May 10, 2014

MICHUANO YA MABINGWA WA MIKOA YAANZA- KITUO CHA MBOZI CHAANZA KWA SARE

RCL Yaanza Kutimua Vumbi Katika Vituo Vitatu Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoshirikisha timu 27 inaanza kutimua
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoshirikisha timu 27 imeaanza kutimua vumbi leo mei 10  katika vituo vitatu vya Morogoro, Mbeya na Shinyanga kwa mechi mbili kila siku.
Kundi A ambalo mechi zake zinachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, African Sports ya Tanga itacheza na Kiluvya United FC ya Pwani saa 8 mchana wakati saa 10 jioni ni Mji Mkuu FC (CDA) ya Dodoma dhidi ya Pachoto Shooting Stars ya Mtwara.
 
Jumapili (Mei 11 mwaka huu) katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya Bulyanhulu FC (Shinyanga) na Kariakoo SC (Lindi) itakayoanza saa 8 mchana wakati saa 10 jioni ni Navy FC (Dar es Salaam) na Abajalo FC pia ya Dar es Salaam.
 
Kundi B katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya litaanza ligi kwa mechi kati ya Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC (Morogoro) saa 8 mchana wakati saa 10 jioni ni AFC ya Arusha na Panone FC ya Kilimanjaro.
 
Mei 11 mwaka huu saa 8 mchana ni Mpanda United ya Katavi na Magereza ya Iringa wakati Tanzanite (Manyara) na Njombe Mji (Njombe) zenyewe zitaumana kuanzia saa 10 jioni.
 
Simiyu United ya Simiyu na Mvuvumwa FC (Kigoma) ndizo zitakazoanza kucheza saa 8 mchana katika kundi C linalotumia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Saa 10 jioni ni mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars FC.
 
Jumapili (Mei 11 mwaka huu), mechi za kundi hilo zitakuwa Singida United (Singida) na Mbao FC ya Mwanza kuanzia saa 8 mchana wakati jioni ni pambano kati ya mabingwa wa Mkoa wa Mara, JKT Rwamkoma FC na Geita Veterans FC ya Geita.
 
Ligi hiyo itamalizika Juni 2 mwaka huu ambapo timu itakayoongoza kila kundi itapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015
 
MATOKEO KATIKA UWANJA WA CCM VWAWA-MBOZI
 
Katika michezo miwili iliyochezwa leo hii baina ya Timu za Morogoro na Rukwa na Mchezo wa pili baina ya Kilimanjaro na Arusha, matokeo ni kwamba timu hizo zimetoka uwanjani zikiwa nguvu sawa baada ya kutofungana
 
Ujenzi Rukwa ilimenyana vikali na Volcano Fc ya morogoro lakini kosa za hapa na pale kwa pande zote zilileta matokeo tasa kwa timu zote
 
Katika mchezo wa pili AFC ya Arusha zilipelekana puta na Panone Fc ya Kilimanjaro na hadi mwisho wa mchezo licha ya kosa kosa za hapa na pale zilizoiandama panone matokeo ya mchezo huo yaliishia kuwa suluhu ya kutofungana.
 
Awali michezo hiyo ilipangwa kuchezwa katika uwanja wa sokoine mjini Mbeya lakini kutokana na uwanja huo kuandaliwa kwaajili ya mchezo baina ya
Timu za Taifa za Tanzania na Zimbabwe michezo hiyo imehamishiwa katika wilaya ya Mbozi kwenye uwanja wa CCM wa Vwawa ambao ni uwanja wa nyumbani wa timu ya Kimondo SSC inayoshiriki ligi daraja la Kwanza Tanzania