Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya SMS Kati ya Wananchi wa Bumbuli na Mbunge wao, Ndugu January Makamba, yamezinduliwa tarehe 29 Januari 2011 kwenye Semina Elekezi aliyoitisha Mbunge huyo kwa viongozi na watendaji wa vijiji na Kata wapatao 250 wa Jimbo la Bumbuli.
Mfumo huo utaanza kutumika tarehe 10 Februari 2011, baada ya kipindi cha elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya mfumo kuu kukamilika.
Kwa kifupi, wananchi wanapaswa kutuma kero, maoni na ushauri kwa Mbunge ambaye kila siku, yeye na wasaidizi wake, watakuwa wanasoma meseji hizi na kuwajibu au kuwatafutia majibu.
Kama kuna taarifa za haraka ambazo inabidi Mkuu wa Wilaya au Mkurugenzi wa Halmashauri, au Mkuu wa Polisi wa Wilaya au Bwana Afya inabidi azijue, basi Mbunge atasaidia kuzifikisha kwa haraka zaidi.
Huduma hii haiondoi haja ya Mbunge kuendelea kutembelea Jimbo na kuonana na watu wake. Ni kwamba, simu au SMS, kama njia rahisi ya mawasiliano, hakuna haja ya kuacha kuitumia wakati wananchi wenyewe wanaitumia sana.
Mazungumzo kati ya Mbunge na mitandao ya simu imewezesha kufanya gharama ya huduma hii iwe 'at cost' na hivyo Mbunge bado kuwa na uwezo wa kuigharamia kwa nusu ya posho yake (wapo Wabunge ambao wamejitolea nusu mshahara kwa jambo moja au jingine - lakini kwa Mbunge wa Bumbuli hili ni muhimu).
Kwa habari nyinginezo tembelea tovuti ya Mbunge:
http://www.januarymakamba.com/
"