Jan 28, 2011

RAMADHAN NASSIB AOMBA FIFA IISAIDIE TFF KUPATA MASHINE ZA KUKATIA TIKETI.

RAMADHAN NASSIB AOMBA FIFA IISAIDIE TFF KUPATA MASHINE ZA KUKATIA TIKETI.: "
Makamu wa pili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF Bw. Ramadhan Nassib akifunga rasmi kozi ya FIFA EVENT MANAGEMENT COURSE ambayo imefanyika kwa Siku tano na iliandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. Katika Kozi hiyo Wadau mbalimbali wameshiriki na kupata vyeti wakati wa kufunga semina hiyo akizungumza wakati wa kufunga kozi hiyo Makamu wa Rais wa pili wa TFF Ramadhan Nassib amesema 'Tunashukuru kwa FIFA kutusaidia mafunzo haya tumeyapata mengi na nadhani yatatusaidia sana katika kuandaa matamasha yetu ya mpira wa miguu hapa nchini'. Ramadhan ameomba FIFA kuisaidia TFF katika suala zima la kupata mashine za kuuzia tiketi kwani suala la tiketi hapa nchini ni tatizo sugu ambalo limekuwa likileta matatizo mengi katika masuala ya mpira wa miguu, 'Tunao uwanja mzuri lakini suala la tiketi ni tatizo kubwa' amesema Ramadhan Nassib tutashukuru kama FIFA itatusaidia.
Mkufunzi Windsar John Kutoka FIFA akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kozi ya FIFA Event Management Course iliyokuwa ikifanyika kwenye Hoteli ya TANSOMA jijini Dar es salaam wadau mbalimbali wa masuala ya mpira wa miguu nchini wamehudhuria katika kozi hiyo. Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF Bw. Boniface Wambura akipokea cheti mara baada ya kuhitimu kozi ya mafunzo ya Jinsi ya Kuandaa Matamasha ya Mpira wa Miguu iliyoandaliwa na FIFA, kozi hiyo imemalizika leo. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania TFF Bw Angetile Osiah akipokea cheti chake mara maada ya kuhudhuria kozi ya FIFA iliyomalizika leo kwenye Hoteli ya TANSOMA jijini Daqr es salaam. Mkuu wa Msoko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF Bw. Jimmy Kabwe akipokea cheti chake mara baada ya kumaliza kozi ya FIFA iliyofanyika kwenye hoteli ya TANSOMA jijini Dar es salaam kozi hiyo iliandaliwa na FIFA na ilikuwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kuandaa matamasha ya mchezo wa mpira wa miguu. Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude ambaye alikuwa ni mmoja wa washiriki wa kozi hiyo akipokea cheti chake kutoka kwa Windsar John Mkufunzi kutoka FIFA wengine wanaoshuhudia ni wakufunzi kutoka FIFA. Washiriki wa semina ya kuandaa matamasha ya mchezo wa mpira wa miguu iliyoandaliwa na FIFA wakifuatilia kwa makini wakati semina hiyo ilipokuwa ikiendelea
"