Adverts

Feb 19, 2013

MBOZI YAKABIDHI MAABARA ZINAZOHAMISHIKA NNE KWA SHULE ZA SEKONDARI

 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI LEVISON CHILLEWA AKIMKABIDHI DIWANI WA MSIA MH MAKUNGANYA MOJA YA MEZA ZILIZOTOLEWA KUFUATIA MSAADA WASERIKALI WA KIASI CHA SHILINGI MILION 24 KWA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KWAAJILI YA KUBORESHA MAABARA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI 
 MMOJA WA WATAALAMU WA MAABARA AKIONYESHA NAMNA ZANA HIZO ZINAVYOFANYA KAZI KABLA YA KUKABIDHIWA KWA WAKUU WA SHULE ZA KATA WALIOONGOZANA NA MADIWANI WAO

 MIONGONI MWA SHULE ZA KATA ZENYE UHITAJI WA VIFAA NA MAABARA AMBAPO KWA MIAKA TAKRIBANI SITA WATOTO WAMEKUWA WAKISOMA BILA KUFANYA MAZOEZI YA VITENDO 
 AFISA ELIMU SEKONDARI WILAYA YA MBOZI BWANA ISAACK MGAYA AKIPEWA MKONO WA SHUKRANI NA BAADHI YA WALIMU NA DIWANI WA KATA YA RUANDA BAADA YA SHULE YA LUMBILA KUPEWA MEZA YA MAABARA INAYPOTEMBEA
 MIONGONI  MWA ZANA ZITAKAZOGAWIWA MASHULENI KWAAJILI YA KUIMARISHA MAFUNZO KWA VITENDO
OFISA KATIKA IDARA YA ELIMU SEKONDARI AKIONYESHA NAMNA YA KUUNGANISHA  MFUMO WA MAJI KWENYE MEZA YA MAABARA

Na Danny Tweve wa Indaba blog.

HALMASHAURI ya wilaya Mbozi imekabidhi meza nne za maabara inayotembea kwaajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa ni sehemu ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari katika masomo ya sayansi.

Afisa Elimu sekondari wilayani Mbozi bwana Isaack Mgaya, amesema meza hizo zenye thamani ya shilingi Milion 24 zinatokana na msaada uliotolewa na serikali mwezi juni wa kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kuziwezesha shule za sekondari kuwa na Maabara zinazohamishika.

Amesema hatua hiyo inaziwezesha shule Mbili za sekondari kwa wilaya mpya ya Momba za Mkulwe na Nkangamo kuwa na maabara wakati kwa upande wa wilaya ya Mbozi shule za sekondari za Msia na Lumbila pia zimenufaika.

Bwana Mgaya amesema Mobile Laboratory kama zinavyofahamika zimebuniwa ili kuwezesha kukidhi mafunzo ya masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari na Vyuo.

Aidha alifafanua kuwa matumizi yake yanawezesha madarasa hayo kuhama hama kulingana na mahitaji na kwamba pia zinaweza kutumika chini ya miti, ama maeneo yasiyo na mifumo ya umeme ama maji hivyo kurahisisha uelewa wa wanafunzi kulingana na mazingira waliyopo

kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Mbozi bwana Levison Chilewa ambaye aliambatana na Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Momba Bwana Juma Kitabuge ameeleza kuwa kutokana na muundo wa maabara hizo, madiwani wa kata zilizonufaika na mpango huo wanapaswa kujenga hoja za kushawishi madiwani wenzao ili kutenga kiwango kikubwa cha fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hizo mbili kwaajili ya ununuzi wa meza hizo ambazo zitakuwa mkombozi kwa watoto katika masomo ya sayansi.

Alisema hivi sasa wanafunzi wamekuwa waoga wa masomo hayo kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi kunawawezesha wanafunzi sasa kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo.

Alisema ni vyema pia kwa shule zilizo karibu kuona namna ambavyo zinaweza kushirikiana kutumia maabara moja kwa kutembeleana hatua ambayo itarahisisha katika ufundishaji na hata kuleta tija katika matumizi ya maktaba hizo badala ya kuazimisha meza hizo kutoka shule moja kwenda shule nyingine hali ambayo inaweza kusababisha uharibifu.

Akizungumzia msaada huo, diwani wa kata ya Ruanda bwana Keneth Mgala amesema, kimsingi hatua hiyo itasaidia kupunguza hali ya matokeo mabaya kwenye masomo ya sayansi ambapo wanafunzi wakti mwingine wanalaumiwa kwa kuonewa kutokana na mazingira yenyewe ya shule kukosa vitu muhimu kama maabara hivyo kushindwa kuhamisha nadharia katika vitendo ama kuoanisha vyote viwili.

Kwa kipindi kirefu,Shule pekee yenye maabara ya kubuniwa na utundu wa mwalimu mmoja wilaya ya Mbozi ipo katika shule ya sekondari ya Vwawa ambapo maaabara hiyo imekuwa  shule kadhaa zimekuwa zikitembelea na  kujifunza ubunifu huo kwa lengo la kwenda kutengeneza katika shule zingine ili kuongeza hamasa ya  wanafunzi kupenda masomo ya sayansi
mwisho