Jan 28, 2011

ROLI LAMWAGA PETROL WANANCHI WAJICHOTEA

Dalili za watu kupoteza matumaini na kuamua kushiriki katika kukoka moto wa petroli kwenye makazi yao leo zimeendelea kujidhihirisha katika kijiji cha Senjele baada ya roli lililoanguka kushambuliwa kwa ndoo za kujichotea petrol.
Gari lililoanguka ni mali ya kampuni ya Hans Company yenye anwani zake Dar es salaam ingawa makao makuu ya kampuni hiyo yanadaiwa kuwa Kenya.
Namba za roli hilo lililoanguka ni  T 322 BLW na Trela lake lenye namba za usajiri T541 BKD lilikuwa likiendeshwa na Dereva mwenye asili ya Kisomali ambaye hata hivyo hawezi kuzungumza kiswahili wala kingereza.
  Habari za kiuchunguzi zimewahusisha baadhi ya walinda amani kujihusisha na ubebaji wa petroli hiyo na kujaza kwenye mapipa na baadaye kuiuza kwa mmoja wa dalali aliyekuwepo kwenye eneo la Tukio aliyetajwa kwa jina moja la Luhandi.
Taarifa zaidi zitawajia