Nov 30, 2010

HAYA YOTE YAPO DUNIANI: MTOTO ALIYEZALIWA UBONGO NJE

 Hivi ndivyo kichwa cha mtoto kinavyoonekana
Matroni wa wodi ya kina mama bi. Haule akimhudumia mtoto na aliyembeba ni Bi Sabina Lyombo mama wa mtoto





Na Sekela Mwasubila, Ulanga


Mtoto mmoja katika hospitali ya Wilayani Ulanga mkoani Morogoro amezaliwa ubongo ukiwa nje baada ya kukosa ngozi ya kichwa huku akiwa mwenye afya njema.



Akiongea na mwandishi Kaimu Mganga Mkuu (W) Dkt Amani Kombe amesema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya jumatatu majira ya saa tatu usiku baada ya mama wa mtoto kujifungua mtoto huyo wa kiume hospitali hapo.



Aliongeza kuwa hali ya mtoto kuzaliwa na kukosa ngozi ya kichwa hutokea wakati wa uumbaji wa viungo mbalimbali vya mwili wa mtoto na hali hiyo huweza kusababishwa na ukosefu wa madini mbalimbali kwa mama wakati wa ujauzito aidha ni tukio la kwanza kutokea katika hospitali hiyo ya wilaya.





Naye mama wa mtoto bi. Silvia Lyombo (20) ambaye ni ujauzito wake wa kwanza alisema kuwa hakupata matatizo yoyote ya kiafya wakati wa ujauzito na alijifungua katika hali ya kawaida mtoto mwenye uzito wa kilo 2.9 na kuwa ananyonya kama kawaida na hana tatizo lolote zaidi ya kukosekana kwa ngozi ya kichwa aidha hakuna dawa zozote ambazo alizitumia katika kipindi chote cha ujauzito wake.



Hata hivyo wataalamu wa hospitali ya wilaya walisema kuwa watampeleka mtoto huyo katika hospitali kubwa mkoani Morogoro kwa uchunguzi zaidi wa nini kifanyike kukabiliana na tatizo la mtoto huyo ambaye hadi sasa yupo hai na afya njema.



indaba2010