Jan 30, 2011

Makamu wa Rais awa Mgeni rasmi katika Mahafali ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam leo

Makamu wa Rais awa Mgeni rasmi katika Mahafali ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam leo: "
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitunuku Shahada, Stashahada na Vyeti kwa wahitimu 445 katika ngazi ya Uhandisi Kompyuta, Uhandisi Ujenzi, Uhandisi Umeme, Uhandisi Elektronik, Mawasiliano ya Anga, Uhandisi wa Mitambo ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara kwenye Mahafali ya Nne ya Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Taasisi hiyo Upanga Dar es salaam. Kulia Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa J.W.A.Kondoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimpongeza Mwanafuzi J. Mgaya Mhitimu Bora kwa mwaka 2010- 2011 katika Taasisi ya Teknologia ya Dar es salaam kwenye mahafali ya nne ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Taasisi hiyo Upanga Dar es salaam, ambapo jumla ya Wahitimu 445 katika ngazi za Uhandisi Kompyuta, Uhandisi Ujenzi, Uhandisi Umeme, Uhandisi Elektronik, Mawasiliano ya anga, Mitambo ya sayansi naTeknolojia na Maabara walitunukiwa Shahada Stashahada na Vyeti.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiongoza maandamano ya wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam katika Mahafali ya nne ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Taasisi hiyo Upanga Dar es salamm. Kwenye Mahafali hayo Jumla ya wahitimu 445 wa ngazi mbalimbali walitunukiwa Shahada, Stashahada na Vyeti. Kushoto Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa J.W.A. Kondoro, kulia Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Profesa Mshoro
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, Waziri wa Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa wa pili kushoto, Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia wa Dar salaam Profesa J.W.A Kondoro kushoto, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Profesa Mshoro, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi hiyo kwenye Mahafali ya nne ya kutunuku Shahada Stashahada na Vyeti, yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Taasisi hiyo Dar es salaam.
"