA TAQWA LAUA DEREVA, KONDA NA ABIRIA NCHINI ZAMBIA


Basi la Taqwa lililokuwa  safarini nchini Zambia limegongana na roli na kuua watu watatu papo hapo.

kulingana na radio One ya nchini Zambia ajali hiyo imetokea eneo la wilaya ya Shiwang'andu katika jimbo la Muchinga leo jioni  na kuhusisha basi lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa linatokea Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambapo limegongana na roli pia mali ya nchini Tanzania 

katika ajali hiyo watu watatu wamefariki akiwemo dereva wa basi OSWARD DAISON MWAWAPA na Konda wake Mapinduzi Gilbert Siwale na abiria mmoja ambaye hajatambuliwa na maiti zao zimehifadhiwa hospitali ya Chansali nchini Zambia.

Abiria wengine watano waliokuwa kwenye basi la Taqwa ambao ni majeruhi wamelazwa kwenye hospitali ya   wilaya ya Chinsali nchini humo.
Mkuu wa polisi jimbo la Munchinga Kamishna wa polisi Remmy Kajoba na Katibu msaidizi wa jimbo la Munchinga Jewis Chabi wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwa njia ya simu.
Roli lilohusika kwenye ajali hilo lina namba za usajiri T302 BBR lenye tela lake lenye namba T453 AHP lililokuwa likitokea Lusaka ambapo ajali imetokea majira ya saa 10.30 (ya zambia) sawa na 11.30 ya Tanzania, katika kijiji cha Chikumba  kilometa 29 kutoka makao makuu ya wilaya ya SHIWANG'ANDU 
Kulingana na taarifa hizo dereva wa roli alikuwa akijaribu kulipitia roli na kuligonga trela la roli na hivyo kubingilika upande wa kushoto
Bus hilo lilikuwa na shehena ya mizigo kutoka Kongo na kulikuwa na abiria 11 tu wakati roli hilo likitokea Lusaka lilikuwa halina mzigo
Naibu Katibu wa jimbo huyo amewataka ndugu na jamaa kutoka nchini Tanzania kwenda kutambua maiti moja ambayo haijatambuliwa na pia ndugu wa marehemu waliotambuliwa ili kuchukua maiti zao
aidha mwanamke mmoja majeruhi bado hali yake ni mbaya na imeelezwa kuwa ni mtanzania pia ambaye jina lake halijapatikana wakti majeruhi wanne hali zao zinaendelea vyema
mwisho

Kanye and Kim put their home up for sale?


About a month ago, it was reported that parents-to-be Kim and Kanye plunked down $11
million for a 10,000-square-foot Bel Air mansion.Now it's being reported that the new Italian style home has been quietly put back on the market. That is according to The Real Estate Stalker.

Property records do indeed now reveal that in late January 2013 the
couple - or at least Miss Kardashian through the same trust connected her
former faux-Tuscan in the Bev Hills P.O.—coughed up an undisclosed
amount of moolah for the big ol' Bel Air Crest crib in question
that sits on three-quarters of an acre with scenic canyon and city views
and was last listed with a $10,750,000 price tag.
However, don't count on K.K and Kanye to gut or expand the five bedroom and 6.5 bathroom mock-Med McMansion, as was previously reported
they planned to do. In fact, don't even count on them moving into the
damn house because, according to Patty, they are already in escrow to
flip the pricey pad for about a million bucks more than the still
unknown amount they paid for the place just three weeks ago.
SOURCE: LINDA LKEJI BLOG- NIGERIA

BABA MTAKATIFU BENEDIKTI XVI AKUTANA KWA MARA YA MWISHO NA WAUMINI ST. PETER'S SQUAREUmati Mkubwa wa Waumini

Moja la jukwaa kubwa la wapiga picha wa kimataifa

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome alikuwepo kuiwakilisha Tanzania.

Wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma walikuwepo pia.

Baba Mtakatifu akiingia kwenye St. Peter's Square

Picha ya Baba Mtakatifu alipotupitia Karibu huku akitubariki

Bendera ya Tanzania


Baba Mtakatifu Benedikti XVI tarehe 27 Februari amekutana na waumini kwa mara ya mwisho kabla ya kung'atuka kwenye nafasi yake ya kuliongoza kanisa katoliki hapo kesho kwenye mida ya saa mbili za usiku.


Umati mkubwa wa watu ulijumuika nje ya kanisa la Mtakatifu Petro kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kuliongoza kanisa katoliki kwa kipindi cha miaka 8 tokea kuchaguliwa kwake.Itakumbukwa kuwa Baba Mtakatifu Benedikti XVI alichaguliwa kuliongoza kanisa katoliki baada ya kifo cha Baba Mtakatifu John Paul II. Mwenyezi mungu amuongoze Baba mtakatifu kwenye maisha yake yote nje ya uongozi wa Kanisa katoliki.


Jumuiya ya Watanzania Roma ikiongozwa na Katibu wake ilikuwepo kuiwakilisha Tanzania kwenye siku hii ya Kihistoria duniani. kwa picha zaidi mnaweza kutembelea hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.


Picha zote zimeletwa kwenu na Andrew Chole Mhella (Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma)

BABA MTAKATIFU BENEDIKTI XVI AKUTANA KWA MARA YA MWISHO NA WAUMINI ST. PETER'S SQUAREUmati Mkubwa wa Waumini

Moja la jukwaa kubwa la wapiga picha wa kimataifa

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome alikuwepo kuiwakilisha Tanzania.

Wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma walikuwepo pia.

Baba Mtakatifu akiingia kwenye St. Peter's Square

Picha ya Baba Mtakatifu alipotupitia Karibu huku akitubariki

Bendera ya Tanzania


Baba Mtakatifu Benedikti XVI tarehe 27 Februari amekutana na waumini kwa mara ya mwisho kabla ya kung'atuka kwenye nafasi yake ya kuliongoza kanisa katoliki hapo kesho kwenye mida ya saa mbili za usiku.


Umati mkubwa wa watu ulijumuika nje ya kanisa la Mtakatifu Petro kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kuliongoza kanisa katoliki kwa kipindi cha miaka 8 tokea kuchaguliwa kwake.Itakumbukwa kuwa Baba Mtakatifu Benedikti XVI alichaguliwa kuliongoza kanisa katoliki baada ya kifo cha Baba Mtakatifu John Paul II. Mwenyezi mungu amuongoze Baba mtakatifu kwenye maisha yake yote nje ya uongozi wa Kanisa katoliki.


Jumuiya ya Watanzania Roma ikiongozwa na Katibu wake ilikuwepo kuiwakilisha Tanzania kwenye siku hii ya Kihistoria duniani. kwa picha zaidi mnaweza kutembelea hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.


Picha zote zimeletwa kwenu na Andrew Chole Mhella (Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma)

Feb 26, 2013

HATUA ZA AWALI ZA KUIANDAA JAMII KWENYE MIRADI YA MAENDELEO NI MUHIMU

 Mhhh hii kazi, mwezeshaji anaonekana kajaa mate mdomoni  kaazi kweli kweli kuwaelekeza wananchi wakuelewe, hasa pale ishu inapokuwa ni ngeni masikioni mwao, na wewe kama mtaalam unataka wailewe

VETERAN MBOZI YAIANGAMIZA TUNDUMA OLD IS GOLD! 3-2

 KIKOSI CHA MAANGAMIZI YA VETERAN MBOZI AMBACHO JANA KILIIFANYIA MAUAJI VETERAN TUNDUMA ALMAARUFU KAMA OLD IS GOLD 3-2
TIMU YA OLD IS GOLD TUNDUMA VETERAN AMBAO WALIJIKUTA WAKIONDOKA NA MANUNDU YA KUPIGWA MABAO 3-2 JANA KATIKA UWANJA WA MAGEREZA

BIASHARA YA SAMAKI MJINI VWAWA MBOZI

 WAJASILIAMALI WA MJINI VWAWA WAKIPUMZISHA NYOYO BAADA YA KUSAKA NOTI   HUKU NA KULE 
HEBU TUMWONE HUYU SAMAKI!!! NDIVYO INAVYOONEKANA MAMA HUYU AKITAMKA KATIKA PITA PITA ZA MITAA YA VWAWA WILAYANI MBOZI

Feb 25, 2013

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman amesema watuhumiwa hao wamewagawanya katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la watuhumiwa 9 wakiwemo askari hao wawili wakidaiwa kuhusika na tukio la kuwaua kikatili na kisha kuwazika dereva na utingo wake
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman akiwa na viongozi wenzake wa jeshi hilo la polisi wakati wa kuongea na waandishi wa habari wa Mbeya
Siraha zilizokamatwa na na jeshi hilo la polisi ndizo zilikokuwa zinatumika na majambazi hayo 
Moja ya bastora iliyotengenezwa kienyeji kwa kutumia vipande vya bomba lakini inatumia risasi za kawaida na nihatari sana siraha hii
Hizi ni vifaa vilivyokamatwa katika matukio mbalimbali yaliotokea mkoani hapa kamanda amewaomba wananchi wa mbeya kuja kuvitambua ofisini kwakwe 
Hizi ni siraha na sare za jeshi ambazo walikuwa wanatumia majambazi hao waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji
Waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
Mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), anaetuhumiwa kuteka na kuua
Hawa ndiyo wanaotuhumiwa  kuwaua  dereva na utingo wake na kisha kwenda kuwazika porini  
Samahani kwa picha hizi zinasikitisha haya niamabaki ya miili ya tingo na dereva wake waliouwawa na watuhumiwa hapo juuJESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja  kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.

Akizungumza na waandishi habari jijini Mbeya Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman amesema watuhumiwa hao wamewagawanya katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la watuhumiwa 9 wakiwemo askari hao wawili wakidaiwa kuhusika na tukio la kuwaua kikatili na kisha kuwazika dereva na utingo wake.

kundi la pili ni la watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya dereva wa polisi lililotokea Wilayani Chunya mkoani hapa baada ya kufanyika uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha mafuta eneo la Matundasi wilayani chunya.

Akitoa ufafanuzi zaidi Kamanda Diwani amesema, katika tukio la kwanza ni lile lililotokea Februari 2 katika eneo la Mafinga,Mkoani Mbeya, ambapo watuhumiwa wa kundi la kwanza waliwateka dereva na utingo wake, Festo Kyando (45) na Jafari lililotokea na kuwaua kisha kwenda kuwazika porini.

Amesema dereva huyo alikuwa ametoka Jijini Dar es salaam kubeba mzigo wa wafanyabiashara kwa lengo la kuleta mkoani Mbeya, lakini kumbe walikuwa wakiwindwa na walipofika mkoani Iringa walitekwa na kufanyiwa mauaji hayo ya kinyama.

Kamanda Diwani amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi lilianza uchunguzi mkali na hatimaye kunasa mtandao huo wa watu 9 wakiwemo askari hao wawili wa jeshi la polisi na JWTZ,ambao uchunguzi umebaini kuwa hutoa mavazi ya majeshi hayo na silaha.

Kamanda Diwani amewataja watuhumiwa hao kuwa MT.85393 Samwel Charles  Balumwina(31) wajiriwa wa jeshi la wananchi kikosi 844 kikosi cha Itende Mbeya na G.1901PC Samwel Kigunye (27) askari wa jeshi la polisi Jijini Mbeya.

Wengine ni mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), Rajabu Mbilinyi(25), Gregory Mtega(25,Francis Sanga(30) pamoja na ndugu ambao ni wafanyabiashara maarufu katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambao ni Japhet Ng'ang'ana(24), Claud Ng'ang'ana(36), Hilally Ng'ang'ana(30)

Hata hivyo amesema walifanikiwa kukamata bidhaa hizo katika eneo la Tunduma ambako tayari zilikuwa zimekamatwa na kwamba miongoni mwa watuhumiwa ndiye aliyeuziwa mzigo huo.

Amesema mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Mbozi Mkoani hapa.

Katika tukio la pili ni lile linalohusisha vifo vya watu wawili wilayani Chunya, ambao ni dereva wa polisi na dereva wa gari la majambazi baada ya kutokea kurushiana risasi.
Amesema tukio hilo lilitokea Februari 6 baada ya watuhumiwa wanne ambao wanashikiliwa na jeshi hilo kufanya uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha matundasi wilayani humo.
Amewataja madereva hao waliouwawa katika tukio hilo kuwa ni dereva wa polisi aliyefahamika kwa jina moja la Jafari, ambapo yule wa majambazi akitajwa kwa jina la  Shabani John.
Diwani amewataja watuhumiwa wanashikiliwa kwa tukio hilo kuwa ni Manase Kibona (37).Emmanuel Mndendemi na Masai Hongole, Mashaka George, John Mahenge, Narasco Mabiki.

Kamanda huyo amezitaja mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Momba  Mkoani Mbeya.

Aidha,kamanda Diwani  amevitaja baadhi ya vielelezo vilivyokamatwa  kuwa ni Bunduki aina ya Shot Gun moja ambayo namba zake zilifutika, Gobore moja ambalo pia namba zake zilifutika, Bastora tatu zilizotengenezwa kienyeji zisizo na namba na zinazotumia risasi za s/Gun.

Vingine ni Risasi 31 za Silaha ya SMG/SAR, Sare za Jeshi (JWTZ), suruali 4, mashati 4 kofia 3 na Viatu jozi mbili , Risasi 99 za S/GUN, Risasi 25 za Bastola na magari yenye namba T 464BLX TOYOTA COROLA,T381 BDR VITZ, T 251 AKU Toyota Pick Up ,T 193 BDY  Toyota Premio na T 214 ASV  Toyot Mark II.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi anawashukuru wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliojitokeza katika ktoa ushirikiano wa kuwasaka majambazi hayo ambapo pia anaendelea kutoa wito kwa watu wenye taarifa za watu ambao haeajakamatwa.
Ameongeza kuwa taratibu za upelelezi zimekamilika ambapo taratibu za kuwafikisha mahamakamani zinaendelea.
   KWA HISANI YA MBEYA YETU BLOG 

Basketmouth acquires custom made Insignia car; 1st person in Africa to own it


One of the biggest comedians to come out of Africa, Bright Okpocha, popularly known as Basketmouth has just taken delivery of the 2013 Opel Insignia car. I heard from a close source to the comedian that it's a bespoke car, meaning that everything was built to Basketmouth's specification. The car is actually not sold at any showroom in the world...you can only order it. And Basketmouth's car I hear, is the only one that has been ordered in Africa. That means no one else has this car in Africa. The car sells for about 42 thousand pounds. Now that's big! Wow! Congrats Basket!!!

SOKONI KATELELO YA VWAWA MBOZI

 AKINA MAMA WAKIELEKEA SOKONI KUUZA BIDHAA MBALIMBALI, SIKU KAMA HII MAHITAJI YA NYUMBANI HUWA BEI CHEEE, HASA NUMBU! UNAZIJUA NUMBU WEWE?
 MBOGA MBOGA SIO MPAKA MUAMBIWE NA DAKTARI  MLE


 MAFURUSHI YA MATUNDA OVERCADOES AMA MAPARACHIHI YAKISAFIRISHWA KWENDA TUNDUMA NA HATIMAYE ZAMBIA NA KONGO AMBAKO MOJA HUUZWA 1000 HADI 1500 WAKATI HAPA YANAUZWA FUNGU SHILINGI 200
HII BIDHAA INAITWA VIMBAMA! ACHA BWANA, WATU TUMEKULIA KWENYE BIDHAA HIZI UKIWA NA SHILINGI KUMI WEWE NI TAJIRI SIKU HIYO WATAKUHESHIMU!

MAGEREZA HOI MBELE YA AFYA, YALALA 3-2

TIMU YA MAGEREZA MBOZI AMBAYO JUZI ILIAMBULIA KICHAPO CHA MABAO 3-2 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI KATI YAKE NA AFYA (HOSPITALI YA MBOZI)
 MOJA YA MAJARIBIO YA TIMU YA AFYA  KUINGIA KWENYE 18 ZA TIMU YA MAGEREZA
 CHIEF AKIWA HANA HAMU BAADA YA KUKUBALI KICHAPO KWA TIMU YAKE
HIKI NDICHO KIKOSI CHA MAANGAMIZI CHA HOSPITALI YA WILAYA MBOZI KILICHOWALOPOA MAGEREZA BAO 3-2 KATIKA UWANJA WAO WA NYUMBANI

Na Mwandishi wetu

Timu ya Magereza Mbozi jana imeonja joto ya jiwe baada ya kubamizwa mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki na Hospitali ya wilaya Mbozi
Katika mchezo huo uliovuta mashabiki  ulifanyika katika uwanja wa magereza Mbozi ambapo hadi mapumziko Hospitali ya wilaya Mbozi ilikuwa mbele kwa bao 2-0
Kipindi cha pili kilianza kwa kufanya mabadiliko kadhaa kwa timu ya Magereza ambapo hatua hiyo iliwezesha kuleta uhai kwa timu hiyo na kujipatia bao la kwanza dakika ya 64.
Dakika chache baadaye timu ya Hospitali ilijipatia bao la 3 na hivyo kuonekana kuwamaliza kabisa nguvu maafande wa magereza. Hata hivyo zikiwa zimebakia dakika chache, magereza walipata bao la pili na hivyo kuufanya mchezo kumalizika kwa Hospitali kutoka uwanjani wakiwa wamenenepa kwa ushindiw  bao 3-2.

HALI YA MBOZI ASUBUHI HII

 HAPA NDIYO POSTA, ENEO LA MAKUTANO YA BARABARA MUHIMU KWENDA MAENEO MBALIMBALI YA UTAWALA NA HUDUMA ZA JAMII
BARABARA YA KUELEKEA OFISI YA MKUU WA WILAYA NA KUUNGANISHWA BARABARA KUU YA ZAMBIA -DAR ES SALAAM