Adverts

Apr 2, 2013

MWANAMKE ABAMBWA AKIMUUZA MTOTO WA KUMZAA KWA SHILINGI 100,000/=



Mwanamke mmoja mkazi wa kitongoji cha Seif katika kijiji cha Chiwezi-Mpemba TABU MWASHITETE  anashikiriwa na polisi wilayani Momba kwa tuhuma za kuumuuza mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka mitano kwa shilingi 100,000/=
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12 jioni baada ya majadiliano ya biashara hiyo yaliyodumu kwa saa 7 baina ya muuzaji na mnunuzi.
Akizungumzia mchezo ulivyokuwa mpaka kumkamata mtuhumiwa, Bwana John Sinyinza ambaye alishakuwa mtumishi wa umma na kustaafu anaeleza kuwa alifuatwa na Bi Tabu majira ya saa tano asubuhi  nyumbani kwake.
Anaeleza kuwa katika mazungumzo  na mama huyo alishitushwa alipoambiwa kuwa anamuuza mtoto ambaye amemtoa Malawi na kwamba lengo la kumuuza anataka kupata fedha kwaajili ya kugharimia kumtoa baba yake mzazi wa mtoto huyo ambaye amefungwa nchini Malawi.
Hata hivyo katika majadiliano ya biashara hiyo, mwanamke huyo alitaka kulipwa kiasi cha shilingi 1,000,000/=(Milioni Moja) ambapo walikubaliana kuwa wangeuziana majira ya saa 12 jioni baada ya kupatikana kwa fedha hizo.
Ndipo bwana Sinyinza kutokana na tukio hilo kutokuwa la kawaida aliwasiliana na vyombo vya usalama na kupewa askari wa kike wa upelelezi ili waongozane eneo la tukio ambapo katika mtego wa kufanyika biashara hiyo, mwanamke huyo alifika akiwa na mwanaye ambaye alikuwa uchi ili wakabidhiane.
Bwana Sinyenga katika kuhakikisha kuwa mwanamke huyo hashtukii mchezo alimtambulisha askari huyo kama binti yake na kwamba walikubaliana kulipata fedha hizo kwa awamu ambapo angemlipa shilingi 100,000/= kwanza na kesho yake angemaliziwa kiasi cha shilingi 900,000/= zilizobakia.
Kufuatia makubaliano hayo mwanamke huyo alimkabidhi mtoto wake kwa mnunuzi na baadaye  kuagana kwa makubaliano kuwa angepewa kiasi kilichobakia na binti huyo wa upelelezi kesho yake.
Baada ya mteja  kutoweka na “bidhaa ya mtoto” ndipo  askari wa upelelezi huyo alipomweka chini ya ulinzi bi mkubwa huyo  na baadaye kufikishwa kituo ch polisi  cha Tunduma ambako katika mahojiano imebainika kuwa mtoto huyo ni  mwanaye ambaye baba yake alishafariki.
Alisema kuwa kutokana na ugumu wa maisha aliamua kumuuza mtoto wake huyo ili apate fedha kwaajili ya shughuli za kiuchumi kama mtaji na kwamba anatambua kuwa wanunuzi wangeweza kumuua mtoto huyo ama kwa matumizi mengine!
Kulingana na fununu za jeshi la polisi mwanamke huyo atafikishwa mahakamani kesho jumatano katika mahakama ya wilaya ya Mbozi