Adverts

Jul 9, 2013

MBOZI YAOMBA KUONGEZA KATA NA VIJIJI VIPYA



Na Angela Kivavala DSJ

Halmashauri ya Wilaya ya mbozi  iko katika mchakato wa kuomba kuongeza kata na vijiji vipya ili kusogeza huduma karibu na wanainchi.

Kata zipatazo sita (6) zinategemewa kuanzishwa  na vijiji 24 baada ya mapendekezo hayo kuwasilishwa ofisi ya Waziri mkuu Tamisemi

Wilaya ya Mbozi ina watu 446,339,Asilimia 88% ya Wakazi wake hujishughulisha na kilimo ambacho huchangia asilimia 80% ya pato la Wilaya.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki katika Maadhimisho ya Siku ya Serikali za Mitaa ambayo hufanyika Julai mosikila mwaka.
Lengo la sherehe hizo ni kutoa mwanya kwa jamii kutambua na kuzifahamu shughuli na huduma mbali mbali zinatolewa na Taasisi za Serikali za Mitaa yaani  halmashauri za Majiji, Manispaa na  wilaya.

ujumbe wa mwaka huu ni “Amani, Uadilifu na Uwajibikaji kwa wote ni Nyenzo muhimu katika mchakato wa Katiba mpya na Ustawi wa Serikali za Mitaa”
Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi inaendelea kusimamia utekelezaji wa mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tuko kwenye mchakato wa kupitia Rasimu ya Katiba iliyotolewa kwa kutumia mabaraza ya Kata yaliyochaguliwa yalisomwa katika hotuba kwa wananchi wa mbozi.

Katika kipindi cha mwaka moja uliopita Halmashauri iliajilia wa tumishi wapya 410 kati yao walimu wa sekondari ni 210 na washule za msingi nio 182 na watumishi wa afya ni 10 ambapo kwa kiasi kikubwa ufanisi wa kazi umeongezeka katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa mbozi

Wilaya ina jumlayashule za sekondari 40za selikari ambapo kati ya shule hizo ni shule 1 tu yenye kidato cha tano na sita Halmashauri ya wilaya ya mbozi iko kwenye mchakato wa kuanzisha shule za kidato cha tano na sita katika kata tofauti.