Adverts

Mar 9, 2013

USIKU WA MWANAMKE MBOZI, VITU VYA ASILI VYAVUTIA WATU


Mama huyu mjasiliamali kutoka Tunduma akionyesha ubunfu wake katika utengezaji wa keki kwa kutumia ndizi na mchanganyiko wa vyakula vya asili 
Huu mlo mate yananitoka kambale bwana watamu!!!
Ugali uliotengenezwa kwa makopa( unga wa Mhogo) ambao kwa kabila la wadigo huula kwa kambale
Mama huyu wa jamii ya Wanyiha akionyesha chakula cha wanyiha ambacho ni ugali wa ulezi, Mboga ni nyanya chungu na kufunikiwa na majani ya migomba kwenye vyungu ambavyo amesema vinahifadhi pia uwezo wa akina baba kwenye yale mambo yetu! Tofauti na masufuria ambayo yanapopata moto ati yanaacha kemikali ambazo zinawaacha hoi akina baba

Mama wa kichaga akionyesha namna mtori unavyoandaliwa, kweli ulikuwa usiku wa mwanamke
Mzuka ukampanda mama huyu kutoka Tunduma na akaanza kuyarudi magoma, tena nakumbuka kitu kilipigwa cha pepe kalle kabasele yampanye! aaah mama aliosha nyoyo za watu saaana tu
akaja Sara Miondoko Mwashambwaa mbona aliwaacha watu midomo wazi kwa kuonyesha vazi la Wanyiha!
Kambale bwana kwa ugali wa