Feb 28, 2011

ULIPUAJI WA MABOMU KUFUATIA MAKAMBAKO

Na Frederick Siwale , Makambako Iringa.
SERIKALI Wilayani Njombe imetoa tahadhari kwa wananchi kuhusu ulipuaji wa mabomu ambao utafanywa na askari wa Jeshi la wananchi Tanzania kikosi cha KJ 514 unaotarajia kuanza leo na kumalizika machi tano mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sarah Dumba amesema,hayo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini makambako akiwatahadharisha kuhusu zoezi la uliopuiaji wa mabomu katika kikosi hicho utafanyika katika  kijiji cha Katenge, na kwamba zoezi hilo ni la kawaida ambalo linafanywa kwa usalama na utaalamu wakijeshi.
Bi. Dumba amesema, taarifa za ulipuaji mabomu zilitolewa  na viongozi wa JWTZ ilitolewa kwa lengo la kuwatoa hofu wananchi hususani katika kipindi hiki ambacho wananchi wapo katika cha mshtuko kutokana na tukio la hivi karibuni ambapo milipuko ya mabopmu ilisababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali huko Gongo la Mboto Jijii Dar es salaamu.
Amesema wananchi wanapaswa kuhakikisha katika siku hizo ambazo zimtangazwa kutofanya shughuli zozote katyika maeneo ya poli ambalo linakaribiana na eneo ambalo limetengwa kwaajili ya ulipuaji mabomu.
Amesema mabomu hayo ni ya milipuko mikubwa na midogo kwa hiyo wananchi wachukue tahadhari kuepukana na athari ambazo zinaweza kujitokeza  kwa wananchi na mifugo yao, ambapo hawqatakiwi kuendesaha shughuli zozote kwa siku hizo tano.
Taarifa za kuwepo kwa ulipuaji mabomu katika kikosi cha  cha JWTZ Makambako zilisababisha hofu katika jamii ambapo tayari wananchi walishaanza kupata woga na wengi wao hawakuwa na taarifa zozote kutoka serikalini hadi pale serikali ilipotangaza rasmi kwa kutumia mabango na mikutano ya hadahara, misikitini na makanisani pamoja na shuleni na katika maeneo mbalimbali.