Adverts

Oct 31, 2013

SHULE YA HOLYWOOD YAAGIZWA KUWASOMESHA KWA MWAKA MZIMA BURE WANAFUNZI 69


Na Mwandishi wa Indabaafrica
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Mh Mlugo ameagiza uongozi wa shule ya sekondari ya Holly Wood ya wilayani Mbozi kuwasomesha wanafunzi 69 wa kidato cha pili waliozuiwa na uongozi wa shule hiyo  kufanya mitihani ya kuingia kidato cha tatu
Katika uamuzi huo alioutoa juzi, Baraza la Madiwani Mbozi limeelezwa kuwa sambamba na hilo, uongozi wa shule hiyo pia umepewa kalipio kwa maamuzi yake kinyume na maelekezo ya wizara hiyo.

 MKUU WA WILAYA MBOZI DR MICHAEL KADEGHE AKITOA UFAFANUZI KWENYE BARAZA HILO LEO
 BAADHI YA MADIWANI NA WATAALAMU WAKIFUATILIA KIKAO HICHO, WA KWANZA MBELE NI MH SAMWEL MTAWA ALIYEIBUKA NA SWALI LA PAPO KWA PAPO KUHUSIANA NA WANAFUNZI WA HOLLYWOOD WALIOZUIWA KUFANYA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI
 MADIWANI WAKIWA WANAFUATILIA MICHANGO UKUMBINI
 MWENYEKITI WA HALMASHAURI KATIKATI NA KOFIA AKIWA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA CCM KUSHOTO KWAKE NA KULIA KWAKE NI KAIMU MKURUGENZI  NA MKUU WA WILAYA ALIYESIMAMA
 MWENYEKITI WA HALMASHAURI MH ERICK  AMBAKISYE MINGA NA KAIMU MKURUGENZI DR CHARLES MKOMBACHEPA

Katika maswali ya papo kwa papo kwenye baraza la madiwani , Diwani wa kata ya Isandula Samwel Mtawa  alimuuliza mwenyekiti wa halmashauri hatua zilizochukuliwa kuwasaidia watoto 69 waliozuiwa kufanya mitihani ya kidato cha pili kutokana na kasoro za kutofikia wastani uliowekwa na shule hiyo kwenye mitihani ya MOCK na majaribio.
Akijibu swali hilo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alisema, Mheshimiwa waziri amepokea malalamiko hayo na kuwasiliana na kamishna wa elimu ambapo ilishindikana kufanywa upya mitihani hiyo kwa mwaka huu, na ikaelekezwa mitihani hiyo kufanywa mwakani.
Naye mkuu wa wilaya ya Mbozi Dr Michael Kadeghe alitoa ufafanuzi wa suala hilo alisema kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ilipokea taarifa za uongozi wa shule hiyo kuwazuia wanafunzi 70 kufanya mitihani ya kidato cha Pili nailifikiwa maamuzi kwa shule hiyo kuzuiwa kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2013/2014
Akitoa maelezo ya adhabu iliyotolewa na waziri Mlugo, mkuu huyo wa wilaya alisema waziri aliagiza uongozi wa shule hiyo kuwaghalimia wanafunzi hayo ada ya mwaka mmoja pamoja na mahitaji mengine ya shuleni hadi watakapofanya mtihani wao wa kuingia kidato cha tatu mwakani.
Aidha imeelezwa kuwa uongozi wa shule hiyo pia uliagizwa kughalimia ada za wanafunzi hao watakaoamua kuhamia shule nyingine kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kujali gharama za shule hizo wanazokwenda.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amekemea tabia iliyozuka kwa shule za sekondari binafsi kuweka utaratibu wa kuchuja wanafunzi kutokana na ufaulu wa mitihani ya ndani kwa lengo la kufanya mashindano ili zionekane shule hizo ni bora kitaifa.

Alisema wakuu wa shule hizo wanapaswa kuonyesha uwezo wao kwa kuwafundisha wanafunzi hadi kufaulu na siyo kuchuja wale wanaoshindwa kwenye mitihani ya majaribio na baadaye kuwafukuza kwenye shule zao.