Sep 28, 2010

HAYA NDIYO MAJI YETU VIJIJINI TUNAKUNYWA HATUFI

EEE bwana ndiyo haya ndiyo maisha yetu vijijini tunakunywa maji wala hatuna shida, ni haya haya, tunachofanya ni kutembea na muhimbili zetu tumboni kila kopo la dawa limo tunajitibu wenyewe, unachotakiwa ni kuruhusu maisha yako yatawaliwe na mazingira siyo uyatawale mazingira kwa sababu hutaweza!!!

Halafu hatuna utaratibu wa foleni nani atangulie nani afuate, hatuna ladies first huku kila mtu ana fulsa sawa- wenyewe mnaita fulsa sawa kwa wote hata watoto wa vijijini wapo ngangali au una maoni ya kimjini mjini?