Feb 2, 2011

Mama Salma Kikwete katika kikao cha Wake wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika

Mama Salma Kikwete katika kikao cha Wake wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika: "
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akihudhuria mkutano wa mwaka wa wake wa marais na wakuu wa nchi za Afrika unaofanyika nchini Ethiopia tarehe 31.1.2011.
Mama Salma Kikwete akishauriana jambo na wasaidizi wake Bibi Neema Mhada (kushoto) na Ndugu Daud Nassib (katikati) wakati wa kikao wake wa Marais na wakuu wa nchi za Afrika.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama Yoo Soon-Taek muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika (OAFLA) kinachofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 31.1.2011.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mama Callista Mutharika, mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Bingu wa Mutharika wakati wa kikao cha wake wa marais wa Afrika huko Addis Ababa tarehe 31.1.2011.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa,WFP, Dr. Sheila Sisulu wakati wa kikao cha wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika kinachofanyika Addis Ababa tarehe 311.2011.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wao Bibi Azeb Zenawi wakati wa kikao chao huko Addis Ababa tarehe 31.1.2011
"