Adverts

Oct 31, 2013

AFIA MAHAKAMANI AKISUBIRI KUMWEKEA DHAMANA MWANAYE TUKUYU


MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Tiger Mwaigomole (70) Mkazi wa kata ya Masukulu wilayani Rungwe amefariki dunia ghafla akiwa katika chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Rungwe akifuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mtoto wake wakati Mahakama ikiendelea.

Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni majira ya saa 9 alasiri ndani ya Mahakama hiyo ambapo Marehemu alifika mahakamani hapo akiwa na mwanaye aliyejulikana kwa jina la Lusajo Tiger (40) wakiwa na lengo la kumwekea dhamana ndugu yao Gwakisa Tiger ambaye alifikishwa mahakamani hapo akituhumiwa kwa kosa la kupigana na kujeruhi katika ugomvi uliotokea kijijini kwao.

Kwa mujibu wa mtoto wa Marehemu aliyekuwa ameongozana nae Mahakamani hapo Lusajo Tiger alisema wakati kesi ikiendelea chini ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Kingwele, ndugu yao alipandishwa kizimbani kusomewa mashtaka yanayomkabili ndipo marehemu alipoanza kutetemeka kwa madai kuwa anajisikia baridi kali sana.

Alisema kutokana na marehemu kulalamikia baridi aliamua kumnunulia chai ya moto ili anywe na kupunguza baridi ambapo baada ya kufanya hivyo marehemu alikata roho muda mfupi baada ya kumaliza kunywa chai aliyokuwa amepelekewa huku akiwa amekaa ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

Kutokana na tukio hilo Askari polisi waliokuwepo mahakamani hapo waliuchukua mwili wa marehemu na kuukimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana kwa ajili ya vipimo lakini hata hivyo mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi ingawa ripoti ya kifo chake haikutolewa mapema.

Wakati huo huo Hukumu ya kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe, John Mwankenja inayowakabili Hakimu Mwakalinga na wenzie watatu huenda ikatolewa Novemba 11 mwaka huu baada ya Mahakama kuu kanda ya Mbeya chini ya Jaji Samwel Karua kumaliza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi kwa upande wa watuhumiwa.

Kwa mujibu wa Jaji Karua alisema baada ya kumaliza kusikiliza pande zote mbili atatumia muda wa siku mbili kwa ajili ya kuandika hukumu ambayo itaitoa Novemba 11, Mwaka huu, kesi ambayo inasimamiwa na Mwanasheria wa Serikali Archiles Mulisa huku watuhumiwa wakitetewa na Mawakili wawili wa kujitegemea ambao ni Simon Mwakolo na Victor Mkumbe.
HABARI NA PICHA NA MBEYA YETU BLOG

TANGAZO LA WAUGUZI KULIPA LESENI ZAO



SHULE YA HOLYWOOD YAAGIZWA KUWASOMESHA KWA MWAKA MZIMA BURE WANAFUNZI 69


Na Mwandishi wa Indabaafrica
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Mh Mlugo ameagiza uongozi wa shule ya sekondari ya Holly Wood ya wilayani Mbozi kuwasomesha wanafunzi 69 wa kidato cha pili waliozuiwa na uongozi wa shule hiyo  kufanya mitihani ya kuingia kidato cha tatu
Katika uamuzi huo alioutoa juzi, Baraza la Madiwani Mbozi limeelezwa kuwa sambamba na hilo, uongozi wa shule hiyo pia umepewa kalipio kwa maamuzi yake kinyume na maelekezo ya wizara hiyo.

 MKUU WA WILAYA MBOZI DR MICHAEL KADEGHE AKITOA UFAFANUZI KWENYE BARAZA HILO LEO
 BAADHI YA MADIWANI NA WATAALAMU WAKIFUATILIA KIKAO HICHO, WA KWANZA MBELE NI MH SAMWEL MTAWA ALIYEIBUKA NA SWALI LA PAPO KWA PAPO KUHUSIANA NA WANAFUNZI WA HOLLYWOOD WALIOZUIWA KUFANYA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI
 MADIWANI WAKIWA WANAFUATILIA MICHANGO UKUMBINI
 MWENYEKITI WA HALMASHAURI KATIKATI NA KOFIA AKIWA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA CCM KUSHOTO KWAKE NA KULIA KWAKE NI KAIMU MKURUGENZI  NA MKUU WA WILAYA ALIYESIMAMA
 MWENYEKITI WA HALMASHAURI MH ERICK  AMBAKISYE MINGA NA KAIMU MKURUGENZI DR CHARLES MKOMBACHEPA

Katika maswali ya papo kwa papo kwenye baraza la madiwani , Diwani wa kata ya Isandula Samwel Mtawa  alimuuliza mwenyekiti wa halmashauri hatua zilizochukuliwa kuwasaidia watoto 69 waliozuiwa kufanya mitihani ya kidato cha pili kutokana na kasoro za kutofikia wastani uliowekwa na shule hiyo kwenye mitihani ya MOCK na majaribio.
Akijibu swali hilo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alisema, Mheshimiwa waziri amepokea malalamiko hayo na kuwasiliana na kamishna wa elimu ambapo ilishindikana kufanywa upya mitihani hiyo kwa mwaka huu, na ikaelekezwa mitihani hiyo kufanywa mwakani.
Naye mkuu wa wilaya ya Mbozi Dr Michael Kadeghe alitoa ufafanuzi wa suala hilo alisema kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ilipokea taarifa za uongozi wa shule hiyo kuwazuia wanafunzi 70 kufanya mitihani ya kidato cha Pili nailifikiwa maamuzi kwa shule hiyo kuzuiwa kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2013/2014
Akitoa maelezo ya adhabu iliyotolewa na waziri Mlugo, mkuu huyo wa wilaya alisema waziri aliagiza uongozi wa shule hiyo kuwaghalimia wanafunzi hayo ada ya mwaka mmoja pamoja na mahitaji mengine ya shuleni hadi watakapofanya mtihani wao wa kuingia kidato cha tatu mwakani.
Aidha imeelezwa kuwa uongozi wa shule hiyo pia uliagizwa kughalimia ada za wanafunzi hao watakaoamua kuhamia shule nyingine kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kujali gharama za shule hizo wanazokwenda.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amekemea tabia iliyozuka kwa shule za sekondari binafsi kuweka utaratibu wa kuchuja wanafunzi kutokana na ufaulu wa mitihani ya ndani kwa lengo la kufanya mashindano ili zionekane shule hizo ni bora kitaifa.

Alisema wakuu wa shule hizo wanapaswa kuonyesha uwezo wao kwa kuwafundisha wanafunzi hadi kufaulu na siyo kuchuja wale wanaoshindwa kwenye mitihani ya majaribio na baadaye kuwafukuza kwenye shule zao.

DC MBOZI AKIRI USHIRIKINA KUILEMEA MBOZI, AOMBA MADIWANI WAKAKEMEE



Baraza la Madiwani la Wilaya ya Mbozi  limeombwa kushiriki katika kukemea matukio ya mauaji yaliyoanza kuibuka ambapo kwa mwezi  September peke yake kumekuwa na matukio  matano.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani la wilaya hiyo Mkuu wa wilaya Mbozi Dr Michael Kadeghe amesema hali hiyo inakwamisha jitihada za kuvutia kwenye fulsa mbalimbali zilizopo kwa kujenga hofu kwa wageni

Amesema pamoja na matukio ya mauaji, pia matukio ya ushirikina katka kipindi hicho hicho yameripotiwa matukio saba

Akifafanua alisema katika kijiji cha Itaka mmoja wa watuhumiwa wa ushirikina alipohijiwa kama anajihusisha na mambo hayo alikiri kuyafanya kwa kutumia “majini”

Inaelezwa na  mkuu huyo wa wilaya kuwa katika kujaribu kupata uhakika wa anachokifanya bwana huyo, alimtaka washindane naye ambapo jamaa alianza kupandisha maruhani yake ili amfanyie uchawi Dc  hali ambayo bwana Kadeghe alilazimika kumzima kwa kumzuia asiendelee

Huku madiwani wakicheka kwenye kikao hicho, Dc alisema kama huyu jamaa alikuwa tayari kufanya ushirikina mbele ya kamati ya ulinzi na usalama unadhani wananchi wa kawaida huko chini hali inakuwaje?

Alisema katika hatua nyingine kumekuwepo matukio ya mara kwa mara ya wanavijiji kuwafukuza watu wanaotuhumiwa kufanya ushrikina vijijini na kwamba katika matukio ya hivi karibuni walimwokoa mwanamke mmoja aliyekuwa aliyetuhumiwa katika kata ya Nambinzo.

Alisema kasi ya wanavijiji kuwahamisha watuhumiwa wa vitendo vya kishirikina wilayani humo vinaashiria kuwa matukio ya imani hizo yamewachosha na yanaweza kusababisha kutoweka kwa amani kwenye jamii.


Alisema yeye hana uwezo wa kuhamisha watu kwenye vijiji na mamlaka hayo anayo mheshimiwa rais pekee hivyo kumekuwa na ugumu kufanya maamuzi ya namna hiyo licha ya viashiria vya ushirikina katika jamii kuoneka.

TUMETOKA MBALI NA BADO TUPO MBALI

Jamani toka enzi hizo bado tunachoshwa na mikoba na kamera mpaka leo! hapa nikiwa nafanya mahojiano na Bwana Njowoka kiongozi wa chama cha soka Mkoa wa Njombe 

PROFESA MHONGO AKWEPA KUZUNGUMZIA SUALA LA KUVUJA MAFUTA KWENYE VISIMA VYA MAJI MLOWO

na Mwandishi wa Indaba Africa
Waziri wa nishati na Madini Mh Profesa Sospeter Mhongo jana ameruka viunzi sakata  la kuvuja kwa mafuta ya diesel kwenye visima vya maji katika mji wa Mlowo na kudai kuwa halihusiani na wizara yake
Akizungumza jana  wakati akijibu swali la mmoja wa Madiwani aliyetaka kujua serikali inafanya nini wakati wananchi wa Mlowo wakiwa afya zao zikiwa hatarini kutokana na kuchota mafuta badala ya maji kwenye visima vya mji huo.
Suala hilo liliwasilishwa na diwani wa Myovizi Mh Cosmas Nzowa ambaye alihoji kama waziri anayeshughulikia masuala ya nishati ambapo mafuta ya diseli ni sehemu ya mamlaka ya waziri huyo ambapo waziri alikuwa akimkatiza katiza wakati diwani huyo akiuliza
“masuala ya mafuta ya diseli ninahusikaje mimi? Waulize NEMC hilo ni suala lao “ alisikika waziri Mlongo kabla ya diwani huyo kufafanua
Diwani huyo alisisitiza suala la Mafuta ni sehemu ya wizara ya Mlongo labda kama imebadilika na ndipo Mlongo aliporuhusu aendelee kuuliza swali lake, “ haya endelea bwana”  uliza tu
Hata hivyo pamoja na swali hilo kuulizwa  kwa lengo la kutaka majibu yam h waziri, inaonekana waziri alilikwepa katika kutoa  majibu pale ambapo alizungumzia zaidi masuala ya Umeme  na jitihada zinazofanyika mkoani Mbeya na pia kwa wilaya ya mbozi  lakini kwenye mafuta ya Mlowo alikauka!
Kwa ujumla wakazi wa mji wa Mlowo wamekuwa wakilalamikia hali mbaya ya maji ya visima vyao kunakotokana na mwingiliano wa mafuta ya diseli yanayohofiwa kuvuja kutoka kwenye bomba la Mafuta la TAZAMA ama kutoka kwenye moja ya visima vya mafuta vilivyopo kwenye vituo vya Mlowo.
Diwani wa Myovizi Cosmas Nzowa akisalimiana na Mh Profesa Mhongo alipofanya ziara yake katika wilaya ya Mbozi kwa lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na  Wakala wa Umeme vijiji  REA jana 
Katika majumuisho yake kwenye kikao chake kilichofanyika ukumbi wa mkuu wa wilaya Mbozi, Waziri Mlongo alielekeza   wananchi kuwa  na nia njema ya kugawa maendeleo sawia katika meneo yote ya nchi badala ya kuwa na uroho wa kila fulsa kuwa kwenye maeneo yao.
Hali hiyo ilitokana  na kila diwani aliyesimama kwenye kikao hicho kuvutia umeme kwenye maeneo yake kuwa haujapitia, na ndipo alipomwinua mbunge wa  Mpanda –Katavi Saidi Kessy na kumuuliza, hivi wewe Kessy kule kwako umepewa kiasi gani na REA?
Mh Kessy alijibu Bilion 10. Mheshimiwa  waziri na Mkoa wa RUkwa umepewa Bilion 30!
Ndipo alipodakia hapo waziri na kueleza” Nyinyi Mbozi kama wilaya mmepewa Bilion 22.57 wakati wenzenu Rukwa kama mkoa wamepewa Bilion 30 hamuoni kuwa mmepata kiasi kikubwa sana? Sasa tukielekeza kila kitu kwenye wilaya yenu jamani tuwe na ulinganifu.


Oct 30, 2013

PROFESA SOSPETER MHONGO AWAPIGA DONGO MADIWANI, MSIPENDE SAFARI MNO!!


 PROFESA MHONGO ALIPOWASILI MBOZI AKISALIMIANA NA MKUU WA WILAYA YA MBOZI DR MICHAEL KADEGHE, NYUMA YAKE NI MBUNGE WA KATAVI MHE. SAID KESSYNA MWENYE SHATI LA KIJANI NI MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI ERICK MINGA
 BAADHI YA WATENDAJI WA WILAYA YA MBOZI PAMOJA NA UJUMBE WA TANESCO WAKIFUATILIA KIKAO HICHO



 KAIMU MKURUGENZI MBOZI DR CHARLES MKOMBACHEPA na MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA MH CHARLES MINGA AMBAKISYE
Mh Profesa Mhongo akizungumzia hali ya huduma za umeme na nafasi za halmashuri  za wilaya katika kuchangia miradi ya UMEME nchini
 BAADHI YA WAKUU WA IDARA NA VITENGO HALMASHAURI YA WILAYA NA SERIKALI KUU WILAYANI MBOZI WAKIFUATILIA MAJADILIANO
 PROFESA MHONGO AKIZUNGUMZA NA WATAALAM HAO PAMOJA NA MADIWANI
AKISALIMIANA NA BAADHI YAWATENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOZI

NA DANNY TWEVE INDABAAFRICA MBOZI 

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo amewataka madiwani nchini kuachana na mitazamo ya kizamani kuwa kila suala linalohusiana na maendeleo ni lazima lielekezwe kwenye serikali kuu wakati wao wanakalia rasrimali zinazoweza kutatua kero hizo.

Akizungumza baada ya kupokea maswali mbalimbali kutoka kwa madiwani wa wilihohudhulia katika mapokezi yake wilayani Mbozi, Mhongo amesema ni vyema sasa halmashauri zikaanza kutenga fedha kwaajili ya kufadhiri miradi ya umeme kama inavyofanyika kwenye miradi mingine

Alisema hali hiyo itasaidia kusukuma mbele jitihada za kujiletea maendeleo na hasa kwa kuzingatia kuwa REA pia imejielekeza katika utekelezaji wa miradi ya umeme wa jua kwaajili ya maeneo maalum kama shule.

Profesa Mhongo alisema ni vyema Madiwani kuachana na ziara na safari zisizo na tija kwa halmashauri zao na kuendelea kutumia vibaya rasrimali za taifa wakati mahitaji ya wananchi ni makubwa kwenye masuala yanayohusiana na maendeleo hususani Umeme na huduma zingine

Alitolea mfano miradi ya umeme wa jua kwenye shule za sekondari zenye madarasa 8 mitambo yake inaghalimu kiasi cha shilingi millioni nne ambazo halmashauri za wilaya zinaweza kutenga kwenye mapato yake na kuwaita REA ili wawezeshe ufungaji wa umeme huo.

Aidha akifafanua hali ya upatikanaji wa umeme nchini Profesa Mhongo amesema kwa sasa  hali ya upatikanaji umeme vijijini ni asilimia 7 na lengo ni kufikia asilimia 20 ifikapo 2015.

Kwa upande wa upatikanaji wa umeme kwa ujumla nchini alisema asilimia 20 ya watanzania wanapata umeme na lengo ni kufikia asilimia 30 ifikapo 2015 ingawa msukumo mkubwa unaelekezwa vijijini

Akitoa takwimu za jumla Meneja Msaidizi wa ufundi wa REA bwana GISSIMA NYAMBO –HANGA alisema kwa wilaya ya Mbozi na Momba REA imetenga shilingi Bilion 22 kuwezesha  umeme  katika vijiji vya wilaya ya Mbozi
Alitaja baadhi ya maeneo yaliyopo kwenye mpango huo ni pamoja na Kamsamba, Hasamba, Hatelele, Isansa, Msanyila, Msia, Nanyala, Senjele, Mbimba, Nkanga, Oldvwawa, Itaka, Itepula, Ndalambo, Msangano, Hezya na Ivwanga

Alisema wateja wa awali 2700 wataunganishwa na mfumo huo wa umeme na kwamba hatua za kumpata mkandarasi zipo mbioni na kwamba utekelezaji wa miradi hiyo utaanza November 2013. 

MPANGO WA UTOAJI WA CHAKULA MASHULENI BADO WASUA SUA


 Mmoja wa madiwani Mh Kalonge kutoka kata ya Igamba akiwasilisha taarifa ya utendaji na uwajibikaji kwa kata yake

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mbozi Mh Allan Mgula kushoto akiwa na kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mbozi Bwana Zabron Lulandala  kwenye kikao cha jana

Na Danny Tweve wa Indaba Africa
Mpango wa utoaji chakula shuleni katika wilaya ya Mbozi , umeendelea kupanuka ingawa kwa meeneo mengi umekuwa ukifanyika kwa vipindi maalumu imebainika.
Katika kikao cha kuwasilisha taarifa za utendaji toka ngazi ya kata zilizowasilishwa na madiwani ikiwa ni utaratibu wa halmashauri kupima  uwajibikaji wa waheshimiwa madiwani, baadhi ya kata zimefanikiwa kueneza mpango huo kwenye vijiji vyote
Kulingana na taarifa hizo kuna kata zenye akiba ya chakula cha miezi 8 kwaajili ya kuhudumia wanafunzi kwenye shule za msingi na  kata zingine bado hazijatekeleza mpango huo kabisa.
Kulingana na taarifa zilizowasilishwa kuna jumla ya gunia 206 za mahindi zilizochangwa na wananchi kuwezesha utoaji wa huduma ya chakula mashuleni hasa kwenye ngazi ya elimu ya msingi, hata hivyo kulingana na idadi ya wanafunzi uwiano wa chakula  hicho kwa idadi ya wanafunzi waliopo wilayani ni sawa na  mlo wa siku mbili ambapo wastani kwa siku mtoto anakula 0.11 kg za wanga.
Wilaya ya Mbozi ina jumla ya wanafunzi 91,311 ambao kati yao 648 ni wa kutoka shule mbili binafsi za msingi na wengine 90,663 ni kutoka shule 155 za serikali.
Hali hii inaonyesha kurudi nyuma katika utoaji wa huduma ya chakula ikilinganishwa na robo ya mwaka iliyopita ambapo taarifa zilizowasilishwa zilionyesha baadhi ya kata zilikuwa zimefikia kuchangia gunia 70 za mahindi.
Kulingana na mwelekeo wa uchangiaji, ni dhahiri katika kipindi hiki cha kuelekea masika, uchangiaji utapungua badala ya kuongeza kwa kuwa kipindi cha mavuno (Julai hadi Septemba) hapakuwekwa msukumo mkubwa kwa wananchi kuchangia chakula  cha watoto mashuleni.
Kata ambazo zimeonekana kufanya vizuri katika uchangiaji huo ni pamoja na Myovizi ambayo shule zake zote saba zinatoa huduma ya chakula, Isandula ambayo shule tano kati ya nane zinatoa chakula, Isansa ambayo shule 6 kati ya 16 zinatoa chakula, Ipunga shule Mbili zinatoa chakula kati ya 5 na Mlowo shule 2.
Zingine ni Vwawa shule 2, Nyimbili shule mbili, Iyula shule 3 na Itaka shule 3. Kulingana a na takwimu hizo kuna baadhi ya kata ambazo katika robo ya kumalizia mwaka wa fedha 2012-2013 ziliweza kutoa chakula lakini sasa zimerudi nyuma zikiwemo Nanyala, Halungu, Igamba na Ruanda.

Ili kuongeza msukumo kwenye usimamizi wa suala la chakula, vikao vya  mabalaza ya madiwani  vya kivyama ambavyo huketi kabla ya baraza la madiwani la halmashauri, vinapaswa kujadili kwa upana suala hilo ili kuweka msukumo wa makusudi katika kuwezesha utekelezaji wa mpango wa uchangiaji chakula mashuleni uweze kutekelezwa.

Oct 29, 2013

VWAWA JIONI YA LEO



Wadau wa Indaba Africa wakiwa katika moja ya karakana za Mji wa Mbozi leo jioni 

 Marekebisho yakiendelea kwenye moja ya magari yanayosaidia ukuzaji wa mji wa Vwawa kupitia shughuli za Uchukuzi wa zana za ujenzi zikiwemo Tofali, Mchanga na mawe

TIMU YA WATAFITI WA NINI KIFANYIKE KUREJESHA MAHUSIANO MTWARA

Baada ya Mvutano wa Haitoki inatoka Mtwara !! timu ya asasi zisizo za kiserikali wanachama wa Tanzania Coalition for Debit and Development TCDD walipiga kambi huko kutafiti namna ambapo wananchi na serikali watarejea mahusiano ya awali na kujenga kuaminiana baina yao.


JIONI HII TUNDUMA

MICHEZO MASAA YA JIONI BAADA YA KAZI HULETA PIA MAWAZO MAPYA YA KIUTENDAJI KWAAJILI YA KUONGEZA UFANISI MAHALA PA KAZI SIKU INAYOFUATA

Tanzania Construction Industry Seminar, 28-29 November 2013, Golden Tulip Hotel, Dar Es Salaam


More Available on www.focustanzania.com

MEET THE SPECIALIST


 Oncology specialist from HCG India, Dr. Sridhar will be available for consultation in Tanzania on 30th October 2013.  The details are as below
Wednesday 30th October 2013
At: Regency Satellite Centre  (Opp to Zanzibar Hotel)  Zanaki street, Kisutu  
Time: 9.30am to 4.30pm
For Appointments please contact: 0685530916, 0786247874, 0657170233.

KUTANA NA MTAALAM 
 Mtaalam wa Saratani kutoka India HCG, Dr. Sridhar atapatikana kwa ajili ya ushauri nchini Tanzania  tarehe 30th Septemba, 2013 kwa  Maelezo ni kama hapa chini
Mahali: Regency Satellite Centre (Mkabala na Zanzibar Hotel) Mtaa wa Zanaki na kisutu, Dar es Salaam 
Muda: saa 3.30 asubuhi hadi 10.30 jioni
Kwa uteusi tafadhali wasiliana na : 0685530916, 0786247874, 0657170233.

Al Ostoora Holiday Travel & Tourist

Al Ostoora Holiday Travel & Tourist
Al Ostoora
Get Full Pacakge for Two Persons of 4 Days and 3 Nights
  • Tickets
  • VISA
  • 4 Star Hotel
  • Transport
  • Desert Safari
  • City Tours
  • Cruise
  • Big Bus
  • Food
For Only
Double $2,300
Al Ostoora
Al Ostoora Dubai
Al Ostoora Dubai
123Tanzania E-Shots

39,000+ Subscribers all over the Tanzania.
123Tanzania.com is the largest B2B online directory of Tanzania with more than 15,000 monthly visitors

Contact Us: English or Kiswahili +255 658 786 235+255 773 858 090+255 22 213 3039

123Tanzania Ltd, Elia Complex, Zanaki Street, P. O. Box 8758, Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 213 3039 | Email: info@123tanzania.com | Web: www.123tanzania.com

Copyright (c) 2013, 123Tanzania Ltd. All Rights Reserved.
.

Customer Service Seminar

Dear Sir/ Madam,
Greetings!
Tasota is pleased to announce Customer Service Seminar by the renowned Customer Service Strategist Guru  – John Tschohl from USA on Saturday, October 26th, 2013 at Hyatt ( Marquee) from 8.30am – 16.30hrs ( with lunch).  ( http://www.johntschohl.com )
The two main Objectives for this Seminar are:
1. Improve Value Added to Customers
2. Understand the constraints of corporate business in terms of Quality Service vs Paying for Service on time

Tickets will be available from September 30th, 2013.  At a minimum costs of  US$ 150 per person.  Once  you advise how many people will attend I will send you a proforma invoice so that you can process payment.
After receiving your confirmation, tickets will be available from 10th October onwards at the TASOTA Secretariat which is at IT Plaza-5th floor.


JOURNALISM TRAINNING OPPORTUNITIES


Oct 27, 2013

NABI NA MHUBIRI WA KIMATAIFA TB JOSHUA, AMETOA MAONO KUWA KUNA KIONGOZI WA AFRIKA MASHARIKI ATATEKWA


TB Joshua Jumapili 27/10/2013, ameonyeshwa rais mmoja Africa atatekwa
aidha ameonyeshwa watu wakiwa club wanacheza then wanalipukiwa na nchi iyo ni jirani na Kenya, Angalizo, amesema siyo kenya tena,

Hata hivyo hajataja nchi yeyote katika Afrika Mashariki ingawa katika ramani ya sasa inaonyesha kuwepo kwa nchi Tano zikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania

Misa ya leo katika kipindi chake cha unabii ndipo alipokuja na unabii huo ambao ni sehemu ya maono aliyooteshwa


amesema ataendelea kuomba ili jumatano na alhamisi ijayo aonyeshwe ni rais gani na nchi gani.

BREACKING NEWS.......JAMAL MALINZI AWA RAIS MPYA TFF


Taarifa zilizoufikia mtandao huu kutoka chumba cha kuhesabia kura kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa TFF ni kwamba Mgombea urais wake Jamal Malinzi ameshinda kwa kura nyingi mbele ya mgombea mwenzake Athuman Nyamlani.
Inaelezwa kuwa Malinzi amejizolea kura 73 kati ya 125 zilizopigwa huku Athumani Nyamlani akiambulia kura 52.
Mchaka mchaka huoulianza kwa Nyamlani kuanza kuongoza wakati wa kuhesabu kura ambapo kura za kwanza 36 kwa 14 za Malinzi ziliamsha shangwe kwa wafuasi wake,lakini baadaye hali ilibadilikwa kwa Malinzi kuweka "gap" kubwa hadi kura 67 kwa 41.
Hali hiyo iliendelea kuwa tamu kwa upande wa kundi la Malinzi kwa mtindo wa Tieni tieni kwa moyo mmoja" na ikiwa hadi mwisho Malinzi akaibuka kidedea huku Tenga akitamka kuwa atampa ushirikiano. Matokoe hayo yalitolewa rasmi saa 8.21 Usiku

Matokeo hayo yalitanguliwa na matokeo mengine ya chaguzi za awali ambapo ilipofika kwa makamu wa rais Walace Karia aliibuka kidedea kwa kuwafunika  Nassib Ramadhan na Iman  Madega  a.ka. Seneta

ASKARI WA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA TANZANIA AUWAWA DRC



Na Kenny Katombe na Chrispin Mvano

KINSHASA (Reuters) – Mmoja wa walinzi wa Umoja wa Mataifa kutoka nchini Tanzania  aliuawa na mwingine kujeruhiwa wakati wa siku ya tatu ya mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi katika mashariki ya Kongo siku ya Jumapili, wakati wakielekea kwenye  ngome ya waasi wa Rutshuru .

Mkuu wa  vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Kongo ( MONUSCO ) alisema mlinda amani kutoka Tanzania aliuawa wakati wa kupambana na waasi wa M23 katika mji wa Kiwanja, kaskazini ya mji mkuu wa mkoa Goma , mji mkubwa mashariki mwa Kongo.
"Askari alikufa wakati wa kulinda watu wa Kiwanja, " Martin Kobler , mkuu wa MONUSCO, alisema katika taarifa. Katika awamu ya kwanza  ya mapigano kati ya jeshi na waasi mwishoni mwa Agosti , waasai hao waliwauawa  askari wawili wa kulinda amani wa Tanzania.
Kufuatia miezi miwili ya utulivu  katika ukanda  wa mapigano, mapigano yamelipuka ghafla Ijumaa baada ya mazungumzo ya amani nchini Uganda kuvunjika baada ya  M23 kutaka viongozi wake wapewe msamaha kamili . Kila upande umekuwa ukilaumiwa na mwingine kuhusika na kuanzisha  mapigano.

Rais Joseph Kabila, ambaye wiki iliyopita alitishia kurejea kwenye  hatua za kijeshi , na kudai kuwa msamaha pekee kwa VIONGOZI wa M23  bila  masharti si haikubaliki.

ANGALIA VUNJA MBAVU YA KENYA XYZ SHOW

pic.twitter.com/3qdsGrPK0U

Oct 26, 2013

KALI ZA JAMII FORUMS LEO!


ASKOFU MSTAAFU RAYMOND MWANYIKA AFARIKI DUNIA



Askofu mstaafu wa kanisa katoliki Jimbo la Njombe, Raymond Mwanyika amefariki dunia jana mkoani Njombe.
Taarifa iliyotolewa na kanisa katoliki Njombe inaeleza kuwa Mwanyika amefariki 24 October,2013


Askofu Mwanyika alizaliwa mwaka 1930 huko kijiji cha Uwemba-Njombe,baada ya makuzi na majiundo yake ya kiroho na kimwili alipata daraja takatifu la Upadre 11/10/1959;mnamo 16/01/1971 Baba Mtakatifu Paulo VI alimteua kuwa askofu wa Njombe,na 25/04/1971 alisimikwa kuwa Askofu rasmi wa Jimbo la Njombe.

June,8 2002 Askofu Mwanyika alipumzika na nafasi yake kuchukuliwa na Askofu Maluma.

Askofu Mwanyika amekuwa Padre kwa miaka 54 na Askofu kwa miaka 42,atakumbukwa kwa majitoleo yake ktk kuwahudumia watu wa Njombe bila kujali tofauti zao za kiimani,alikuwa mstari wa mbele ktk kuendeleza huduma za jamii kama hospitali na shule,huduma za maji na umeme ktk maeneo mengi ya Njombe,Makete mpaka Ludewa.

Anatarajiwa kuzikwa 29/10/2013 ndani ya kanisa katoliki la Njombe(Njombe Cathedral)....Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina lake lihimindiwe.
hapa ni baadhi ya taarifa  muhimu juu yake kwa mujibu wa jarida pepe la  Vatican
DateAgeEventTitle
1930
BornUwemba
11 Oct 195929.8Ordained PriestPriest
16 Jan 197141.0AppointedBishop of Njombe, Tanzania
25 Apr 197141.3Ordained BishopBishop of Njombe, Tanzania
8 Jun 200272.4ResignedBishop of Njombe, Tanzania
24 Oct 201383.8DiedBishop Emeritus of Njombe, Tanzani
AMINA

Oct 24, 2013

JITIHADA ZA KUJITANGAZA NA KUVUTIA WAWEKEZAJI ZAANZA




MBOZI DISRICT COUNCIL











MBOZI DISTRICT INVESTMENT PROFILE
          

THE LAND OF COFFEE AND HOSPITALITY


Oct 23, 2013

KITIMOTO LICHA YA CHANGAMOTO ZA KITAFITI, BADO WATEJA NI WENGI


Mmoja wa watengenezaji wa kiti moto maarufu wilayani Mbozi Bwana Mwashuya akiwa mtamboni kuandaa mnyama tayari menu kamili ya siku ya leo!