Hakyanani kama mambo yenyewe ndiyo haya mtaendelea kuwalaumu watu bure, hivi akitokea chizi mmoja akitokea akanyang'anya masanduku haya inakuwaje.
indaba2010
Oct 31, 2010
MASANDUKU YA KUPIGIA KURA YABEBWA KWA BAISKELI
Masanduku ya kura yanaposafirishwa kwa baiskeli. hii ni kijiji cha Igamba yakielekea Zelezeta.
indaba2010
WAZEE HAWA WANAPOTIMIZA JUBILEI YA NDOA YA MIAKA 75
Mzee Malila akiwa na mkewe katika ibada ya kukumbuka miaka 75 ya ndoa yao, shughuli ilifanyika kwenye kijiji chao cha Lwanjilo.
Oct 28, 2010
Njoo ufanyiwe maombi
Mhubiri akifanya huduma zake kwa staili ya nyumba kwa nyumba kama iliovyo kampeni za siasa bongo, hapa akiwa madukani Tunduma akitoa huduma kwa wafanyabiashara. indaba2010
MPUNGA HUU UNALIWA NA WAZAMBIA KULIKO WABONGO
shehena ya mpunga ikishushwa mashineni katika eneo la Karoleni Tunduma tayari kwaajili ya biashara ya mchele kwa wazambia ambao ndiyo wateja wakubwa katika eneo hilo^mpakani.
JAMANI BEI NZURI YA MAYAI YA KIENYEJI YAPO HUKU VIJIJINI
Mayai ya kienyeji bei yake ni 250 kwa moja wasiliana nasi kwa nambari hapo juu kona ya kulia hata kama unataka trey 1000.
NAUZA NAUZA NAUZA
haya nauza nauza hivi ndivyo biashara haigombi katika eneo la Tunduma, eneo hili maarufu kama black market hata mafuta ya ndege yanapatikana hapa
Mtaa wa Kongo katika mji wa Tunduma
Wadau wa blog hii wakiwa katika mitaa ya border ya Tunduma kufanya shopping kabla ya siku ya uchaguzi manake kwa eneo la Tunduma huwa mambo hayatabiriki, watu wameshaanza kununua mchele,unga na bidhaa za chakula kujihami na vijimambo vya mpakani, wakati ambapo tayari jeshi la polisi nalo limeweka lile gari maarufu kama kojozi kwaajili ya rasha rasha za election2010
SHAMBA LA EKARI MIA TANO LINAUZWA MBOZI
Ndugu watanzania, shamba kubwa lenye ukubwa wa ekari 500 lipo wilayani Mbozi kilometa 9 kutoka kwenye lami linalofaa kwa kilimo cha Ngano/shayiri, kahawa, mahindi na viazi. wasiliana na muuzaji kupitia namba iliyopo kwenye utangulizi wa blog hii hapo juu, tutakuunganisha na muuzaji.
Tundumq na bajaj mpaka lini?
huu ndiyo usafiri wa kila siku Tunduma inakadiriwa kuwa kila bajaj wastani kwa siku hulaza mapato kati ya shilingi 20,000 hadi 30,000 hizi ni zile zinazopelekwa kwa wamiliki wake achilia mbali walizobana madereva wake
Kiatu kinachoitwa bajaj kinavyowatoa chicha akina dada
Kiatu kinachoonekana hapo juu ndicho kinachovaliwa na watanzania wanawake wengi ikilinganishwa na viatu aina zingine vilivyotengenezwa na viwanda vya wachina vilivyopo hapa nchini na nje ya nchi, wakati wanaume wengi wakiwa wamevaa yebo yebo!
Mkemia wa umri mdogo akifanya uchakachuaji wa maji Tunduma
Mkemia kutoka mitaa ya Tunduma akijaribu kufanya uchakachuaji wa maji katika moja ya mitaa ya Tunduma, haifahamiki alikuwa analenga kufanya nini katika utafiti wake na matokeo yake atayatangaza wapi.
Oct 27, 2010
MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU MBOZI
Vifaa kwaajili ya uchaguzi mkuu 2010 vikiwa vimewekwa nje ya bohari kuu ya halmashauri ya wilaya ya mbozi tayari kusambazwa kwenye vijiji na kata.
Oct 25, 2010
TAARIFA KUTOKA SCOAN(TB JOSHUA JUU YA UNABII WA UCHAGUZI WA BONGO FEKI!!!!
Katika siku za hivi karibuni kulizuka uvumi nchini kwamba TB Joshua ametoa unabii kuhusiana na uchaguzi mkuu wa Tanzania kwa mwaka 2010, anchor wa mtandao huu baada ya kufuatilia kwa muda kwenye vipindi vyake hakuona chochote na hivyo kulazimika kumwandikia TB joshua kutaka ufafanuzi kupitia official website yake ya www. scoan.org haya ni sehemu ya majibu aliyonipa kupitia e mail yangu.
To: http://de.mc526.mail.yahoo.com/mc/compose?to=dtweve1@yahoo.com
Sent: Wed Oct 20th, 2010 6:58 AM PDT
Subject: IMPORTANT NOTICE
Calvary greetings in the mighty name of Jesus Christfrom The Synagogue, Church Of All Nations.
We have received inquiries from various persons inTanzania regarding a rumour that is being spread throughout the countryconcerning Tanzania’s upcoming elections. The rumour states that a prophecy wasgiven by Prophet T.B. Joshua concerning these elections and the partiesinvolved.
We, The Synagogue, Church Of All Nations, hereby statethat there was no prophecy given by Prophet T.B. Joshua regarding Tanzania, hergovernment, or her people.
Please note with utmost importance: If a prophecy hasbeen revealed by Prophet T.B. Joshua, it will first be broadcast on Emmanuel TVand subsequently posted on our websites: www.scoan.org (http://www.scoan.org/)and www.emmanuel.tv (http://www.emmanuel.tv/)
We continue to keep the nation of Tanzania, her peopleand her leaders in prayer. For the only way to show someone you love them is bypraying for them. We love the nation of Tanzania and believe, by God’s grace,that the best is yet to come.
Emmanuel! God is with us!
The SCOAN
www.scoan.org
info@scoan.org
To: http://de.mc526.mail.yahoo.com/mc/compose?to=dtweve1@yahoo.com
Sent: Wed Oct 20th, 2010 6:58 AM PDT
Subject: IMPORTANT NOTICE
Calvary greetings in the mighty name of Jesus Christfrom The Synagogue, Church Of All Nations.
We have received inquiries from various persons inTanzania regarding a rumour that is being spread throughout the countryconcerning Tanzania’s upcoming elections. The rumour states that a prophecy wasgiven by Prophet T.B. Joshua concerning these elections and the partiesinvolved.
We, The Synagogue, Church Of All Nations, hereby statethat there was no prophecy given by Prophet T.B. Joshua regarding Tanzania, hergovernment, or her people.
Please note with utmost importance: If a prophecy hasbeen revealed by Prophet T.B. Joshua, it will first be broadcast on Emmanuel TVand subsequently posted on our websites: www.scoan.org (http://www.scoan.org/)and www.emmanuel.tv (http://www.emmanuel.tv/)
We continue to keep the nation of Tanzania, her peopleand her leaders in prayer. For the only way to show someone you love them is bypraying for them. We love the nation of Tanzania and believe, by God’s grace,that the best is yet to come.
Emmanuel! God is with us!
The SCOAN
www.scoan.org
info@scoan.org
KWETU KUDUNDANA NI SEHEMU YA JANDO
Haya ni maisha ya kila siku kwa vijana waliopigika vijiweni, wanapodhulumiana hata shilingi 50/= ya sigara mambo huwa hivi kila siku. Ndiyo sababu kazi ya polisi kukamata vibaka inakuwa nyepesi kwakuwa kwa kuwaaangalia tu makovu usoni utabaini kuwa hawa ni watu waliozoea vipigo!!!!! hapa ilikuwa ni kituo cha mabasi cha Vwawa makaburini Jumamosi iliyopita.
WADAU VALUE FOR MONEY WANAPOPOZI KWA FOTO!!!
Jamaa wa idara ya ukaguzi wa ndani katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi (Kama wanavyofahamika kwa jina la utani la Value for money) wakiwa ngangali kinoma nje ya mjengo wa halmashauri hiyo baada ya kurejea kutoka shughuli za vijijini ambako kunahitaji usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa program mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa kupitia halmashauri hiyo. Kuanzia kulia ni dada nani hii, akifuatiwa na Sheikh Waziri Mwasa, Girlbert Rwehumbiza na Maganga Henze
WADAU NAO WALIKUWEPO
Kuanzia kulia ni Dr Charles Mkombachepa(mganga mkuu wa wilaya ya mbozi), Papa, Mwanasheria wa mji mdogo wa Tunduma Mwasalemba wakiwa kwenye pozi la picha katika harakati za kukabidhiana magari ya taka.
Hii ni sehemu tu ya mambo ya taka zinazozalishwa na wakazi wa mji wa Tunduma, wastani wa tani 37 huzalishwa kila wiki katika mji wa Tunduma hali ambapo uzoaji wake hapo awali ulikuwa kati ya Tani 15,000 hadi 20,000. Baada ya kupatikana magari haya mawili hali ya mambo inatarajiwa kubadilika na kuwa bomba sana man!!!!!!!!!!!!!!
Hii ni sehemu tu ya mambo ya taka zinazozalishwa na wakazi wa mji wa Tunduma, wastani wa tani 37 huzalishwa kila wiki katika mji wa Tunduma hali ambapo uzoaji wake hapo awali ulikuwa kati ya Tani 15,000 hadi 20,000. Baada ya kupatikana magari haya mawili hali ya mambo inatarajiwa kubadilika na kuwa bomba sana man!!!!!!!!!!!!!!
CHILEWA AKIFANYA MAJARIBIO KWENYE MOJA YA MAGARI YA TAKA
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Levison Chillewa akijaribu kuwasha moja ya magari yaliyotolewa kusaidia shughuli za usafi katika mji mdogo wa Tunduma ambao upo mpakani mwa Tanzania na Zambia.
MAANDALIZI YA WEKA TUNDUMA SAFI YAANZA
Kampeni kubwa ya kuufanya mji wa Tunduma kuwa safi ikiwa ni harakati za kuiondoa aibu kwenye macho ya nchi jirani kutokana na hali ya uchafu wa mji huo hapo awali- sasa imepamba moto baada ya halmashauri mama ya wilaya ya Mbozi kuamua kuusaidia mji mdogo wa Tunduma magari mapya mawili ya kuzoa taka yaliyonunuliwa kwa zaidi ya milion 150. Huu ni mfano mzuri kwa miji mingine katika kuhakikisha suala ya la usafi wa mazingira kuwa moja ya maeneo ya kimkakati. Tunduma ingawa ni sehemu ya eneo la wilaua ya Mbozi bado shughuli zake za kiuchumi kwa sehemu kubwa zinachangia mapato ya moja kwa moja kwenye serikali kuu (HAZINA) lakini wananchi wanahoji kiasi gani kinarejeshwa kwa uhalibifu wa mazingira unaofanywa na shughuli hizo kwenye eneo hilo kwa ujumla? manake maambukizi ya HIV kwa sehemu kubwa yanachangiwa na shughuli hizo za border post any way tupo kwenye majadiliano karibuni
Christian naye ana matumaini na Tanzania ijayo
Ingawa mama yake anaonekana kama anaelekea kukata tamaa kwa jinsi ninavyoendesha serikali ya familia yangu lakini kijana wangu Christian anaonekana ana matumaini makubwa na serikali yangu baba yake! Nakutakia maisha marefu na yenye busara na neema mwanangu Christian
Oct 5, 2010
UWANJA WA AMANI ZANZIBAR UPO TAYARI KUTUMIKA
Baada ya ukarabati wa kampuni kutoka China, uwanja wa amani unaonekana murua ukiwa umewekwa zuria kwenye eneo la kukimbilia huku hoteli zake zikiwa saafi baada ya ukarabati mkubwa: picha kwa kudesa kutoka issamichuzi blog
Oct 4, 2010
PM AKIWA NA BAN Ki Moon septemba 27,2010
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana huku akipiga picha na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kabla ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za Umoja huo jijiniNew York Septemba 27, 2010. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye umoja wa Mataifa.indaba2010
MAMBO YA FEDE KWENYE MTANDAO WA KATUNI
Mtembelee Mtaalam wa katuni hizi za kisiasa na kijamii na nyanja nyingine muhimu katika
.BLOG: www.artsfede.blogspot.com.
indaba2010
BARUA YA MTOTO KWA MWENYEZI MUNGU
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 alikuwa anahitaji sana shilingi 100,000
(Laki moja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake
akamwambia "muombe Mungu atakupatia. Mtoto alianza kuomba kila siku na kila
mara lakini hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia uamuzi wa
kumuandikia barua Mungu ili asome maombi yake.
Kisha akai-post barua ile. Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua
kwa
ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona bahasha iliyoandikwa
"Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali pa kuipeleka, Wakaamua
kuifungua.
Barua ilisomeka hivi:
"Mpendwa Mungu,
Jina langu ni EMMANUELEY, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la tatu
katika
jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania , bara la Africa .
Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja baada ya
kuomba bila kupata majibu toka kwako.
Naombasana unisaidie kwani mimi ni mtoto mdogo na sina uwezo wa kufanya
kazi na
kupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu ni maskini
sana .
Natanguliza shukrani.
Wako mtiifu,
EMMA."
Wafanyakazi wa posta walifurahishwasana na barua hiyo na kisha wakaamua
waipeleke kwa Rais . Rais naye alipoipokea ilimfurahisha
sana na
kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto huyo akidhani
kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingisana .
Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:
"Mpendwa Mungu wangu,
Nashukurusana kwa kusikiliza maombi yangu na kunitumia pesa nilizokuomba.
Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu yaTanzania .Kama ilivyo kawaida yao , wamekata kiasi cha sh. 98,000 kwa ajili ya kodi , kwa hiyo wameniletea Sh. 2000 tu
(Laki moja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake
akamwambia "muombe Mungu atakupatia. Mtoto alianza kuomba kila siku na kila
mara lakini hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia uamuzi wa
kumuandikia barua Mungu ili asome maombi yake.
Kisha akai-post barua ile. Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua
kwa
ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona bahasha iliyoandikwa
"Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali pa kuipeleka, Wakaamua
kuifungua.
Barua ilisomeka hivi:
"Mpendwa Mungu,
Jina langu ni EMMANUELEY, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la tatu
katika
jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania , bara la Africa .
Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja baada ya
kuomba bila kupata majibu toka kwako.
Naomba
kazi na
kupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu ni maskini
Natanguliza shukrani.
Wako mtiifu,
EMMA."
Wafanyakazi wa posta walifurahishwa
waipeleke kwa Rais . Rais naye alipoipokea ilimfurahisha
kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto huyo akidhani
kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingi
Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:
"Mpendwa Mungu wangu,
Nashukuru
Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu ya
MAMBO YA MUSTAPHA HASSANALI
Designers listerning to Patrick Lumumba of the Production Facility they visited on 30 September 2010.
Designers attending how the pattern drafting works
Picha kupitia mtandao wake.
Designers attending how the pattern drafting works
UNAKUMBUA ENZI ZA BUJAGA IZENGO KADAGO?
Hii ni taarifa ya habari kutoka Radio Tanzania Dar es salaam Msomaji ni BUJAGA IZENGO KADAGO" huyu ndiye askofu wa sasa namkumbuka sana mdau huyu kwa vichekesho balaa! hongera mdau kwa kukamua shule kisawa sawa! (indaba2010)
What is Lipenenga? wazee wanawafundisha vijana
Kwenye watu wazima haliharibiki neno, Wazee kama hawa ni hazina kwa utamaduni wetu ni nadra sana kuona vijana wakiendeleza ngoma zetu za asili na matokeo yake utamaduni wa asili unazizimia na badala yake mambo ya vidole juu yoyo nyiiiiingi!! vimetawala kwenye maisha ya kila siku
indaba2010
indaba2010
KIJIJINI KWETU WANAFUNZI WANA NJIA NYINGI ZA KUJIFUNZA JIOGRAFIA
Kama huko mjini mnatumia ramani za Ukutani, siye huku tupo kivitendo zaidi! ramani zetu zipo physically yaani mwanafunzi anashiriki kuiandaa hadi kuitumia! si unajua soda nazo za shida hivyo mnatangaziwa kwesho kila mtu aje na visoda(vizibo) kumi sawa sawa!!!!! basi baada ya kuleta inakuwa raw material ya ujenzi wa ramani ya africa mashariki.(indaba2010)
HII SIYO SEKONDARI YA KATA, NI PRIMARY MOJAWAPO KATI YA NYINGI ZILIZOMO MBOZI
Jengo la shule ya msingi mojawapo iliyopo wilayani Mbozi, kwa ujumla wilaya ya Mbozi inapokuja kwenye ujenzi wa shule zake za msingi kwakweli inafagiliwa kwa namna majengo yake yalivyosimama! DED ujiko ujiko!!!!!!!
indaba2010
indaba2010
VIJIJINI NDIYO ZETU KILIMO NA UFUGAJI SAMAKI
Mmoja wa wananchi wa wilaya ya Mbozi aliyejengewa uwezo kupitia idara za Kilimo, Maliasili na Maji namna ya kuhifadhi raslimali maji na huku akitumia bwawa lake kwaajili ya Kilimo cha Bustani, Migomba pamoja na ufugaji Samaki kijiji cha Igamba (indaba2010)
HUYU DOGO AKICHOKA MIKONO ANAWEZA KUSOGEZA MDOMO!
Kazi ya kukamua ng'ombe inaelekea kuhama kutoka matumizi ya vidole vya mkono hadi kwenda mdomoni manake dogo anaonekana kusogea kila dakika inavyoyeya baadaye atakamulia mdomo wake! (indaba2010
SIJASIKIA KWENYE KAMPENI WATU WAKIAHIDI KUTOA BAJAJI BURE VIJIJINI
Hivi wazee kama hawa wananyunda kwa mguu kilometa 850 kwa siku nyie mnawaangalia tu!! mbona hatuwasikii mkitoa ahadi ya kuwagawia bajaj bure? hivi mzee na yebo yebo zake hizi unadhani zitadumu kwa wiki mbili kama kila siku utaratibu ndio huo? yangu macho (indaba2010)
HAPA NDIPO MAKAO MAKUU YA WILAYA YA MBOZI
Eeebwana Ndiyo: hapa ndipo wa hapa hapa tunaishi! ndiyo makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi na pia ofisi za Mkuu wa wilaya Mbozi zimo humu humu mjengoni, vipi kwenye upande wa mazingira tunajalieeee? (indaba2010)
SASA TUMEHAMIA ILASI BUS BAADA YA WAHAPA HAPA MWINGINE KUTOKOMEA
Safari zetu kwenda mjini sasa hivi zinaaminika kupitia kampuni hii ya mzawa baada ya Mzawa mwingine kufulia sijui kufanya nini manake tunaona kama inasua sua vile! any way tunawapongeza kwa pamoja kutufanya wakazi wa Mbozi kuiona Dar Kila siku kupitia mabasi yenu (indaba2010)
Oct 3, 2010
ENZI ZA KUREKODI HOTUBA KWA RADIO CASSETTE!!!!
Wakazi wa mjini Iringa wakirekodi moja ya mikutano ya kampeni zinazoendelea hivi punde kwa kutumia chombo hicho kipyaaaa! aina ya Aterch kama enzi za mwalimuuuu kumbe kuna recoders ndoooooogo kama pini technolojia bwana!!!
KARIBU KWA HUDUMA ZA INTERNET
Kwa huduma mbalimbali za bidhaa za ofisini, photocopy, fax na internet kwa ujumla tembelea Indaba Business Centre iliyopo mkabala na MBOCU ama wasiliana nasi kwa +255764947555. KARIBUNI SANA
KIJIWE MAARUFU CHA DRAFT MBOZI
Kijiwe hiki siku zote hukosi wadau wa draft, hapa ni ustadh -teacher akiwa anamenyana na Profesa Kipara huku wadau wengine wakifuatilia !!