Nov 9, 2010

WATOTO WANNE WAJIFICHA UVUNGUNGI MWA HOOD NA KUSAFIRI HADI DAR

Basi la Abood lenye namba za usajiri T542 AZE limenusurika kupata ajali jana baada ya Watoto wane wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya, kujificha na kukalia mdumowa breki kwenye chesisi ya basi hilo na kusababisha mfumo wa breki kushindwa kufanya kazi.


Habari kutoka kwa mmoja wa abiria waliosafiri na basi hilo Bwana Edmund Makombe na kuthibitishwa na kondakta wa basi hilo bwana Ayoub Nassoro, Watoto hao walikuwa wamejilaza kwenye mfumo wa breki na wengine kwenye chasis.

Imeelezwa na watoto hao kuwa walipanda waliingia kwenye basi hilo alfajiri katika kituo kikuu cha mabasi cha Mbeya na kujificha uvunguni kwenye chasis ambapo mmoja wao alijilaza kwenye waya za breki, na kwamba wakiwa karibu na hotel ya aljazeera iliyopo Ruaha Mbuyuni walishitukia dereva akisimamisha gari kwenye moja ya maeneo yanayofanyiwa matengenezo.

Kwa mujibu wa Kondakta wa basi hilo Ayoub Nassoro maarufu kama Nyerere , anasema wakati gari limesimama kwaajili ya kusubiri magari kupishana alienda kuchungulia uvunguni kwaajili ya kuangalia hali ya tairi na ndipo alipowakuta watoto wawili wakiwa wamekilaza kwenye difu ya nyuma.

Anasema kuwa baada ya kuwatoa hao wawili, walimweleza kuwa wapo wengine uvunguni humo na katika kuchugulia wakawakuta kwenye chasis huku mmoja akiwa ameshikilia waya za mfumo wa breki.

Watoto hao wamejitambulisha kwa majina ya Frank John (12), Fabi Yusuph (12), Christopher Tweve (10) na Yohaba Robart (12) wote wakazi wa Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya.

Wakizungumza katika hoteli ya Aljazeera ambako walinunuliwa chakula na wafanyakazi wa kampuni ya Abood na baadaye kuachwa ili warejeshwe mbeya na mabasi yanayoelekea Mbeya , wamesema sababu za kurtoroka kwao ni kutokana na hali ngumu ya maisha na kwamba walitegemea kwenda Dar es salaam kutafuta maisha.


Wanadai kuwa tayari kuna wenzao ambao wameshasafiri kwa utaratibu huo na kwamba hawana mawasiliano ingawa wanaamini wapo Dar es salaam na huenda wana maisha mazuri ndiyo sababu wakashawishika nao kwenda huko.
Licha ya kondakta kuelezea kuwa gari lilisimama katika utaratibu wa kawaida wa kulichunguza, mmoja wa abiria ambaye alikuwa karibu na kiti cha dereva anaeleza kuwa alimsikia dereva akimwelekeza kondakta huyo aangalie kwenye mfumo wa breki baada ya kubaini kuwa mzito tofauti na siku zingine.

Anaesema akiwa anaagalia uvunguni alibaini kijana huyo akiwa amejilaza kwenye waya wa breki na ndipo alipotoa taarifa kwa dereva kuwa kuna watu uvunguni.

Mashuhuda wa tukio hilo wameonekana kushangazwa na ujasiri wa watoto hao ambao wakati wakitolewa uvunguni walikuwa wamechafuka sana kutokana na vumbi la uvunguni kuwatanda usoni huku wakiwa wamechoka.