Sep 30, 2010

UTANI KWA WACHAGA HUUU

Mchagga alinunua mbuzi! Akamwambia mpishi; Nyama nusu ipikie pilau na nyingine itie kwenye friza! Kichwa fanya supu na miguu fanya mchuzi chukuchuku! Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa! Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.

Mpishi akamuuliza : Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye

simu yako?

UPENDO NKONE NDANI YA NDOA SOON!!!

Baada ya kuishi katika hali ya ujane kwa zaidi ya miaka tisa,mwimbaji wa nyimbo za injili hapa nchini Bi Upendo Nkone anatarajia kufunga ndoa na Mchungaji John Mbeyela oktoba 17 mwaka huu.

Gazeti la Majira limeeleza kuwa Upendo Nkone anatarajia kuagwa oktoba 11 nyumbani kwao Kigoma,Tanzania na ndoa yake na mchungaji huyo ambaye ni mgane mwenye watoto watatu itafungwa katika kanisa la Naioth maarufu Kwa Mwasota lililopo Mabibo Makuburi jijini Dar es salaam.Mwimbaji huyo aliyeanza kuimba miaka mitano iliyopita amefanikiwa kutoa albamu tatu ambazo ni Mungu Baba,Hapa Nilipo na Zipo faida

MAMBO YA UCHAGUZI MKUU 2010

Ebwanaeee unacheza na kutetea jimbo la uchaguzi hiki ni chama tawala kikiwa na mkakati wa maji kwa wote kaaazi kweli kweli!

KAKOBE AKANA KUHUBIRI SIASA KANISANI

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF),Zachary Kakobe amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu kumzushia uongo kuwa amekuwa akifanya kampeni kwenye kanisa lake.
Akizungumza  leo asubuhi, mchungaji Kakobe amesema kuwa hawezi kufanya kitendo hicho kwani anafahamu haki ya kila raia.
“Mimi siwezi kumpigia mtu kampeni isipokuwa Jumapili iliyopita nilikuwa nikitoa elimu ya uraia kwa waumini waungu ili kujua haki na wajibu wao katika siku ya kupiga kura, ” amesema.
Mchungaji Kakobe amesema kuwa katika siku hiyo kulikuwa na wagombea mbalimbali kutoka katika vyama siasa kwenye ibada.
Amesema kuwa aliamua kutoa elimu ya uraia kwa waumini wake ili kutekeleza agizo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) la kila kiongozi kutoa elimu ya uraia kwa watu wake.
“Mimi nilikuwa natimiza agizo la NEC kwani kitendo cha mtu kumpigia kura mtu ni cha utashi wake mwenyewe na siwezi kumlazimisha mtu amchague mtu fulani, ” amesema Kakobe.
Amesema kuwa kuna baadhgi ya watu wana mambo yao ambapo wamekuwa wakitengeneza jambo bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha.
Hata hivyo Kakobe amesema kuwa wakati huu ni muhimu hivyo kitendo cha kutengeneza jambo na kulizungumza hadharani si kizuri.
Jana Taasisi ya Maimamu ya Bukhary ya Kiislam inayoongozwa na Sheke Khalifa Khamisi ilitoa tamko la kumkanya Askofu Kakobe kuacha ushabiki wa kisiasa ndani ya kanisa kwa kitendo cha kuwataka waumini wake kumchagua mgombea fulani.
Katika taarifa ya taasisi hiyo ilisema kuwa kitendo cha askofu huyo kufanya hivyo kinaweza kuhatarisha amani nchini.

MCHUNGAJI GEOFREY MWAKIHABA ALIPOPEWA BARAKA YA ASKOFU MSAIDIZI

 Mchungaji huyu nakumbuka ndiye aliyefungisha ndoa yangu, dalili ni njema kwa safari yako ya kumtumikia mungu.
Washarika wa usharika wa KKKT Forest wanakutakia utekelezaji mwema wa majukumu ya nafasi hii kubwa ya kuwa (askofu msaidizi) mshauri mkuu wa askofu wa KKKT dayosisi ya Konde.

MZEE RAMADHANI ALLY ASTAAFU SAUTI YA UJERUMANI

Watangazaji wa sauti ya Ujerumani kuanzia kushoto ni Sekioni Kitojo,Ramadhan Ally ambaye amestaafu,Abdul Mtulya na Aboubakary Liongo wakiwa wamepozi kabla ya party ya kukata na mungu iliyofanyika kumuaga mzee Ramadhan Ally ambaye amestaafu utangazaji Deutchwelle baada ya kutumikia miaka 40 kila lakheri mzee!. Picha kwa hisani ya Mdau Michuzi

MZEE MARIDAD TUMBO LINASOKOTA AMA

Hii ilikuwa kwenye moja ya shughuli zangu-sendoff ya mke wangu bwana weee ilikuwa burudani kweli kweli utadhani tumbo linasokota vile!!!!

#links

#links Kwa huduma mbalimbali za bidhaa za ofisini, photocopy, fax na internet kwa ujumla tembelea Indaba Business Centre iliyopo mkabala na MBOCU ama wasiliana nasi kwa +255764947555. KARIBUNI SANA

MUNGAI ATINGA MAHAKAMANI

Leo mchana katika mahakama ya Hakimu mkazi Iringa, mzee Mungai alipanda kizimbani kujibu tuhuma za Rushwa wakati wa mchakato wa uchaguzi ndani ya chama cha mapinduzi, hapa akitoka nje ya mahakamani. kesi yake imesogezwa mbele hadi October 15 mwaka huu. Picha kwa hisani ya Godwinfrancis.blogspot.com

UKISHA LEWA PACKING INAKUWA SHIDA

Hawa ndiyo walevi wa ulaya alama za packing hazionekani sasa magari yanakaa kivyake vyake

KIU BABA INAWEZA KUKULAZIMISHA UFANYE YASIYOFANYIKA!!!!

yaaa haya ndiyo maisha ya hapa hapa duniani, mbinguni ni kuimba mapambio tuuuu

ZEEE MAPOREJI!!!! KIJIJINI WATOTO WANATAKATA BWANA!!!!!

Yaa hawa ni wakazi watarajiwa wa kijiji cha Kamsamba walikutwa na Camera yangu wakiwa wanajiroad uji wa mtama kwenye uwanja wa wazi nje ya nyumba yao hii ni sehemu ya kawaida kwa maisha ya vijijini sijui huko kwenu mjini?

UNAPOFIKA TUNDUMA USIHANGAIKE, ULIZA HIGH CLASS HOTEL

Tunduma inazidi kupanuka, hii ni hoteli nyingine iliyojengwa kwaajili ya Huduma kwa wageni wanaoiingia katika mji huo unaokua kwa kasi! Tunduma always provides  comfort  to the guests, why not take a night in High Class Hotel, Waambie wenzio wakalale hapa kalagabahoooo

DARAJA KUUUUUBWA ANALOTARAJIA KUJENGA JK KAMSAMBA

Nakumbuka mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ahadi zake alitaja kuwa daraja la Kamsamba kuunganisha Upande wa Rukwa litajengwa kupitia TANROADS mkoa wa Mbeya, hii ni habari ya Matumaini kama utekelezaji wake utafanyika, huu ndiyo upana wa mto huo ambao kila mwaka umekuwa ukimeza maisha ya wananchi wa eneo hilo kutokana na kuwepo mamba wengi kwenye mto  huo ambao hutokea ziwa Rukwa.

UNAKUMBUKA ENZI ZA MH SIMBASA ELIAKIMU BUNGENI

Aliyevaa Kapelo ya CCM mwanzoni ndiye aliyewahi kutikisa bunge miaka ya nyuma wakati akisimamia kamati ya Maadili na haki za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na huyo si mwingine ni ELIAKIMU SIMPASA sasa ni mwananchi wa kawaida tunakaa naye kwenye viti vya nyuma!!!
Huu ndiyo msongamano wa magari katika mji wa Tunduma, mkakati wa kujenga kituo cha pamoja baina ya nchi za Tanzania na Zambia katika ukaguzi wa magari utasaidia kupunguza msongomano kwenye mji huo. Unajua matokeo ya msongamano huu ni nini? dereva anashuka gari likiwa kwenye foleni anaenda hotelini anachukua chumba anamaliza shida za muda mfupi anarejea bado msongamano vile vile!!!!!

UNAKUMBUKA ENZI ZA NYIMBO YA MTAA WA SABA

Sasa nimehamia mtaa wa saba!!! unahamaje na hicho kiatu?  ilikuwa watu wanakula raha kwa kwenda mbele manake hiyo kitambaa eneo la paja bana halafu chini malizia mwenyewe!!!!

TUKUGHULISYA INDISI--- ZOTE MIA

WAKAZI  wa kijiji cha Kiwira wilayani Rungwe wakifanyiana taiming kwenye kuuza ndizi baada ya wadau wa blog kupack mahala ! ndizi katika eneo hili huuzwa shilingi Mia moja kwa ungo kama zinavyoonekana!!!!!! mwee vijijini kuzuri chakula buuuurereeeee!!!!!!!!!

Sep 29, 2010

RIDHIWAN AKUTANA NA MAGUMU IRINGA- WANYALU WASEMA SWELA


Na Francis Godwin,Iringa


MTOTO wa mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Jakaya mrisho Kikwete ,Ridhiwan Kikwete leo ameonja joto la jiwe katika ziara zake za kampeni ndani ya CCM baada ya kutimuliwa mbio zaidi ya mara moja wakati akitaka kufanya kampeni za CCM katika taasisi za umma.
Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapindunzi (UVCCM) Taifa akiwa na viongozi akiwemo aliyekuwa mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela na washiriki wengine wa kura za maoni kama Jescar Msambatavangu walifika katika shule ya msingi Ipogolo wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kumuunganisha mgombea ubunge wa jimbo hilo Monica Mbega na Mwakalebela japo mkakati huo uligonga ukuta.
Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake cha ndani ya vijana wa CCM kwa lengo la kuvunja makundi ndani ya chama hicho ,aliyekuwa mmoja kati ya wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo hilo Msambatavangu alipita mitaani kujaribu kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza mtoto huyo wa Rais Kikwete japo waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.
Hata hivyo baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo kwa ajili ya kutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili katika shule hiyo ya msingi Ipogolo bado msafara huo uliweza kufika katika eneo hilo kwa ajili ya mkutano japo idadi ya vijana waliokuwa wamefika ilikuwa ni kama vijana 10 pekee.

SASA HII INAITWA JINO KWA JINO TUTACHAKACHUANA

 eeeeeeeeeeeh hizi ndizo walizorejesha hawa jamaa kutoka kyama cha nani hiiiiiii si mnaona wenyewe rangi?
Aaaaaa wapiii!!! jamani si mnaona rangi za chama cha nani hiiiiiii!! eeeeeh wamerejesha zote hizi tena zingine nimeacha nyumbani , na watu kibao na nani hiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

JAMANI KUMBE DAWA ZA KUONGEZA MCHINA NI HATARI

Eeebwana !!! jamaa keshaharibikiwa  majukumu yote ya uumbaji hawezi tena hii yote ni kwasababu ya kudanganyika na matumizi ya zana za kichina za kuongeza maboresho ya ndoa!!! tahadhari hasa kwenye maeneo ya mijini ambako kuna malalamiko mengi ya wanaume kuishiwa nguvu na uwezo wa kutumika, msijeenda kwa magagula na wachina kuongeza sijui unene, sijui urefu  yatawakuta haya!!

ALAJII INAPOKOLEA WATU WANAANZA KUACHIA BACKGROUND

Eeeh hii ninayoonyesha mimi ndiyo imeshuka jana kwenye pipa!!!! aaah wapii hunizidi mimi hii imeshushwa kwenye helkopta ya mgombe leo mchana!! ndivyo wanavyoonekana wakibisha hao wawili walioamua kutuonyesha uumbaji wa mwenyezi on reversed side !!! ilikuwa kwenye masuala ya mijumuiko bwana!.

HIVI WANAPOZIPIGA KAVU KAVU NI UCHAKACHUAJI WA AMANI AMA

 Unafikiri sikuogopi nakuogopa oooooh!!!! ndivyo anavyotamka huyo mwenye ka kijani kabla hajabanwa na haja ya kichapo
Oooh Adija naye hataniwi!!! yaani ameamua kumfanyia mwenzake fumu!! aah yanini malumbano bora tuzichape kavu kavu kama ni masuala ya kuchakachua amani mie sijali bwana, ila nikichaniwa nanihii itakuwa mbaya !!!

Hizi ndiyo kampeni za uchaguzi mkuu

Ebwana ndiyo kazi ipo kwenye mchakato atakayeshinda hoyeee atakayepigika hoyeee, ila hatutaki uchakachuaji tafadhari!!!!!!!!!!!!

HIZI NDIZO HARUSI ZETU VIJIJINI

Mmoja wa wadau wa karibu na blog hii akiwa kwenye mwinuko mkali kutoka upande wa pili wa mto  huko Ileje hii ilikuwa ni baada ya kufunga pingu za maisha  na kwa kuwa huku kwetu vijijini magari yanaachwa upande wa pili yaani ng'ambo ya mto kutokana na masuala  mazima ya miundo mbinu  basi ilibidi Bi Harusi atambulishwe kwa staili hii kuwa  nyumbani ni nyumbani hataka kama hatupandi magari!!!!

Baada ya hapo tulimpitisha kwenye vitindi vya Ulanzi -wenyewe tunaita kwenye mianzi na kumtambulisha rasmi kuwa hapa ndipo tulipokulia na kilikuwa kinywaji chetu cha kila wakati tulipojisikia kuondoa uchovu wa mazingira yetu hatarishi basi tulizima stim na ulabu kidogo na nchi ikaendelea kuwa nzuri mpaka leo!

OOH KIONGOZI NATAMBUA UWEPO WAKO

Ndivyo anavyoonekana kuzungumza Bwana Mwantona ambaye katika mazingira yetu ya kazi ni mtu mhimu sana hasa kwenye kipengere cha uwezeshaji! manake ili uende kijijini unahitaji mkono wa DT afanye kazi yake then inakuwa rahisi eye to eye contact na wananchi kisha mkafanya mambo yenu ya uragbishi na ujasilishaji na uchakachuaji!!!!!!

MDAU ANAPOUNGANA NA MWANAYE KUKUMBUKA SIKU YA KUZALIWA

 Ni binti wa mdau wa blog hii bwana Mtoni, yeye anaitwa Irene anasema hakuna kulala mpaka hii blog ifahamike ndani na nje ya Bongo manake vinginevyo sauti zetu vijijini hazita sikika!!
Haya baba Pokea Keki kuashiria kuwa hata huku vijijini tunamudu kufanikisha matukio kama haya. Ilikuwa wakati wa kuadhimisha miaka  mitatu ya Binti Mtoni au yeye mwenyewe anaitwa Irene.

WAHESHIMIWA WANAPOPEANA MSIMAMO WA TUKAZUNGUMZE NINI BUNGENI

Mh Mwakyembe (Kyela MP) anaonekana akiteta jambo na Mh Zambi (Mbozi Mashariki Mp) kama wapo kwenye group discussion vile kama tungekuwa kwenye mazingira ya Vyuo. Hii ilikuwa wakati wa uzinduzi wa kituo cha kulelea wato walio katika mazingira hatarishi cha Lucy Mwandosya huko Lufilyo Rungwe.

Enzi za Mwalimu tulikuwa tunavaa hivi

Yanini malumbano! yanini maneno!!! najiweka pembeni kuepusha msongamano!!!! hizi ndizo nyimbo za siku hizi enzi zile kwa kiatu hiki usingeweza kucheza nyimbo zenu za vidole juu mara umeshika suruali sehemu za siri  mara oooh yoyo eyo eyooo!!! enzi za mwalimu bwana unamkuta mtu amevaa slimu na kibwanga aka fundi malizia kitambaa changu huko chini na juu afro ama way!!!! au sikuwepo

NAKUMBUKA SANA TRIP ZA VIJIJINI HASA KAMSAMBA

Nakwambia field hatulembi hasa njaa ikivuka lengo! hapa watu wanajitupia kwa supu bila kujali imechinjwa kwa kuinamishiwa kibla ama laa  wala hatuulizi nani kachinja sie ni kula tuu!!

SIKU TULIPOTEMBELEA OFISI YA DC WA ISOKA ZAMBIA

Hapa ndipo ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Isoka Zambia, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Aden Mwakyonde akiwa na Mstahiki meya wa jiji la mbeya wakisaini kitabu cha wageni kwa mkuu wa wilaya hiyo kwenye vikao vya ujirani mwema. Kwa taarifa yako Zambia ipo kwenye hatua za kufanya reforms za kuanzisha local govt, hawana wenzetu kule yaaani walitushangaa kishenzi

UTALII MBOZI NA MKOA WA MBEYA KWA UJUMLA HUWEZI KUMALIZA VIVUTIO VILIVYOPO

Hapa hiki kitu inaitwa Kimondo sawa sawa !!!


hii kitu inaitwa Kijungu kwa kinyakisya- au daraja la mungu
 Nia pale pale daraja la mungu pamoja na pango lake la asili
 Hapa ndipo alipobatiziwa mmisionary wa kwanza kufika Rungwe alikuwa anaitwa mwakasungula, miaka ya 1880!

MZIKI UKIKOLEA HUWA TUNABADILI STEPS

Hali ikiwa mbaya zaidi huwa tunaharibikiwa kabisa tunaanza kuwa nyani kasoro mkia! tunatembelea mikono weee baadaye watatafuta namna ua kutunyamazisha !

HIZI NDIYO MBWEMBWE ZETU WATU WA VIJIJINI

 Wakati nyie huko mijini mpaka sijui muende klabu sijui mnaita casinoni sijui  wapi siye huku vijijini burudani zetu ni hizi! waangalie wajanja wetu wakiwa wamepiga tinted halafu na jina la kijiji kwenye paji la uso wakimaanisha ni wazalendo zaidi!!! mjini utakuta mtu amevaa sijui Justin Timberland, Tupac nk huku sisi ni uzalendo zaidi!.
 Midadi ikitupanda  huwa tunamwaga radhi, sema tu mshukuru kuna watoto wanatembelea blog hii vinginevyo ningeachia tu !!!!!!!
Halafu nani kakwambia ngoma inachezwa bila wazee? lazima palipo wazee haliharibiki neno!!!

PIA KUNA MAMBO YA KALE KAMA HAYA

Hili ndilo linaloaminika kuwa jiko lililotumika miaka ya 1800 kufua chuma kwaaajili ya kutengenezea bidhaa mbalimbali zikiwemo zana za kilimo na silaha. Mambo haya yanapatikana katika wilaya ya Mbozi kata ya Kapele.

Baadhi ya mabaki ya chuma kilichotengenezwa na jiko la hapo juu kikionyeshwa na mmoja wa wazee wanaosimulia juu ya kusikia habari za jiko hilo kwa babu zao miaka ya 1916! ulikuwepo??? je tukiita watalii hizi siyo helaa????

HIII NDIYO HAZINA YA UTALII WA SILI WILAYA YA MBOZI

 Unyayo wa mtu wa kale kwenye jiwe  kubwa wenyewe wanaita jabari katika kijiji cha Nkangamo wilayani Mbozi, hizi zote ni hela tu!!!!!

Mdau wa Blog Bwana Mwakitwange akijaribu kudocument akina mama wanaotumia jabari lenye unyayo wa binadamu wa kale, kuanikia mazao yao katika kijiji cha Nkangamo

MZIGO UKIZIDI HUWA TUNABEMBEA

Huyu bwana anaonekana wazi hakula asubuhi kabla ya kuingia kwenye michakato ya kusaka noti, baada ya kuzidiwa na uzito wa mkokoteni aliamua kuomba msaada kwenye tuta eneo la Black Market Tunduma, hii ilikuwa jana asubuhi.