Adverts

Jan 21, 2014

SAFARI YA MWISHO YA MZEE PETER MWANG'ONDA ILIVYOKUWA LEO

 Mzee Conel  Abson Mwang'onda akibadilishana jambo na mwanaye Thom Mwang'onda kwenye msiba wa  mzee Peter Mwang'onda kaka wa Conel Abson Mwang'onda aliyefariki mwishoni mwa wiki katika hospitali ya wilaya ya Mbozi na kuzikwa leo nyumbani kwake Hanseketwa wilayani Mbozi
 Jeneza la Marehemu Peter Mwang'onda likiwa linaandaliwa kwaajili ya kuagwa nyumbani kwake
 Akina mama wakiwa wanajipanga kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu
Mc wa shughuli ya mazishi hayo bwana Charles Mwakipesile akitoa utaratibu wa ibada ya mazishi na hatimaye kumpuzisha mpendwa Peter Mwang'onda 

 Baadhi ya wastaafu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano waliungana na familia katika ibada ya mazishi
 Kutoka kushoto ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi Tanzania DCI -Mzee Mwaitenda, Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya John  Mwakipesile, RSO Mbeya Bw. Salimini, Aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Conel Abson Mwang'onda  wakifuatilia ibada ya mazishi

 Watoto wa familia ya Mwang'onda iliyopatwa na msiba wa baba yao Mzee Peter
 baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya mazishi
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbozi Bw. Mdalavuma akimpa Pole Mzee Mwang'onda kwa kufiwa na kaka yake  mzee Peter

 Mzee Mwaitenda akitoa heshima za mwisho
 Mzee Colnel Abson Mwang'onda akiwa na mkewe wakiweka shada la maua
 Watoto wa kiume wa familia ya Mwang'onda wakiweka mashada ya maua
 John Mwakipesile akiweka shada la maua
 Safari ya Mwisho ikitimia, wakati jeneza likiingizwa kaburini  huku Mzee Mwang'onda akiangalia kwa uchungu safari ya kaka yake kwenda mavumbini

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABAS KANDORO akisalimiana  na aliyemrithi nafasi hiyo Mzee John Mwakipesile wakiwa msibani hapo
 Kandoro akipeana pole na Mzee Mwang'onda  baada ya kuwasili na kushiriki mazishi
 Kwaya ikitumbuiza kwenye eneo la ibada ya mazishi
Ibada hiyo ilimalizika kwa kupata chakula cha pamoja
PICHA ZOTE KWA MSAADA WA MWAIPULA VIDEO CENTRE