Adverts

Feb 14, 2013

MAHAKAMA KUU YAENDELEA KUTOA DOZI, YAMHUKUMU MIAKA 10 KWA KUUA BILA KUKUSUDIA


 WAKILI SHAMBWE SHITAMBALA AKIZUNGUMZA NA MTEJA WAKE KABLA YA KUANZA KWA KIKAO CHA MAHAKAMA KUU, KINACHOENDELEA KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA YA MBOZI
 
 
 

MAHAKAMA KUU KANDA YA MBEYA IMEMHUKUMU MKAZI WA ITAKA WILAYANI MBOZI JUMAPILI SILWIMBA KWENDA JELA MIAKA 10 KWA KOSA LA KUMUA BILA KUKUSUDIA  MWANAKIJIJI MWENZAKE MAWAZO EDSON MWAMPULE.

AKITOA HUKUMU HIYO JAJI MFAWIDHI NOEL PETER CHOCHA AMESEMA, ADHABU HIZO ZITUMIKE KAMA UBAO WA MAFUNZO KWA WANANCHI WA WILAYA ZA MBOZI NA MOMBA KUTOKANA NA KUKITHIRI KWA VITENDO VYA MAUAJI KAMA VILE HAKUNA UTAWALA WA SHERIA

AKISOMA MAELEZO YA SHTAKA BAADA YA KUREKEBISHWA KUTOKA MAUAJI YA KUKUSUDIA, WAKILI WA SERIKALI CATHERINE PAUL AMEKIAMBIA KIKAO CHA MAHAKA KUU KINACHOENDELEA KWENYE UKUMBI WA MAHAKAMA YA WILAYA MBOZI KUWA MNAMO JANUARY 16 MWAKA 2009, MSHTAKIWA ALIMUUA  MAWAZO  EDSON MWAMPULE KWA KUMCHOMA KISU KIFUANI HIVYO KUSHTAKIWA  CHINI YA  KIFUNGU CHA  195 CHA KANUNI YA ADHABU

WAKILI HUYO ALIENDELEA KUFAFANUA KUWA KATIKA KUTENDA KOSA HILO, PAMOJA NA UGOMVI WAO KUAMLIWA NA MMILIKI WA KLABU YA POMBE ZA KIENYEJI BARAKA LAITONI, WALITULIA KIDOGO NA KUJIVUTA PEMBENI AMBAKO UGOMVI ULIANZA TENA NA  HUKO NDIKO ZILIKOSIKIKA SAUTI ZA MTU KUCHOMWA KISU

UPANDE WA MASHTAKA ULIWASILISHA MAELEZO HAYO PAMOJA NA VIELELEZO VIWILI VIKIWEMO  TAARIFA YA DAKTARI WA HOSPITALI YA MBOZI MISION YA UCHUNGUZI WA MWILI WA MAREHEMU NA RAMANI YA ENEO TUKIO  LA MAUAJI LILIPOTOKEA

AWALI WAKILI  SAMBWE SHITAMBALA ALIYEKUWA ANAMTETEA MSHTAKIWA, ALIMWOMBA JAJI KUMBADILISHIA SHITAKA MTEJA WAKE KUTOKA KOSA LA AWALI LA KUUA KWA KUKUSUDIA  AMBALO  MSHTAKIWA ALILIKANA NA AKAWA TAYARI   KUKIRI KOSA DOGO LA MAUAJI  BILA KUKUSUDIA   AMBAPO WAKILI WA SERIKALI CATHERINE PAUL HAKUWA NA PINGAMIZI NALO NA HIVYO SHAURI HILO LIKABADILISHWA

KUFUATIA KUKUBALIWA KWA MABADILIKO HAYO MSHATAKIWA ALISOMEWA SHTAKA LA MAUAJI BILA KUKUSUDIA, JAJI ALIMHOJI MSHATAKIWA KAMA ANAKUBALIANA NA MAELEZO YA WAKILI WA SERIKALI YA KUUA BILA KUKUSUDIA AMBAPO ALIYAKUBALI.

BAADA YA KUKIRI KOSA, JAJI ALIMTIA HATIANI NA HIVYO KUMTAKA WAKILI WAKE KUTOA UTETEZI KAMA ANAO HATUA AMBAYO ILIFANYWA NA WAKILI SHITAMBALA AMBAYE ALITAJA HOJA TANO ZA KUMWOMBA JAJI AMPUNGUZIE ADHABU ZIKIWEMO ZA KIPINDI ALICHOKAA MSHTAKIWA MAHABUSU.

WAKILI SHITAMBALA ALIIELEZA MAHAKAMA KUWA MAREHEMU PIA ALITENGENEZA MWENYEWE MAZINGIRA YA KIFO CHAKE KUTOKANA NA KUJIWEKA KWENYE MAZINGIRA YA ULEVI NA UGOMVI HIVYO YAWEZEKANA PIA KUWA ISINGEKUWA KIFO YAWEZEKANA MAREHEMU MAWAZO ANGEKUWA KIZIMBANI LEO HII  WAKATI AMBAPO MSHTAKIWA ANGEKUWA MAREHEMU!

NAYE MSHTAKIWA BAADA YA KUPEWA NAFASI NA JAJI AKITAKA KUJUA KAMA KUNA LA NYONGEZA KWAKE, ALIMWELEZA “ MH JAJI NINA AFYA YA MGOGORO HIVI HAPA NINA DAWA MFUKONI”

HIVYO ALIIOMBA MAHAKAMA IMFIKIRIE  KUMPUNGUZIA ADHABU KWAKUWA ANAENDELEA KUTUMIA DAWA NA AFYA YAKE SI NZURI

JAJI KATIKA HUKUMU YAKE AMESISITIZA KUWA VISINGIZIO VYA ULEVI KATIKA KUTIMIZA DHAMIRA MBAYA DHIDI YA BINADAMU MWINGINE HAVIKUBALIKI KATIKA JAMII NA KWAMBA MAHAKAMA NDIYO UWANJA PEKEE WA MAFUNZO KWA KUTOA ADHABU ITAKAYOMFANYA MTU KUJUTIA KOSA ALILOLITENDA NA PIA KUWA DARASA KWA WENGINE WENYE NIA KAMA HIZO

“NAKUHUKUMU UENDE JELA MIAKA 10 ILI IWE WEWE UBAO WA MAFUNZO KWA WENGINE KWASABABU VITENDO KAMA ULIVYOVIFANYA WEWE NI VYA KIWANGO CHA KUPINDUKIA AMBAVYO VINAHITAJI ADHABU KALI” ALIHITITIMISHA JAJI CHOCHA.