| Nimejiunga na TANU tangu mwaka 1966, mimi ni mwana CCM tangu
kuanzishwa kwake  1977 na ni mjumbe wa NEC
Sina uhusiano mbaya na UVCCM, sina uhusiano  mbaya na yeyote ambaye ni
mwana CCM.
Napenda kuongelea kuhusu 2015,  sijaamua kama nitagombea au sitagombea
Wananchi ndio wenye uwezo wa kila  jambo katika nchi, wananchi ndio
wanaopiga kura na ndio wanaoamua nani awe  kiongozi na nani asiwe.
Makundi matatu yanayoamua nani awe kiongozi ni  WANANCHI, CHAMA
anachotoka mwanasiasa na DOLA
Kwanini  nimewaita?
Kumeibuka malumbano ndani ya CCM na UVCCM kutokana na matamshi  ambayo
yanakanganya na mimi ni mmojawapo ambaye nimeshambuliwa  sana.
Nipo hapa kwa niaba yangu mwenyewe, sijatumwa na yeyote na  SIMSEMEI
YEYOTE. Nipo hapa kama Frederick Sumaye.
Ningeyapeleka kwenye  chama hasa NEC lakini kwakuwa na wenzangu
wameanza kwa mtindo wa kuitisha  vyombo vya habari nami nafuata
utaratibu huo
Lengo si kushindana wala  kupimana nguvu, lengo ni kuweka uwazi kwa
wananchi watambue  uhalisia
Baada ya kuona wananchi wanavyoyapokea maandamano ya CHADEMA na  kwa
hamasa kubwa nilishauri CCM itoe ushirikiano kwa serikali kwa  kuyajibu
wanayotoa CHADEMA ili kuweza kuweka hali halisi. Mimi kusema  CCM
ifanye sikumaanisha MIMI SIMO.
Aidha, sijasema serikali isifanye  kazi yake. Waziri Wassira amefanya
kazi ya serikali vema tu
Katika  utaratibu wa kawaida, chama kinafanya kazi yake baadae serikali
inakuja  kumalizia yanayobakia. Kama kazi ya siasa haijafanyika vema na
chama basi  serikali hubeba lawama zisizostahili.
Malumbano ya kisiasa hujibiwa  kisiasa, CCM walitakiwa kuwajibu CHADEMA
na si kazi ya serikali kufanya kazi  ya kisiasa
CCM inafahamu kazi ya kisiasa na kimekuwa kikifanya hivyo  tangu
zamani. Viongozi wetu wamekuwa wakifanya hivyo kwenye kila ngazi.  Ni
shughuli ya chama na haihitaji maamuzi ya vikao.
Akiongea Sumaye  linaonekana tatizo kubwa na tena ni utovu wa nidhamu.
Nimeshutumiwa na hata  kutukanwa na wengine ndani ya chama
Nifafanue:
Nimeshutumiwa kuwa  namshutumu mwenyekiti wa chama. Nilijibu nikadhani
mambo yameisha kumbe ndo  kwanza yameanza.
Nimeshutumiwa na UVCCM Pwani kuwa - Sumaye na Lowassa  wana mpango wa
kukivuruga chama ili wafikie malengo yao 2015
Kama  Lowassa na Sumaye wanautaka urais 2015, kwanini washirikiane?
2015 kutakuwa  na marais wawili?
Hakuna sehemu hata moja ambapo niliwahi kumtaja rais  katika maongezi
yangu, madai kuwa namtukana na kumchafua rais ni tuhumu za  uwongo
kabisa
UVCCM wanadai sisi tumeshiba na sasa tumevimbiwa...  Tuwaache nao wale
kama sisi.
Haya ni matusi na kejeli na inasikitisha  sana
Ina maana UVCCM wana mgombea wao ndo maana wengine tunaonekana  kero
kwao kwani tunamvurugia mtu wao. Vijana wenye tamaa ya KULA ni  hatari
kwa taifa
Eti vijana wanataka wamweke mtu wao ili wale?  Imenishtua sana!
Wanadai tunakibomoa chama, wanadai kuwa tunataka rais  atoke kaskazini.
Kwa madai yao nchi itaendelea kusonga mbele na wanatupa  pole
tunaodhani rais lazima atoke kaskazini.
Ubaguzi huu wa ukanda  tena kutoka UVCCM mkoa wa Pwani usipochukuliwa
hatua utalipeleka pabaya  taifa!
UVCCM wana mpango wa kupambana kina Sitta na Sumaye. Wanataka  hawa
wasipewe nafasi katika chama, wanadai watapigana ndani na nje ya  chama
kuhakikisha watu hawa hawapewi nafasi.
My comment:
Sitta  yashaanza kumkuta ya UVCCM huko Tabora!
Kuna maoni mengine yanaweza kuwa  na athari kwa chama hivyo ni juu ya
kiongozi husika kuangalia athari ya kutoa  maoni husika.
Serikali yoyote iliyochaguliwa kidemokrasia LAZIMA itasemwa  na
kukebehiwa. Kiongozi yeyote na chama chochote  kilichochaguliwa
kidemokrasia, kitasemwa na watu watakikebehi. Si  ajabu
Nimeshtushwa SANA na kauli ya UVCCM mkoa wa Pwani kuwa suala la  rais
ajaye 2015 lipo mikononi mwa rais Kikwete! Hili linanishtua,  siamini
kama rais Kikwete anamjua rais ajaye 2015
Sasa hivi mtu yeyote  akiongea ndani ya CCM ataambiwa anautaka urais,
hii inaweza kuwaziba wengi  midomo
Nawaomba watanzania, yeyote atakayejaribu kutumia njia za  udanganyifu
kwa RUSHWA, KUTENGANISHA WATU, tumkatae kwa nguvu  zote
Tunakosa muda wa kujielekeza katika mambo ya msingi tunaanza siasa  za
kupakana matope - Sumaye
Nategemea nimeeleweka, sitarajii kuibua  malumbano na sitarajii kurejea
kuongea na waandishi juu ya hili. Mimi ni  mwana CCM na sipo chama
chochote cha siasa zaidi ya hiki.
Mungu  Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
MASWALI
SWALI:  Kwanini hujaandika barua CCM?
JIBU: Mimi sijaandikiwa barua, sijibu kwa  barua
SWALI: Mtu akikutukana ujue KATUMWA NA BABA na ndo maana  baba kakaa
kimya. Kwanini usijiondoe CCM?
JIBU: Ukiona mtoto  anamtukana mtu mzima uelewe ametumwa ama
anamtukanisha mtu mzima lakini kwa  hili la sasa yote yamo. Maana
hatujakaa kutuma vijana. Siwezi kutoka CCM  sababu ya vijana
SWALI: Toka miaka ya 70 kwanini watu wa kaskazini  wanasemwa vibaya?
Hawafai? Toa ufafanuzi kuhusu kauli yako ya 2005 kuwa  ATAKAYEINGIA KWA
KUCHAFUA WATU KWA KALAMU ATATUMIA VISASI  kuongoza.
JIBU: Nilishasema awali, ubaguzi wa kimaoeneo ni hatari sana na  si kwa
kaskazini tu. Kuhusu suala la U-Kaskazini haina maana maana  haijawahi
kutoa rais hata akitokea Bagamoyo leo akawa anafaa hakuna  neno.
Tusitazame watu kwa wanakotokea ama dini zao na rangi zao.  Hata
bungeni kuna kauli za kibaguzi, tumezikemea bila kujali  eneo.
Pili, ya 2005: Ni tabia mbaya kuchafuana hata kama ni  udiwani,
niliyasema na bahati hayajatokea.
SWALI LA KUBENEA: Vijana  wamejitokeza kutetea mafisadi, unatoa rai
gani? Lakini ultimatum wanazotoa si  sahihi, labda watoe ushauri.
JIBU: Vijana wanatetea mafisadi ama nani,  sijui... ila misemo yao
inanitisha
SWALI LA BBC: Imejitokeza  kuzungumza mambo ya chama nje ya chama, kama
chama mnalionaje hili  haliwaaibishi?
JIBU: Future ya CCM ni nzuri ila kuna mambo LAZIMA  yafanyike. Yale
madhaifu lazima tuyaondoe.
kutoka www.mjengwa.blogspot.com |