Na Danny Tweve
Iringa.
Shirika la kazi duniani tawi la Tanzania limetaja Tanzania kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI kutokana na kupitiwa na barabara kutoka nchi zenye kiwango cha juu cha maambukizi.
Akizungumza kwenye mafunzo ya waelimisharika wa masuala ya mapambano dhidi ya UKIMWI katika maeneo ya Kazi,
Mratibu wa Mradi wa Kuongeza Uwezo wa kiuchumi na Kupunguza hatari ya Maambukizi kwenye Njia za Usafirishaji kwa chini ya ILO upande wa Tanzania Bi Tulanoga Matimbwi ameeleza hayo jana mjini Iringa wakati akielezea mwelekeo wa mradi huo.
Amesema wakati Tanzania kwa upande wake kiwango cha maambukizi ni 5.7% nchi zinazolisha(feed) barabara kuu ya TANZAM zina maambukizi makubwa hii ikienda sambamba na barabara ya Dar es Salaam hadi Namanga.
Alitolea mfano kuwa nchi zilizo kwenye ukanda wa barabara ya TANZAM hali ya maambukizi ni kubwa kuanzia Zambia ambako kiwango cha maambukizi ni 15.03%,Malawi 14.02%,Zimbabwe 24%,Afrika Kusini 18% Botswana 23.9% na Msumbiji 12%.
Kutokana na hali hiyo amesema ni muhimu kuimarisha jitihada za kukabiliana na maambukizi mapya kwenye vituo vinavyopitiwa na barabara hizo kuu, ili kupunguza madhara ya mwingiliano huo.
Ameainisha kuwa uelimishaji katika mipango yake unalenga zaidi kwenye maeneo ya kazzi katika sekta binafsi na sekta ya umma na kwamba kupitia miundo iliyopo katika ngazi za wilaya itawezesha kufanikisha mapambano hayo.
Mafunzo hayo yanahusisha washiriki kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Dar es Salaam na NJORUMA na wengi wao ni kutoka asasi zinazojengea uwezo vikundi vya kijamii, waratibu wa UKIMWI na maafisa ushirika.
Baada ya dozi hii nawatakia kilalakheri katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe mosi Decemba, Mungu awabairi na kuwajaza nguvu wale wote wanaopata huduma majumbani na wanaopata dawa katika maeneo mbalimbali nchini mwetu na duniani kote. Mchango wenu katika maendeleo ya nchi bado tunautegemea msikate tamaa tupo pamoja nanyi katika kuhakikisha kuwa afya zenu zinaendelea kuimarika kwa kuimarisha huduma za tiba majumbani lakini pia katika kliniki za CTC. ahsante
indaba2010