Adverts

Jun 30, 2013

KIMONDO SUPER SPORT CLUB YAINGIA DARAJA LA KWANZA KWA KUIGAGADUA POLISI JAMII BAO 3-1


PICHA ZOTE NA CAPTIONS KWA HISANI YA MWANAFASIHI(MAHIRI WA SIMULIZI BLOG).


WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKIPEANA MIKONO NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII, KABLA YA KUANZA KWA MECHI YA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KATIKA UWANJA WA SOKOINE LEO JIONI


TIMU YA POLISI JAMII YA BUNDA-MARA


TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI-MBEYA


GOLIKIPA WA TIMU YA POLISI JAMII  EMANUEL DAUD AKISHANGAA GOLI LILILOFUNGWA NA MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO CHARLES HIZA DK YA 12


GOLI LILIPITILIZA NA KUPENYA KWENYE NYAVU NA KUSABABISHA REFARII NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA MBEYA KUREKEBISHA NYAVU HIZO KWA DAKIKA KADHAA KABLA YA MPIRA HAUJAWEKWA KATI












Add caption








GOLI LA TATU KWA UPANDE WA KIMONDO BAADA YA MPIRA WA PENALT GOLI LILIFUNGWA NA MCHEZAJI LUKA MPOSHI DK 59


WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKISHANGILIA GOLI








KIPUTE KINAENDELEA UWANJANI




PATASHIKA KATIKA GOLI LA POLISI JAMII




NDEREMO NA HOI HOI ZILITAWALA BAADA YA KIPYENGA CHA MWAMUZI KUPILIZWA HUKU KIMONDO FC IKIWA MBELA KWA MABAO 3-1


POLISI WALILAZIMIKA KUMTOA NJE YA UWANJA REFARII KUTOKANA NA KUZONGWA NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHEZO




HOI HOI ZA FURAHA ZINAENDELEA


MASHABIKI WAKIWA WAMEMNYANYUA JUU MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK AMBAKISYE BAADA YA TIMU HIYO KUJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU TANZANIA BARA








SHANGWE NA HOI HOI ZINAENDELEA KATIKA DIMBA LA KUMBUKUMBU YA SOKOINE MKOANI MBEYA






KOCHA WA TIMU YA POLIS JAMII MADENGE OMAR AKILALAMIKIA UTARATIBU WA UENDESHAJI WA LIGI HIYO


PONGEZI ZINAENDELEA


'TUMESHINDA TUNAMSHUKURU MUNGU TUMEPITIA VIGINNGI NA VIKWAZO VINGI'' AKIONEKANA ANASEMA MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK MINGA






SHABIKI WA TIMU YA KIMONDO MBEGU MOJA AKIWAZAWADIA WACHEZAJI WA TIMU HIYO SH. 200,000 BAADA YA USHINDI






Na DannyTweve

Timu ya Kimondo super sports club ya Mbozi mkoani Mbeya imeungana na ... kuingia daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kumaliza mchezo wake jana kwa kuifunga timu ya Polisi jamii ya Bunda mkoani mara mabao 3 -1.

Katika mchezo mzuri na wakasi uliofanyika uwanja wa sokoine jijini Mbeya ulishuhudia Polisi Jamii wakicheza kufa na kupona licha ya maelezo ya kocha wao kuwa walishtukizwa mchezo huo kwani TFFA awali walitangaza kuwa ungechezwa siku ya jumapili.

Bao la kwanza la Kimondo liliwekwa wavuni mnamo dakika ya 12 kupitia kwa Charles Hiza baada ya kupokea pasi kutoka kwa Geofrey Mlau na kumchungulia mlindamlango wa Polisi Jamii Emmanuel Daud na hatimaye kumchambua na kuhesabu bao la kwanza

Mashambulizi ya hapa na pale yaliendelea kwa timu zote ambapo mnamo dakika ya  17 Cosmas Mwazembe wa Kimondo SSC aliunganisha wavuni kwa kichwa krosi ya Charles Hiza na kuifanya Kimondo kuongeza hamasa kwa mabao 2 ya haraka haraka waliyoyapata.

Hata hivyo sherehe hiyo ilidumu kwa dakika 30 tu kwani Polisi jamii kupitia kwa Joseph Onyango waliweza kuihada ngome ya Kimondo na kuachia shuti kali lililodakwa na kutemwa kwenye nyavu na kipa wa Kimondo Daud Pius ha hivyo kuwafanya Polisi Jamii kutoka kipindi cha kwanza wakiwa na matumaini ya kurejesha bao la jingine katika kipindi cha pili.

Bao la tatu kwa Kimondo lilifungwa mnamo dakika ya 59  kwa njia ya penati kupitia kwa Lucas Baraka baada ya mshambuliaji Geofrey Mlau kuangushwa eneo la hatari katika purukushani za kumdhibiti akiwa njiani kwenda langoni mwao.

Mnamo dakika ya 57 mwalimu wa Polisi jamii Bunda  Madenge Omary alitolewa eneo la benchi la ufundi baada ya kumtukana  mwamuzi wa mchezo huo Daudi Ahadi kutoka jijini Dar es Salaam  na akizungumza baada ya mchezo huo, alisema wachezaji wake wamechezeshwa wakiwa wamechoka kutokana na kuwasili asubuhi jijini Mbeya na kulazimishwa kucheza wakati TFF ilikuwa imetangaza mchezo huo kuchezwa siku ya jumapili na si jumamosi.

Akizungumzia kupanda daraja kwa timu yao Mkurugenzi wa Timu ya Kimondo Erick  Minga ndoto za wilaya ya Mbozi kuwa mkoa zinakwenda sambamba na ukuzaji wa soka wilayani humo ambapo watahakikisha timu yao inapanda daraja na kuingia ligi kuu msimu ujao na kuwataka wananchi wa mkoa wa mbeya kwa ujumla kushiriki katika kuchangia mafanikio ya timu zao.

Alisema tayari sasa mkoa utakuwa na michezo mfululizo katika uwanja wake wa sokoine kwa kuwa kuna timu mbili za ligi kuu, pia Kimondo itavuta michezo ya daraja la kwanza hatua ambayo wananchi watafadi uhondo wa soka mkoani mwao kwa mwaka  mzima.



Jun 27, 2013

MBOZI YAENDELEA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA MAJI SAFI NA SALAMA


Na Angela Kivavala- Mbozi   

Asilimia 44   wakazi wa wilaya ya Mbozi ndiyo wanaopata huduma ya maaji safi na salama imefahamika

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Mbozi Levison Chillewa amesema kwa sasa wilaya inategemea aina tatu za vyanzo vya maji vikiwemo  visima, mitiririko na maji ya chemichemi zilizo boreshwa.

Akifafanua  Chillewa amesema  kuna  jumla ya  visima virefu na vifupi 105 chemichemi za asili 40 mitiririko 5 na matanki 6 yanayotumika kuvuna  maji ya mvua.

Chillewa amesema kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSR),wilaya inatekeleza  miradi ya ujenzi  wa  miundombinu  ya maji katika wilaya ya mbozi ambapo hadi sasa visma vitano vinajengwa ikiwa ni vyanzo vya usambazaji wa maji katika vijiji vitano vya wilaya ya mbozi

Aidha Kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, halmashauri ya wilaya ya Mbozi   imewezesha baadhi ya shule za sekondari na  hususani miradi ya ujenzi wa hosteli pamoja na baadhi ya huduma kama zahanati na nyumba za walimu kuwa na  mfumo wa uvunaji wa maji ya mvua  kwa kuwekewa  tanki za plastiki (SIMTANK) zenye ujazo wa kati ya lita 5000 hadi lita 10,000.

Kuhusiana na uhifadhi wa mazingira, Mkurugenzi huyo amesema wilaya ya mbozi vyanzo vya 23 tayari vimepimwa na vipo kwenye hatua za kuwekewa alama za kudumu.

 aidha halmashauri ya wilaya imeanzisha mfumo wa  kuifadhi takwimu  za vyanzo vya maji ambapo hadi mwezi mei jumla ya vyanzo vya maji 471 vilikuwa vimetambuliwa pia vyanzo vya maji vimepewa kipaumbele na kamati za maendeleo za vijiji na kata.

Pamoja na mafanikio wilaya imekuwa ikikumbanana changamoto mbalimbali ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya maji unaotokana na kulima kujenga kuchoma moto na kuchunga mifugo kwenye vyanzo vya maji na gharama kubwa za uchimbaji na ujenziwa miundombinu ya maji.

Wilaya imeweza kuwekamikkati ya kuzikabili changamoto hizo ikiwa nipamoja na  kuelimisha jamii kuusu umuhimu wa tuunzaji wa vyanzo vya maji kulinda na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchiikiwa ni pamoja na upandaji wa miti  katika vyanzo vya maji, vijiji vyote vyawilaya vimepewa jukumula kudhibiti uharibifu katika vyanzo vya maji

Kwa mwaka 2013/ 2014 halmashauri imetengewa TSH 1,425,470,049 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya maji wilaya ya mbozi

Mwisho

 

Jun 23, 2013

KIMONDO YA MBOZI YAZIDI KUPETA LIGI YA MABINGWA RAUNDI YA PILI, YATOA SARE UGENINI MUSOMA

Timu ya Kimondo ya wilayani Mbozi imeendeleza wimbi la kujitengenezea mazingira mazuri kuingia ligi daraja la kwanza  Tanzania bara baada ya kuilazimisha sare ya bao 2-2 Timu ya Polisi Jamii ya Musoma katika uwanja wake wa Nyumbabi wa Karume mjini Msoma
Polisi jamii ambao walianza kupata bao lao la kwanza walijikuta wakishindwa kubana na badala yake wakaachia mnamo dakika ya 36 baada ya Kimondo kupanga mashambulizi huku wakiwasiliana kwa kutumia kiwemba, kindali na kinyiha huku wakiwaaacha maafande wakishangaa hadi Geofrey Mlau akiandika bao la kwanza na lakusawazisha.
Nyumbani ni nyumbani ilidhihirika baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa nguvu sawa kwa kufungana bao moja kwa moja, kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya kasi kutoka polisi jamii ambao waliweza kupata bao la pili mnamo dakika ya 67 lakini halikudumu muda mrefu kwani mnamo dakika ya 75 hali ilikuwa mbaya kwa wenyeji
Alikuwa Imani Wilson aliyewainua mashabiki wa Musoma bila kujali uzalendo kwa timu yao na kuamua kushangilia timu ya wageni Kimondo SC baada ya kutungua shuti la kufa mtu lililomfanya mlindamlango wa Polisi Jamii kujifanya kama vile alikuwa akisikiliza simu kwa jinsi lilivyoingia na kumchanganya kabisaa.
Ikiongozwa na mlezi wao ERICK MINGA Kimondo iliendelea kufanya mashambulizi yenye lengo la kuwadharirisha wenyeji kwenye uwanja wao wa nyumbani hata hivyo mashambulizi hayo yaliiishia kwa kosa kosa, hadi timu inatoka uwanjani wananchi wa Musoma walishindwa kuvunga na badala yake wakajikuta wakitoa mikono ya pongezi kwa mtanange mtamu ulioonyeshwa na Kimondo Sc.
Katika kudhihirisha nia ya kupata mkoa mpya wa Songwe, Wilaya ya Mbozi kupitia wadau wake imeendelea kusukuma mbele ajenda ya michezo ambapo miongoni mwa wadau FULL DOSE ambaye amejitokeza mbele kuidhamini timu hiyo anaeleza kuwa tutaingia mkoa mpya tukiwa na timu mpya ya ligi kuu!!
 
 
Add caption