Adverts

Apr 30, 2013

KATIBU MKUU IKULU ASIFU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TASAF NA MKURABITA MBOZI

 Katibu mkuu ofisi ya rais  Ikulu Bw.Peter Ilomo(aliyekaa mwenye shati jeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya Mbozi baada ya kufanya ukaguzi wa miradi chini ya TASAF na ile ya MKURABITA
 akionyeshwa ramani ya makazi ya eneo la karoleni mjini Tunduma ambako makazi yanatarajiwa kuhaulishwa ili kuruhusu ujenzi wa miundombinu kama barabara na mifumo ya maji taka huku wengine wakiwekewa utaratibu mzuri ikiwa ni pamojana kupatiwa hati Miongoni mwa miradi chini ya Tasaf ambapo bweni la shule ya sekondari ya Isandula limekamilika na kufungwa umeme wa jua kuwawezesha watoto wa kike kusomea katika mazingira salama
 Wanafunzi wakiimba wimbo wa Tanzania nakupenda kwa moyo wote! wakati katibu mkuu ofisi ya rais alipotembelea mradi wa bweni la shule yao
 Mratibu wa TASAF MBOZI Bw. Hamis Mtoni mwenye tshirt ya njano akitoa ufafanuzi kwenye mradi wa ujenzi wa daraja linalounganisha eneo la Matengu na Old Vwawa  lililojengwa na kaya zenye uhaba wa chakula kupitia TASAF awamu ya pili
 Hapa akitembelea mradi wa mashine ya kukoboa mpunga ya watoto yatima katika mji wa Vwawa
akizungumza na watendaji katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi, kushoto kwake ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Levison Chilewa