Jul 29, 2011

Taswira Mbalimbali Za Ziara Ya Kikazi Ya Rais Jakaya Kikwete Huko Mtwara




Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ubanguaji unaofanywa na wakulima wadogo katika kijiji cha Kitama,Wilayani Tandahimba wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika ghala jipya za mazao wilayani Tandahimba.
Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dr.Zulkarnain Ikaji akimwonesha Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete gari la kubebea wagonjwa aina ya bajaj litakalotumika katika Zahanati ya Sengenya wilayani Nanyumbu jana
Rais dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua korosho iliyosindikwa kwa mashine katika kiwanda cha Rift Valey Foods, wilayani Tandahimba.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua chanzo cha Maji ya mradi wa Makonde Water Supply katika bonde la Kitangari wilayani, Newala, mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.
Rais Dr.Jakaya Mrisho kikwete na kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dr.Zulkarnain Ikaji wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi Zahanati ya Sengenya, iliyopo wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara Jana.Picha na Freddy Maro-IKULU

"

LUDACRIS: NINAZO NYIMBO ZA KUTOSHA KUKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WANGU KATIKA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA JUMAMOSI

Mwanamuziki Ludacris kutoka nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika asubuhi hii kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dare es salaam, Ludacris alikuwa akizungumzia onyesho lake atakalolifanya kesho, katika tamasha la Mwendelezo wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwabja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, katika picha kulia ni Mkurugenzi wa radio Clouds Ruge Mutahaba. Ludacris amesema anazo albam saba hivyo katika albam hizo anatarajia kutoa burudani ya kutosha ili kukonga mioyo ya mashabiki wa wa muziki wake nchini Tanzania
Mwanamuziki Ludacris wa pili kutoka kulia akiwa katika mkutano huo kulia ni Ruge Mutahaba mkurugenzi Clouds kushoto ni Caroline Ndungu, aliyekuwa mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweriers na Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo.
Meneja wa bia ya Serengeti Lager Allan Chonjo akizungamza katika mkutano wa waandishi wa habari wakati alipozunguzia tamasha la Serengeti Fiesta, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, katikati ni Mwanamuziki Ludacris na mwisho ni Mkurugenzi wa Clouds Ruge Mutahaba.
http://fullshangwe.blogspot.com/
"

Soulja Boy Cops Himself A $55 Million Private Jet / Man Calls NFLer Larry Johnson The "N" Word And Sues Him For Assault

Soulja Boy is celebrating turning 21-years-old with a $300K birthday bash in Miami...and a $55 Million private jet to top it off! Yes....you read that number right.

Get the deets on the king of conspicuous consumption inside and find out about the man suing Larry Johnson for assault, and who called him the 'N' word!

A source close to Soulja Boy told TMZ that the rapper bought himself a G5 to celebrate his 21st birthday this week. And guess how much it set him back......$55 Million!

So what does $55M get you these days?

Well....the jet itself cost $35 Million, but Mr. Boy spent an additional $20M pimping the jet out with '...12 custom Italian leather seats, flat screen TVs, 4 liquor bars, a special travertine tiled floor, and Brazilian hardwood cabinets.' He's also installing a luxury bathroom and getting a custom paint job with his logo on it.

And in case you thought that was over the top, he's also spending $300K on a big birthday party in Miami tonight.

Hmmm.....it''s his money and he can do whatever he wants. I just wonder will we be revisiting these purchases in 2021 on VH1 'Behind The Music' wondering what the hell he was thinking...while we trace where all the money was spent.

Also in the news....

Former All-Pro running back Larry Johnson is being sued by a man who claims Larry gave him a brutal beat down after a Miami party. But before you take his side, the man reportedly told the cops 'This n**ger is going down' while he was filing his report.

According to the civil lawsuit fild last week, John Phillip Graney says Larry Johnson punched and kicked him after a party in May. And when Miami beach police responded, John told them,

'This n**ger is going down. He needs to learn a lesson, it's going to cost this prick.'

You can view some of John's injuries here:

John says he suffered cuts to his face and ear, 3 herniated discs and a torn rotator cuff.

When asked about the 'N' word comments, his attorney said John does not recall making those comments. Of course not.

Larry Johnson, who has a history of angry lash outs, has responded through his lawyer saying this is an extortion attempt to get money from him.

"

MATUKIO KUTOKA BUNGENI DODOMA

Mbunge wa Mtera, Job Lusinde akiwa na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 29, 2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanakwaya ya Kanisa la Moravian ya Mbeya Mjini kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 29, 2011. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
"

Jul 25, 2011

MBEYA PRESS WAUNGANA NA WANAHABARI KATIKA MAOMBOLEZO YA DANNY MWAKITELEKO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

CHAMA cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mbeya(MBPC) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwanahabari mwenzetu,Danny Mwakiteleko kilichosababishwa na ajali ya gari jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa MBPC mkoa wa Mbeya,Christopher Nyenyembe amekielezea kifo hicho kubwa ni pigo kubwa katika tasnia nzima ya habari hasa kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao marehemu enzi za uhai wake.

“Mwakiteleko alikuwa kamusi ya kitaaluma na kisima cha fikra,mfumbuzi na mbunifu wa kazi mbalimbali za kihabari na aliweza kufanya kazi zake na kuibua vipaji vya waandishi wengine,hakika wengi hawatakuja kumsahau”Alisema Nyenyembe.

Kwa kutambua uwezo aliokuwa nao kwa niaba ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya nachukua fursa hii kutoa pole za dhati kwa ndugu na familia yote ya Mwakiteleko bila kuwaacha marafiki zake wa karibu na wafanyakazi wa New Habari alikokuwa akifanya kazi kama Naibu Mhariri Mtendaji.

Kifo cha Mwakiteleko licha ya kuwa pigo kubwa katika tasnia ya habari kwa namna moja au nyingine kimetuachia fumbo kubwa kwa wanaharakati wengine waliokuwa wakitumia kazi zao kupiga vita vitendo vya hujuma,rushwa na ufisadi wa kutisha katika Taifa letu.

Mwakiteleko alikuwa kioo hasa cha jamii katika kutekeleza majukumu yake,alikuwa mpole,mkalimu na mcheshi wakati wote lakini alikuwa makini zaidi katika usimamizi na utendaji wake wa kazi ambao ulimjengea heshima na nidhamu kubwa katika uongozi wake kama Mhariri kila alipokuwepo.

Tunatambua kuwa kifo ndiyo njia pekee ya kumtenganisha binadamu yoyote na ndugu zake,marafiki na jamaa wa karibu waliozoeana na kwa kuwa hayo ndio mapenzi ya MUNGU,tumuache Mungu aitwe Mungu na jina  lake lihimidiwe Milele…AMEN.
IMETOLEWA NA 
CHRISTOPHER NYENYEMBE
MWENYEKITI
MBEYA PRESS CLUB

WAZIRI MUNDU ATUA MBEYA, ATETA NA MKUU WA MKOA KWA SAA1.15

Waziri Mundu akisaini kitabu cha wageni katika uwanja wa ndege wa mbeya mara baada ya kuwasili uwanjani hapo na kupokelewa na uongozi wa mkoa wa mbeya uliongozwa na Afisa katika sekretalieti ya Mkoa bwana Moses Chitama

Miongoni mwa viongozi walioongoza na waziri Mundu pamoja na watu waliofika kumpokea wakiwa kwenye chumba cha VIP ambamo waziri alipumzika dakika chache kabla ya kwenda kuonana na mkuu wa mkoa wa Mbeya. Waziri mundu aliwasili uwanjani hapo majira ya saa 1.40

Na Danny Tweve
Waziri wa Uchukuzi Omary Nundu amewasili mkoani mbeya akiwa na ujumbe wa watu wanne akiwemo kiongozi wa chama cha wasafirishaji wa mizigo Zacharia Hans Pope kwa lengo la kushughulikia mgomo wa madereva wa magari yanayopeleka mizigo nje ya nchi.
Waziri huyo ambaye awali alipanga kuzungumza na madereva hao majira ya saa 10, kwa matarajio ya kuwasili saa 9.00 alasiri alichelewa na kutua uwanjani mbeya majira ya saa 1.40 Usiku.
Mara baada ya kuwasili alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya ambapo aliungana na kamati ya Ulinzi na usalama akiwa yeye na ujumbe wake ambapo waliteta kwa takribani saa 1.15 juu ya mgogoro huo.
Imeelezwa kuwa mkutano huo utafanyika asubuhi majira ya saa tatu katika eneo la Sogea mjini Tunduma.
Indaba africa kama kawaida itaendelea kuwapa kila kinachojiri  kuhusiana na suala hilo, ambalo kwa namna moja limeathri uchumi wa nchi, huku hali ya uchafuzi wa mazingira katika mji wa Tunduma ikiendelea kushika kasi kutokana na msongamano wa magari ambao umepelekea hata huduma za jamii kupungua eneo la Vyoo .

BRECKINGNEWS>BAADA YA HALI YA HEWA KUCHAFUKA TUNDUMA, OMARY NUNDU ATOKEA MCHANA HUU



Taarifa zilizoufikia mtandao wa Indaba zinasema, waziri wa uchukuzi Omary Nundu atazungumza mchana huu na madereva wa magari yanayosafiri kati ya Tanzania na nchi zingine kupeleka na kuleta mzigo maarufu kama Transit.
Mkutano huo ni matokeo ya kugomewa kwa jitiohada zote zilizofanywa na viongozi wa mkoa wa Mbeya ambapo mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile jana alimtuma mkuu wa wilaya kupeleka ujumbe wa kuwataka wasitishe mgomo huo wakati mambo yao yakishughulikiwa, lakini wakati mkuu huyo wa wilaya akisoma barua hiyo alipofikia mwisho akataja imesainiwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya John MWAKIPESILE ghafla wakalipuka kuzoea,

Awali walikuwa wakipiga makofi kwa kila kipengere kilichosomwa, lakini ilipofika hatua ya kusoma aliyeandika waraka huo basi hali ikawa siyo, jambo linaloashiria kuwa walihisi hizo zilikuwa ni porojo za kuwatuliza na si ujumbe kutoka kwenye mamlaka za juu kama walivyotaka.\
Omary Nundu amelazimika kufika leo hii baada ya gari moja lililokuwa likiendeshwa na mtanzania mwenye asili ya somalia kuzuiwa na madereva wenzake likiwa barabarani na kisha wakachomoa funguo na kutokomea nazo, hivyo kuzuia shughuli za barabra kuu ya Tunduma -Mbeya.
Imeelezwa kuwa gari hilo linatumia passwords ama mzingo katika kuliwasha ambapo pia ni lazima funguo iwe halisi ambapo vibonyezeo vyote vipo kwenye funguo hali ambayo ililazimu polisi kuwa wapole kwani walishaanza kubutua mabomu.

Kilicjhotufikisha hapo ni matokeo ya serikali kuchukulia juu juu mgogoro huo ambapo ilionyesha kuto kuupa uzito unaostahili katika kushughulikia zmalalamiko waliyoyatoa madereva yakihusisha haki zao pamoja na baadhi ya kero ambazo tayari zimeanza kupatiwa ufumbuzi.
Madereva hao walianzisha changamoto hiyo tangu  July 17 baada ya kuandika barua kwenda kwa waziri mkuu lakini ikakosa majibu kwa kipindi chote hatua ambayo wakaamua kuchukua maamuzi lakini wakionyana wenyewe kutokujihusisha na uharibifu wa mali.
Hata hivyo taarifa zilizozagaa jana zilianza kuonyesha hofu kubwa baada ya kudaiwa baadhi ya madereva hao wametegesha petroli kulipua magari ikiwa polisi wangetumia mabomu ama kuanzisha operesheni ya FFU, hatua hiyo iling,amuliwa na idara za Inteligensia ambapo magari ya zima moto yaliandaliwa jana kukabili hali hiyo wakati magari ya washa washa yalipokuwa yakizunguka na kutoa tahadahari jana jioni. 
Mtaendelea kuelezwa kinachoendelea kupitia blog hii

Jul 22, 2011

CHUO CHA MIPANGO DODOMA KUWA NA JENGO REEFU KULIKO YOTE MKOANI DODOMA

Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Chuo cha Mipango Dodoma kama nilivyouona nikiwa kwenye mazingira hayo jana

Jengo refu kuliko yote Mkoani Dodoma litakalokuwa na Ghoroga Nane likiwa kwenye hatua za unjenzi nyuma ya Ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma, jamani mipango mie sijui nilie manake enzi nikisoma hapo jamani majengo yalikuwa baado lakini sasa vitu vimeota kama uyoga!!!!

Nani kakwambia darasa linaangalia utu uzima, hapa naelekezwa namna ya kuboresha logical frame work! ama kwa kiswahili mnaita Bao Mantiki

Hapa wazee wangu hawa wa Chuo cha Mipango wakisukuma draft kwa burudani zao wakati wa mapumziko getini, raha kweli!


HII NI DODOMA, MAKAO MAKUU YA TANZANIA



Hapa ni Anglican cathedral


Msikiti Mkubwa uliopo Dodoma karibu na eneo la Chako ni chako, nimeukubali mandhari zake hasa masaa ya jioni

Ndege ikitua katika uwanja wa ndege wa Dodoma kama nilivyoinasa nikiwa katika harakati za kuelekea chuo cha mipango
Mnara uliopo karibu na ofisi za TAMISEMI wenyewe tunaita round about

HAYA AKINA MAMA BIDHAA MPYA MNATANGAZIWA

WADAU VIATUZIII HAOOO WAMESHUSHAAA MAMBO NI YALE YALE YA FUNGA KAZI ZA VIATUUUUZIII unyayooooo AMBAPO SASA MABIHARUSIII NA MASHORIII WOOTE WANAOTHAMINI MIGUU YAO...KUTINGA KIATU CHA VIATUZI NI SAWA NA KUUKATIA INSURANCE MGUU WAKO KWANIIII NI VYA UKWE'E hudhuriki MBALI NA VIATU KUNA CLUTCHZ ZILE STYLE MPYA (ENVELOPE CLUTCH) NA BILA KUSAHAU VITUPIOOOOO (ACCESORIEZ)
KUONA ZAIDI MAMBO ZAIDI DUMBUKIA BLOGUNI
WANAPATIKANA:: SEA VIEW PLOT NO.10
MAWASILIANO:: 0715 850855
MABLOCKING COLOR KIBAO....KAJIBLOKUENI
HIZI HAPA NDO ENVELOPE CLUTCH....umeona ee kitu cha bahasha hapo kati