Adverts

Mar 25, 2013

KIBAKA AUWAWA MBOZI JIONI HII, NI BAADA YA KUVAMIA KWA MUASIA

Huyu ndiye kibaka mzoefu kulingana na hukumu ya wananchi waliyoitekeleza katika eneo la Uhindini mjini Vwawa katika wilaya ya Mbozi ambako yeye akiwa na wenzake wawili wanatuhumiwa kuvamia na kupora kwenye nyumba ya mwananchi mwenye asili ya kiasia  na kuiba fedha na mali nyingine wakati mvua inanyesha mchana wa leo
 Marehemu ametambuliwa kwa jina la Joseph John Mapunda mkazi wa eneo la Ilolo katika mji wa Vwawa

 Picha zote na Mdau Chimika

Na Danny Tweve Mbozi
Mtu anayedhaniwa kuwa kibaka mkazi wa eneo la Ilolo Joseph John Mapunda ameuawawa na wananchi wenye jazba wakati akitekeleza uhalifu kwa kuvunja na kuiba katika moja ya nyumba zilizopangishwa na mtanzania mwenye asili ya asia katika eneo la sokoni mjini VWAWA wilayani Mbozi

Tukio hilo limetokea majira ya saa 9 alasiri  wakati mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika maeneo mengi ya wilaya ya Mbozi, kuonyesha kuathiri shughuli nyingi za mjini hapo kutokana na kuambatana na upepo mkali.
Fulsa hiyo ilikuwa mwafaka kwa vijana hao kufanya matukio ya uhalifu katika eneo la Nyumba ya jengo la SACCOS ya walimu mjini Vwawa na kujikuta mmoja akitumbukia kwenye mikono ya wananchi.

Kifo cha kijana huyo kimekuwa somo mbele ya jamii ambapo mkuu wa wilaya ya Mbozi akizungumza mara baada ya kuopolewa kwa mwili wake majira ya saa 12.40 kutoka kwenye kichaka kikubwa ambacho ni chanzo cha maji, kimezua gumzo kwa jinsi kijana huyo alivyofahamika kwa matukio ya hapa na pale toka enzi za utoto wake.